Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
Spika Wa Bunge Akutana Na Ujumbe Wa Timu Ya Kujitathimini Katika Maswala Ya Utawara Bora Barani Afrika
Zile posho zilizokataliwa zimerudi kwa mlango mwingine, kwani wamebuni utaratibu wa vikao vya nje ya vikao vya kawaida vya bunge ili kujilipisha posho. Vikao vya wabunge vimeshamiri, na hata hawana muda wa kushughulikia mambo ya majimboni mwao. Misafara isiyoisha ya kutalii nje ya nchi kwa visingizio vya ukaguzi wa mashirika ya umma na majifunzo, utalii ni kama hata majukumu ya kushiriki vikao Dodoma hakuna umuhimu vile. Balozi zetu za nje zimenyang'anywa majukumu, sasa kazi hizo zinafanywa na wabunge wa bunge letu.
Hii tathmini ya utawala bora nini zaidi ya semina elekezi zilizofanywa na serikali ya Rais wetu Kikwete, matokeo yake ndio sawa na kutilia kibatari mafuta ya taa ili utambi uungue vizuri. Ninachoona mimi ni kuendelea kutumia pesa za walipa kodi bila manufaa na badala yake ujumbe wa watu wawili au watatu ungetosha na kisha kwenda kutoa lecture kwa wabunge wote.
Katika picha vikao vya kujitathmini vilipaswa kufanyika wakati wa vikao vya kawaida huko Dodoma, lakini vimepangiwa muda nje ya vikao vya kawaida ili kujenga mazingira ya kujilipisha posho. Kwa hali hii ni sawa na sikio la kufa kutosikia dawa. Wajumbe wote hao ilikuwa lazima wahudhurie au watatu au wawili wangetosha kupata ujumbe wa kuwafikishia wabunge wengine mjengoni?
Wajumbe wa timu ya kujitathimini katika maswala ya Utawara Bora barani Afrika (Africa Peer Review Mechanism –APRM)
wakiwa katika kikao cha pamoja na Spika wa Bunge na wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge
mara baada ya kukutana nao Ofisi za Bunge Dar es salaam.