Bunge lamjibu Mbowe, ladai pesa wametuma hospitalini tarehe 20 Sept sababu hawakuwa na akaunti ya hospitali

Kaka haya masuala si ya kucheka kaka, ni masuala ya kuwakemea na kuwananga kwa nguvu zetu zote. Hili ni jambo la kufa na kupona kwa maisha ya Lissu na yetu pia. No time to waste bro...
Sicheki kwa furaha bali huzuni kuu kutokana na matendo yanayoendelea yasiyo ya kiutu yakiongozwa na uongo ulio dhahiri ambao tunalazimishwa tuuamini huku tukiendelea kupoteza upendo baina yetu na kuogopana kutokana na matukio na matamko. Je kizazi chetu kitarithi nini ikiwa tunatakiwa kutoukataa uongo na kupongeza uzandiki pindi utamkwapo na wenye mamlaka?
 
Halafu kwamba ni emergence wanajua sana tu... NIMSHUKURU YULE MBUNGE ALIYEDHAMINI GHARAMA ZA NDEGE maana ile alirespond very positive kwenye emergence situation...

Yaani...
1. Unakusanya hela halafu unakaa nazo huku ulijua LISU ana risasi kadhaa mwilini
2. Unaandika barua isiyo na sahihi ya yeyote
3. Unathubutu kujieleza eti ulikuwa unatafuta akaunti
4. Unakaa na hela muda wote huo, je kama ingekuwa ndo HELA PEKEE INAYOSUBILIWA KUOKOA MAISHA YA LISU, angekuwepi leo..??

HII NCHI TUNAHITAJI KUBADIRIKA KWA KIASI KIKUBWA.. KUANZIA VIONGOZI HADI WANANCHI
Najiuliza tukihoji ni kwanini mpaka sasa Mhe. Spika Ndugai kiongozi wa bunge na ofisi yake hawajafika Kumuona Tundu Lissu sijui watakuwa na majibu gani?
 
Kuna wakati acheni akili za kushikiwa... HAO ULIOWATAJA HAKUNA MWENYE TAARIFA ZA ULIPWAJI WA HELA HIZO...!!

Yaani mchango wa matibabu ya LISU lijue bunge tu kwamba limelipa..!!! AU BUNGE LIMEJILIPA KWENYE AKAUNTI YAKE....??!
Wwe ndo umeshikwa akili mpumbavu.... Hospital iliulizwa kwamba wamepokea hela wakasema hawakuona? Mbowe ametoa breakdown ya fedha zilizopokelewa kwa account ya CDM tu kwasbb ndo ana access nayo hii ya hospital atajuaje kama kuna hela imeingia. Spika alinusa harufu ya ufisadi kwenye hizo fedha zinazochangwa kupitia account ya CDM akaamua kuzituma moja kwa moja hospital. ssa hapo tatizo lipo wp? Si waulize hospital kama kuna fedha imeingia ili iendelee kutumika kwenye matibabu. Mijitu mingine unyumbu umewaingia kwenye damu mpaka mnatia hasira. Yaani hamuwezi kutumia hata common sense ya kawaida tu kuhoji vitu vyepesi kama hvi mpka msubiri muambiwe.

Tena baada ya conference ya leo ilibidi muombe risiti muone kama kweli hizo fedha mlizoambiwa zimetumika zililipwa hospital au hata muone invoice.
 
Bunge mmefanya jambo jema, Hakuna mtanzania mwenye akili timamu na anaye jua udhaifu wa mwenyekiti wa chama juu ya pesa na kumtumia fedha.

Na hata sasa fedha ikichangwa baadae utasikia alikikopesha chama katika kumhudumia mgonjwa na anataka alipwe.
Ayo ameshayafanya sana na ndiomaana Bunge walikua macho. Bora fedha zichelewe lakini zifike sehemu salama.
 
1.Ni aibu sana na kitu ambacho hakiwezekani kwa taasisi kubwa kama bunge kuhangaika kupata mawasiliano na akaunti ya hospitali husika, na kwamba hawajui taratibu za malipo nje ya nchi..!!!

2. Statement ya Mbowe kwamba "............pamoja na kwmb aliomba akaunti ya hospitali aziingize......." inaonesha kwamba ALIOMBA AKAUNTI NA AKAPEWA, ila hakuziingiza.

Daaah....!!!
 
Ofisi ya bunge ilimuuliza mbowe jinsi ya kuzituma hizo fedha,na Mbowe akawaambia watume ktk akaunti ya chama,lakini ofisi ya bunge ikakataa na kumtaka Mbowe atume akaunti ya hospitali,Mbowe alifanya hivyo.Hii ni kwa mujibu wa Mbowe mwenyewe,akiongea na viongozi wa chama Leo hii. Sasa swali ni kwanini walimpigia Mbowe simu na kumuuliza nia yao ya kutuma pesa?Pili kwanini walipotuma hawakumwambia kuwa tayari zimetumwa?Je kulikuwa na sababu ya kisayansi iliyosababisha mgonjwa mahututi kucheleweshewa fedha za matibabu?Hapa kuna jambo la kujifunza.
 
Jamani mie hata aongeee Mkuu wa nchi na ikagongwa mihuri yote ya taasisi za serikali kwa hili la Lisu serikali haisafishiki.

Mbowe akihutubia nimejikuta naumia utadhani naona kila tukio lililompata Ndg TL, jamani nimetambua uwezo wa watawala wetu ni wa kupingwa na kila mwenye akili timamu.

Hoja za Jana za mh Zitto na hotuba ya mh Mbowe ya leo imenifanya niione serikali haina mpango mzuri na taifa hili.

From today:nimeona viongozi wa watawala walivyo jaa ukatili na hawana huruma hata kidogo,kibaya wanakazana kusema tuwaombeee, hivi ni Mungu yupi huyo wanaotaka tuwaombeee?

Eeh Mwenyezi Mungu naomba umponye ndg yetu Tundu Lisu katiba jina la YESU KRISTO,kila asomae Hapa na aseme Amina.
Amina
 
HAIWEZEKANI ULIPE, halafu uwe na taarifa wewe mlipaji pekee...

Halafu hayo ni maandishi tu

Na tusisahau ndege iliyompeleka Lisu Nairobi alisema HELA KATOA MBUNGE WA CCM.... MA MARA IKAWA PAAP CCM IKAMWANDIKIA BARUA YA KUMPONGEZA wakati Nyalandu kwa msaada alioutoa kwa watoto wa LUCKY VICENT HAKUANDIKIWA CHOCHOTE
Nyalandu naye chadema? nini
 
Back
Top Bottom