Bunge laibana Serikali kuipa KADCO mkataba wa uendeshaji uwanja wa Ndege KIA badala ya TAA

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,355
8,043
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imemtaka Waziri Prof. Makame Mbarawa kueleza sababu za Serikali kuuacha Uwanja wa KIA kwa Kampuni ya Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege (KADCO) ambaya haipo.

Spika Dkt. Tulia amesema “Wanasema mkataba unamalizika Juni 2023 ni mkataba gani? wakati hiyo KADCO haipo kwasasa na haya mazungumzo ya mkataba yanatokana na nini? Kwa nini Serikali haikuurejesha TAA Kwa sababu haya yote yasingejitokeza kama CAG hakuona kuna shida,”.

Kutokana na hilo, Spika Dk Tulia Ackson amempa siku 2 Waziri Prof. Makame Mbarawa kulieleza Bunge kwanini KIA iko chini ya Kampuni ya Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege (KADCO) badala ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA).

=========================

Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amembana Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa kuhusu umiliki wa Kampuni ya Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege (KADCO).

Mbarawa amekutana na kibano hicho Alhamis Novemba 3, 2022 mara baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza na Dkt. Tulia kulitolea ufafanuzi suala hilo ambalo liliibuliwa bungeni kwenye taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Akizungumzia kuhusu umiliki wa KADCO, Profesa Mbarawa alisema kampuni hiyo inamilikiwa kwa asilimia 100 na Serikali tangu mwaka 2011 baada ya kununua hisa za wabia watatu. Amesema kampuni hiyo imekuwa ikilipa gawiwo na ushuru serikalini kasoro kwa miaka miwili ya 2019/2020 na 2020/2021 ambako kulikuwa na tatizo.

“KADCO inaendeshwa kwa mujibu wa Sheria za kampuni na haiko chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), kwa sababu mamlaka ya Viwanja vya Ndege iko chini ya sheria ya wakala wa Serikali. “Hivi sasa tuko katika mpango wa kuibadilisha iwe kuifanya iwe mamlaka,”amesema.

Amesema pengine huko mbele ndipo wanaweza kuibadilisha na kuziunganisha taasisi hizo mbili lakini kwa sasa ni taasisi zinazoendeshwa kwa sheria tofauti. “Nilifikiri hili ni jambo muhimu la kulieleza kwasababu leo limeelezwa kuwa ni kampuni inayomilikiwa na watu wa nje wakati sio kweli wakati inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100,” amesema.

Baada ya maelezo hayo Dk Tulia alimhoji uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere unaendeshwa na kina nani ambapo Profesa Mbarawa alijibu kuwa unaendeshwa na TAA. Hata hivyo, Dk Tulia alihoji tena mkataba unaozungumziwa wa kati ya kampuni KADCO ni upi wakati tayari Serikali imeshamiliki kampuni hiyo kwa asilimia 100.

Akijibu Profesa Mbarawa amesema ni mkataba wa Serikali kwa asilimia 100 lakini kwa jina unaendeshwa na kampuni ya KADCO na kwamba ni jina tu. Amekanusha kuamsha jambo jipya na kwamba wanatazama taarifa CAG zinasemaje kuhusu jambo hilo ambapo ameona kuna shida.

Profesa Mbarawa amesema kamati imepata nafasi ya kuonana na watu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na watu wa KADCO lakini bado imeonekana kuna changamoto.

“Wanazungumzia mkataba unamalizika Juni 23 ni mkataba gani? Kwa sababu hiyo KADCO sasa haipo kabisa sasa haya mazungumzo ya mkataba yanatokana na nini? “Kwa nini Serikali iliporejesha haikurejesha TAA kama inavyofanya kwa Dar es Salaam? Kwa sababu haya yote yasingejitokeza kama CAG hakuona kuna shida,” amesema.

Hata hivyo, Dk Tulia alimweleza Profesa Mbarawa aende akafanyie kazi maswali hayo na kwamba atampa nafasi hiyo tena kesho kutwa (Jumamosi).
 
Back
Top Bottom