Bunge lajadili malori kukwama bandarini

Majaliwa anaanza kushindwa kasi ya Mama. Kama Leo hatafukuza watu kazi basi hatoshi hata kidogo. Siku tano bandari! Magufuli aliharibu sana hii nchi akatengeneza mfumo wa kila mahali lazima aende yeye ndio pasonge

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
Mkuu unamlaumu JPM bure. JPM alifanya mambo yaende kwasababu anajua kusimamia mambo. JPM aliisafisha sana Bandari. Kuongoza watu wa nchi hii si kazi ndogo. Hata uje na sheria nzuri kama huna msimamizi nchi hii kazi bure. Kipindi cha JPM urasimu ulipungua mno. Namkumbuka JK siku moja alisema msibani kwa JPM, " Watu wale wa Ardhi ni wagumu balaa". Kama Rais mstaafu anajua. Mzee Mwinyi (Mheshimiwa) alishawahi sema ilivyo ngumu kuleta nidhamu serikalini. Hata Mheshimiwa Mbowe angekuwa Rais angekumbana na hayo. Nadhani Mindset zetu au tamaduni zimetuathiri kimtindo na pia hatuna institution kali za kuwajibishana. Mimi Hayati JPM bila kumumunya Maneno alijitahidi sana na hili la Malori ungesikia mziki wake. Watu wengi hufanya kazi kwa kuogopa kupoteza kazi, wakiachwa wanazoea na kubweteka. Makampuni Private hasa ya nje huwa hayana woga kumtimua mtu akiwa mzembe ndiyo maana watu huwa wana nidhamu. PM akazane pia katika hili.
 
Ndugu zangu,

Wabunge wa CCM wanapiga kotekote

========

Bunge lajadili malori kukwama bandarini Dar​


Bunge la Tanzania limeahirisha mjadala wa Wizara ya Afya kwa takribani nusu saa ili kujadili sakata la malori kutoshusha wala kupakia mizigo kwa muda wa siku tano katika Bandari ya Dar es Salaam.

Dodoma. Bunge la Tanzania limeahirisha mjadala wa Wizara ya Afya kwa takribani nusu saa ili kujadili sakata la malori kutoshusha wala kupakia mizigo kwa muda wa siku tano katika Bandari ya Dar es Salaam.

Hoja ya kuahirishwa kwa mjadala imewasilishwa leo Jumatano Mei 12, 2021 na mbunge wa Mafinga Mjini (CCM), Cosato Chumi.

Chumi amesema Bandari hiyo ndio chanzo kikubwa cha kuendeleza nchi na kufanikisha miradi, “malori hayashushi wala kupakia mizigo kwa maana uchumi kwa namna fulani umesimama. Na tunazungumzia ushindani kati ya bandari yetu na nchi jirani.”

“Katika hali hii hatuwezi kukaa kimya na kuacha mambo ya namna hii yaendelee ndio maana ninajenga hoja tuahirishe mjadala ili tujadili jambo hili nyeti.”

Amesema kuna mizigo inayokwenda kwenye miradi mbalimbali ikiwemo wa uzalishaji wa umeme wa maji katika bwawa la mwalimu Nyerere na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), lakini imekwama katika bandari hiyo.

Amesema mizigo inayokwenda nchi jirani imekwama wakati Taifa linatarajia bandari hiyo kuwa na ushindani.

Baada ya hoja hiyo, Naibu Spika Dk Tulia Ackson aliruhusu hoja hiyo ijadiliwe kwa muda wa dakika 20 ambapo wabunge saba walipata nafasi ya kuchangia.

Akijibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema tayari Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekwenda Dar es Salaam kushughulikia suala hilo.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma>> Malori yakwama bandarini Dar, madereva walalamikia ukiritimba na rushwa kurudi kama zamani
Waziri Mkuu anatakiwa asaidiwe maana kila mara anatembelea bandari lakini hakuna mabadiliko ya utendaji yanayoonekana
 
Hilo tukio hilo lilikuwa maigizo tu. Badala ya kupoteza dk 20 'kujadili' Jenista angeambiwa atoe taarifa yake yaishe. Kwani Tulia alikuwa hajui PM amekwenda Dar?
Hapo ujue huenda kuna jambo lilikuwa linafunikwa kwa kuzua mjadala mpya wa "maroli!!"
 
Hapo ujue huenda kuna jambo lilikuwa linafunikwa kwa kuzua mjadala mpya wa "maroli!!"
Ewaaah! Haiingii akilini PM aondoke eti Spika na naibu, hawajui.
Spin hiyo, kipo wanatufanyia hawa hujuma. TRA kila mara imekuwa kawaida SANA, system down, leo iimekuwa dharura izungumzwe bungeni.

Wanataka kumhujumu mama Rais.
Mizigo kukwama kisa system, ni kawaida SANA hapo bandarini, hata enzi za mwendazake.
Washaanza KOMEDI SHOO

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Cosato Chumi unatuwakilisha vizuri sana wana Mkwawa High School wenzio.

Wewe ni product nzuri ya Makanyagio Casino kabla haijawa University.
Kwenye siasa kila kitu huwa na motive.. Ukifuatilia sana utakutana na figisu za kina Kakoko humo!
 
Ewaaah! Haiingii akilini PM aondoke eti Spika na naibu, hawajui.
Spin hiyo, kipo wanatufanyia hawa hujuma. TRA kila mara imekuwa kawaida SANA, system down, leo iimekuwa dharura izungumzwe bungeni.

Wanataka kumhujumu mama Rais.
Mizigo kukwama kisa system, ni kawaida SANA hapo bandarini, hata enzi za mwendazake.
Washaanza KOMEDI SHOO

Everyday is Saturday............................... 😎
Naam huu ndio unaweza kuwa ukweli wenyewe...
Na tusubiri
 
Back
Top Bottom