Bunge laitaka Serikali kuhakikisha wanafunzi wenye sifa na wamekosa mikopo kupokelewa Vyuoni haraka

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,355
8,043
Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson ametoa agizo hilo Leo Novemba 1, 2022 baada ya kuwahoji Wabunge ambao kwa pamoja wamepitisha Azimio la kuitaka Serikali ihakikishe Wanafunzi wenye vigezo wanaendelea na Masomo.

Hatua hiyo inakuja baada ya kuwepo taarifa za Wanafunzi wenye vigezo vya kupata mikopo, kuzuiliwa Vyuoni kutokana na Bodi ya Mikopo kutowapa au kuchelewesha Mikopo yao.

Spika Tulia amesema Wanafunzi wote wenye vigezo vya kupata Mikopo warudi vyuoni na Serikali ihakikishe wanapokelewa wakati ikiendelea kutafuta fedha.
 
Huyu Tulia anabwabwaja tu. Amri hiyo anampa nani? CEO wa HESLB au Samia? Mazuzu yamekaa humo eti wabunge. Kwenye katiba ambayo hairuhusu imperial presidency, wabunge wanaweza kui command serikali, siyo kwetu kwa wajinga!
 
Umeongea ukweli mtupu ,nchi yetu mara nyingi viongozi huja na matamko tu bila kupima,kuchunguza na kufuatilia.
Wao Helsb wanadai kuwa mwaka huu wanufaika watakuwa 42k while mwaka jana walikuwa 70k+ na wanadai kuwa hizo pressure za wasiansa watakabiliana nazo
 
Yah ,Inabidi mambo yafanyike kiuweledi na kutoa ufumbuzi wa kudumu isewe matamko ya zima moto.
 
Makusanyo duni. Kundi kubwa la wanufaika bado wanatanga tanga mtaani

Either Serikali ili Refund mfuko OR kutoa ajira mpya Bodi wapate Client wengi kuongeza makusanyo.
 
Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson ametoa agizo hilo Leo Novemba 1, 2022 baada ya kuwahoji Wabunge ambao kwa pamoja wamepitisha Azimio la kuitaka Serikali ihakikishe Wanafunzi wenye vigezo wanaendelea na Masomo.

Hatua hiyo inakuja baada ya kuwepo taarifa za Wanafunzi wenye vigezo vya kupata mikopo, kuzuiliwa Vyuoni kutokana na Bodi ya Mikopo kutowapa au kuchelewesha Mikopo yao.

Spika Tulia amesema Wanafunzi wote wenye vigezo vya kupata Mikopo warudi vyuoni na Serikali ihakikishe wanapokelewa wakati ikiendelea kutafuta fedha.
Tanzania 🤣🤣🤣
 
Hizi akili za ccm,zimeoza sasa Hilo agizo ndio litaleta fedha?fedha haziletwi na matamko!!bodi ya mikopo inapokea pesa kutoka hazina !kama pesa haitoshi,hiyo mikopo itatoka wapi?
Hao wabunge wanapiga Domo tu,wangekuja na mkakati maalum,punguza posho serikalini,hakuna kununua magari,au baadhi yaliyopo yapigwe mnada,Ili kutunisha mfuko wa bodi ya mikopo.
Nje ya hapo,hizi ni swaga tu,
Kwanza wao watoto wao hawategemei hiyo mikopo.hawawezi kusikia uchungu
 
Makusanyo duni. Kundi kubwa la wanufaika bado wanatanga tanga mtaani

Either Serikali ili Refund mfuko OR kutoa ajira mpya Bodi wapate Client wengi kuongeza makusanyo.
Serikali ipunguze waendao Chuo Kikuu
 
Wala msipate taabu kufanya argument, chama huwa na vikao na kuafikiana mambo yao kabla ya kikao, ni jambo ambalo wameafikiana kua wataipa serikali maelekezo alafu itatekeleza!

Simply ni create tatizo, solve tatizo.
 
Inasemekana zinatokana na UVCCM wengi kukosa mikopo..coz kelele hizi hatujawahi zisikia miaka mingine vijana wetu walipokuwa wanateseka kwa kukosa mikipo
 
Huyu Tulia anabwabwaja tu. Amri hiyo anampa nani? CEO wa HESLB au Samia? Mazuzu yamekaa humo eti wabunge. Kwenye katiba ambayo hairuhusu imperial presidency, wabunge wanaweza kui command serikali, siyo kwetu kwa wajinga!
Wewe unafanya kazi HESLB? Kwanini speaker na wabunge wasihoji na kutafuta suluhisho? Bunge si moja ya mihimili mikuu mitatu katika utekelezaji wa masuala muhumu yahusuyo mustakabali wa nchi?!
 
Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson ametoa agizo hilo Leo Novemba 1, 2022 baada ya kuwahoji Wabunge ambao kwa pamoja wamepitisha Azimio la kuitaka Serikali ihakikishe Wanafunzi wenye vigezo wanaendelea na Masomo.

Hatua hiyo inakuja baada ya kuwepo taarifa za Wanafunzi wenye vigezo vya kupata mikopo, kuzuiliwa Vyuoni kutokana na Bodi ya Mikopo kutowapa au kuchelewesha Mikopo yao.

Spika Tulia amesema Wanafunzi wote wenye vigezo vya kupata Mikopo warudi vyuoni na Serikali ihakikishe wanapokelewa wakati ikiendelea kutafuta fedha.
Futuhiiiii ndiyo ni FUTUHI.
 
Hizi ni siasa za kishamba haiwezekani kila mwenye sifa za kupata mkopo akapata na hii ipo toka bodi hii imeanzishwa! Haiwezekani kila mwanafunzi akapata mkopo eti kisa ana sifa labda watwambie tangia lini kila mwenye sifa anapata mkopo?

Pamoja na shida waliyonayo bodi ya Mkopo ila naona kuna dalili ya wazi kabisa hapa CEO wa bodi ya mkopo anaundiwa zengwe na sababu ya kufukuzwa!
 
Back
Top Bottom