Bunge lakubali Hoja ya Mnyika dhidi ya CCM kutumia fedha haramu kwenye uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge lakubali Hoja ya Mnyika dhidi ya CCM kutumia fedha haramu kwenye uchaguzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Serayamajimbo, Feb 3, 2012.

 1. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnyika ametoa hoja kuwa Sheria ya fedha haramu iingizwe kifungu cha msajili wa vyama kudhibiti fedha haramu kwenye vyama na uchaguzi. Alisoma ripoti ya utafiti Fulani (sikupata jina vizuri) wenye kuonyesha CCM ilivyotumia fedha haramu za EPA Kagoda, Tangold, Deep Green na Meremeta. Akapendekeza kifungu kipya katika sheria ili ufisadi huo usijirudie. Mwanasheria Mkuu Werema akamuunga mkono na bunge likapitisha.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  wanapitisha lakini utekelezaji wake ni zero.
  Rais, waziri mkuu wanavunja sheria na katiba hakuna wa kuwasurubisha basi ujue hamna lolote!
   
 3. Y

  Yetuwote Senior Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bora sheria iwepo na wao waivunje. Hiki kitakuwa kgezo cha kuwashitaki baada ya kipindi chao.
   
 4. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  alafu hawa jamaa hawajasema walitumia shiling ngapi kwenye uchaguzi 2010
   
 5. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Hayo yote hayana faida kwa mlalahoi kama mimi.
   
 6. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uongo mwingine umepitiliza kipimo cha uongo
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Viva to mnyika kwani ukitaka kumchezea simba sharubu unaanza kumkuna mkia kisha mgongo mpaka kuzifikia sharubu so soon tutawang'oa
   
 8. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wabunge wakiwa bungeni hoja wanazotoe sio za vyama wanavyotoka ni hoja za taifa, hakuna hoja ya bunge au chama anachotoaka
   
 9. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Tutawaondoa madarakani nakuwawajibisha soon nawaesabia siku zao
   
 10. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sioni ubaya ni jambo jema kwa afya ya taifa letu.
   
 11. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nikumwomba Mungu atujalie tupate rais anaesimamia haki na sheria na kufuata sheria
   
 12. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #12
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bora na wewe umeona, sijui waliishia katikati!
   
 13. m

  mopaomokonzi JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mnawaondoa kupitia jf. Labda mnawaondoa ndani ya jf
   
 14. theophilius

  theophilius Senior Member

  #14
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  sheria ya fedha haramu ipo siku nyingi, na msimamizi wake mkuu ni BOT lakini ndio wao waliokuwa wakitoa ruhusa benki kupitisha fedha haramu za EPA, hata zilipostukiwa na mabenki: kwa msajiri wa vyama vya siasa, sijui atatumia ujasiri upi wasiokuwanao BOT!
   
 15. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #15
  Feb 3, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,496
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  Haita kaa hata siku mija uyaone kwa staili hiyo mkuu! Yaani watu wachote mahela ya wizi mahali waje wahonge wapinga kura wewe unaona hutapata faida?! pole!

  Naona faida nzuri utakayoipata ni kutoka kwenye posho za wabunge zilizoongezwa kwani tumeambiwa tutakuwa tunapewa tukiwaomba barabarani!
   
 16. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #16
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mnyika Jembe la ukweli, Big up mh.
   
 17. M

  Makupa JF-Expert Member

  #17
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Zitto amka mwenzako anafikiria mbali wewe umebaki kufanya siasa za kujitafutia umaarufu binafsi, siku zote ni nchi kwanza acha double standard kuna shirika moja la hifadhi ya jamii mbona uko nalo karibu sana kuna nini
   
 18. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #18
  Feb 4, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Nadhani uamuzi wa Zitto kumwachia Ms. Lissu asome hotuba ile ili yeye Zitto apate nafasi ya kuelezea mengine kwa mapana ulikuwa ni uamuzi wa busara sana. Lakini kwa bahati mbaya Zitto hakuwa na muda wa kutosha, na pia hapakuwepo wabunge wengine ambao ndani ya muda wao, wangezidi elimisha umma juu ya tatizo hili, kwani Lissu na Zitto hawakuwa na muda wa kuyamaliza yote.

