singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
OFISI ya Bunge imesema kitendo cha baadhi ya watu wakiwemo viongozi muhimu katika jamii kuendelea kuzusha mjadala na hata kulaumu uamuzi uliofanywa na Mwenyekiti wa Bunge kuamuru askari kuwatoa nje wabunge, ni kuingilia Mamlaka ya Bunge na kutofahamu vyema Kanuni za Bunge.
Imesema hayo katika taarifa yake baada ya kuwapo kwa mjadala katika jamii ambao mwishoni mwa wiki ulimgusa Askofu Mkuu mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Frederick Shoo ambaye wakati akitawazwa kushika wadhifa huo, alishutumu askari kuingia bungeni kuwatoa nje wabunge.
Ilisema, “kitendo cha baadhi ya watu wakiwemo viongozi muhimu katika jamii kuendelea kuzusha mjadala na hata kulaumu uamuzi uliofanywa na Mwenyekiti wa Bunge kuamuru Askari kuwatoa nje wabunge waliokuwa wanazuia Bunge lisitekeleze majukumu yake kunatokana na kutofahamu vyema Kanuni za Bunge pamoja na kuongozwa na mitazamo na hisia za kisiasa jambo linalosababisha kuingilia Mamlaka ya Kipekee ya Bunge.”
Taarifa hiyo iliyotolewa kupitia kwa Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa ya Bunge, imetaka ifahamike kuwa, maamuzi yote yanayofanywa ndani ya Bunge huzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria.
“Kitendo cha wabunge wachache walioonesha utovu wa nidhamu na kudharau mamlaka ya kiti kwa kuzuia shughuli za Bunge zisiendelee ni jambo lisilofaa kuvumiliwa na linapaswa kudhibitiwa ili kuwezesha ufanisi wa chombo cha uwakilishi wa wananchi,” ilifafanua.