Bunge lajadili mabadiliko ya sheria kujusu dhamana ya kesi za uhujumu uchumi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amesema kwa kuwa kesi za uhujumu uchumi hazina dhamana ipo haja sasa kwa wabunge na Bunge kutunga sheria ya marekebisho na kubadilisha pale ambapo itaona panafaa.

Hayo ameyabainisha leo Januari 30, 2020, Jijini Dodoma, kwenye Mkutano wa 18, Bunge la 11, Kikao cha Tatu, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Sabrina Sungura, lililohoji sababu ya vijana wengi wakiwemo kina Tito Magoti kukutwa na kesi za uhujumu uchumi, na kukaa mahabusu muda mrefu, je Bunge halioni kama ni muda muafaka sasa kufanya mabadiliko ya sheria ya uhujumu uchumi ili kuwapa nafasi Majaji na Mahakimu ambao wamekuwa wakiendesha kesi hizi ili waweze kutoa dhamana.

"Kuhusu suala la mabadiliko ya sheria ya uhujumu uchumi, nadhani ni Mamlaka ya Bunge hili kutunga sheria na kubadilisha pale ambapo inaona panafaa, na kama kuna utaratibu mwingine wa kuleta hoja binafsi ili sheria hii ya uhujumu uchumi, iweze kubadilishwa" amejibu Mhandisi Masauni.
 
Hawa akina lugola na wenzake ni vipofu wanachoangalia ni chini ya miguu yao kwamba mamlaka ya umma yana ukomo
 
Taabu ni kuwa hata kwa majaji hawafiki. Wanasota kule kwa mahakimu wa mahakama za wilaya na mkoa...au hata za mwanzo wakitaka washitaki!
 
Back
Top Bottom