  Pamoja na mapungufu haya yote, Ms Lissu na Zitto wamefanya kazi nzuri sana. Tofauti na hotuba ya Lissu, Hotuba ya Mkullo ilipwaya sana. Lissu alifanya kazi nzuri kuelezea umma kuhusu mchakato mzima wa jinsi gani fedha haramu zinazaliwa mpaka hatua ya kuwa fedha halali. Zitto nae alielezea mengi mazuri, e.g. alihimiza umuhimu wa kuanzisha a "Real Estate Regulator", ili kupunguza kasi ya mafisadi kujenga majengo makubwa kiholela holela kwa nia ya kusafisha fedha zao. Tahadhari aliyotoa Zitto kuhusu hili ni muhimu sana - kwani ni kweli wahusika hawawekezi kwenye ‘Real Estate' kutokana na mahitaji ya soko, bali kutokana na ‘interest' zao za muda mfupi zenye kulenga kusafisha fedha zao, na kazihii ikikamilika na baadae nguvu ya soko kujaza nafasi hii, itakuwa balaa. Zitto pia alifafanua vizuri jinsi gani fedha hizi zinachangia kuporosha shillingi yetu dhidi ya dolla, jinsi gani vijana wanaingizwa katika uhalifu wa madawa ya kulevya n.k.

  Kuna mambo mengine muhimu ambayo kina Lissu na Zitto hawakuwa na muda wa kutosha kuyazungumza ili wananchi waelewe kwa undani zaidi juu ya athyari za tatizo hili. Kwa mfano:

  1. Madhara ya fedha hizi katika chaguzi zetu za vyama na pia chaguzi kuu. Nje ya madawa ya kulevya, binafsi nadhani madhara kwa chaguzi kuu ni makubwa kwa wananchi kuliko mengine kwani haki ya wananchi inaporwa na nguvu ya fedha, na kupelekea wananchi kuchagua viongozi wahalifu ambao ni sumu kubwa kwa uchumi wetu na mustakabali wa taifa. Huko nje wanaongelea tatizo kigaidi zaidi, lakini kwetu, tatizo zaidi ni hili la uvurugaji wa demokrasia.

  2. Fedha chafu zinavuruga maamuzi ya kibiashara katika uchumi wetu. Maamuzi kuhusu mikopo, uzalishaji, uwekezaji n.k hayaendani na hali halisi ya soko na uchumi kwa ujumla kwani fedha hizi sio rasmi.

  3. Magendo mengi ya bidhaa mbalimbali, kama vile chakula kupelekwa nje, wafanyabiashara kuficha mahindi na sukari ili kufanya bei zipande, ni matokea ya fedha hizi.

  4. Fedha haramu huvuruga ‘Price Mechanisms', kwani ni kawaida kwa majangili haya kuwekeza kwenye uzalishaji wa bidhaa fulani, na kwa vile hela yao ni ya dezo dezo, hawajali kuuza bishaa zao chini ya bei ya soko. Hii inawaumiza sana wazalishaji wengine ambao wao bei zao zinatokana na gharama halisi za uzalishaji.

  5. Fedha hizi zina madhara kwa muundo wetu wa kibenki kwani leo benki inaweza pokea fedha nyingi, halafu kesho zikatoka zote, hivyo kutibua assets, liability na operations za benki husika.

  6. Kuna madhara kwenye riba (interest rates). Majangili hawa hawaendi kuwekeza kwenye biashara zenye high returns kutokana na kanuni za soko, badala yake wanawekeza popote pale ili mradi fedha zao zisigundulike kirahisi. Hii huchangia distortion ya interest rates.

  7. Pia Serikali inapoteza mapato mengi kwani sehemu kubwa ya fedha hizi hutoroshwa nje ya nchi badala ya kubakia nchini kusaidia shughuli za Maendeleo. Matokeo yake ni uhaba wa fedha kwa ajili ya shughuli za Maendeleo hivyo kupelekea wananchi kupewa mzigo mkubwa zaidi wa kulipa kodi zaidi.

  8. Huko miaka ya nyumba, nyingi ya fedha hizi zilinunua viwanda vingi sana vilivyokuwa vya serikali zamani. Kutokana na nguvu ya majangili haya kifedha, waliweza ku ‘out bid' watu wengine ambao walikuwa na malengo yenye manufaa kwa taifa, hasa kuvifufua viwanda hivi. Tofauti na hili, majangili haya ndiyo yalinunua viwandda vingi na kuamua kutovifufua. Na wengi wa wale waliovifufua, hawakufanya hivyo kwa kuheshimu makubaliano na serikali. Badala yake viwanda vingi vikageuzwa kuwa ma ‘go-down', pamoja na vituko vingine vingi, hivyo kushindwa kuinua uchumi wa maeneo yale kama ilivyotarajiwa na wengi.
   
 19. Gerald

  Gerald JF-Expert Member

  #19
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu uwa unanifurahisha sana kwa michango yako yenye tija kwa taifa ongera sana ingawa ni ganmba ni wachache mno.
   
Loading...