Bunge laahirishwa kwa mbwembwe hadi februari 8,2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge laahirishwa kwa mbwembwe hadi februari 8,2011

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makoye2009, Nov 18, 2010.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Rais wa Watanzania milioni 5 ameahirisha Bunge kwa hotuba iliyojaa unafiki,majigambo,uongo na ahadi kemkem zisizotekelezeka hadi hapo Tarehe 8,Februari,2011.
  Ukweli ni kwamba Hotuba hii imeacha vichefuchefu masikioni mwa Watanzaia walio wengi.

  Nitazungumzia machache yaliyojitokeza kwenye hotuba hii ya JK ambayo hakusema ukweli:

  1. UDINI: Swala la udini amelizungumzia tena kwenye speech yake. Mimi Napata taabu kidogo kwanini UDINI imekuwa kama ndiyo sera ya CCM tangia wakti wa kampeni na hata baada ya Uchaguzi. Kuna nini hapa? Inavoonekana ni kwamba KIKWETE ANAKIMBIA KIVULI CHAKE MWENYEWE. Yeye Kikwete na chama chake CCM ndiyo waliomwaga upupu wa udini wakti wa kampeni kwa hofu ya kushindwa na CHADEMA na si vinginevyo. Jambo la kushangaza kabisa jambo hili bado linamrudia mwenyewe.Nitaeleza: Kwenye uteuzi tu wa Wabunge 3 alioufanya jana Wabunge wote ni WAISLAMU,Zakhia Meghji,Vuai Nahodha na Prof. Mnyaa. Sasa mdini hapa NANI? Tujadili.


  2. USPIKA:Kampongeza sana Anne Makinda kwamba CCM inapofika swala la kuwapa wanawake nafasi hawaoni ajizi na ndiyo maana wamempa huku akimpongeza Mhe.Samwel John Sitta kwa kazi nzuri kwenye Bunge lililopita na kumtakia kila la kheri kuwawakilisha wana Urambo Masahariki. Unafiki mkubwa. Nilimwona Mzee Sitta akifumba Macho akiangalia juu kwenye dari nafikiri alikuwa anaumia moyoni jinzi alivyonyangÂ’anywa tonge mdomoni.Kama alikuwa anafanya kazi nzuri Bunge lililopita kwanini mmemuondoa?

  3. AHADI YA UTEUZI WA BARAZA LA MAWAZIRI: Kwamba eti atateua viongozi waadilifu,makini na wachapa kazi . Jambo hili siyo kweli. Maana tayari ameshaanza kuteua watu walewale waliomwangusha kwenye awamu yake ya Kwanza. Mizengo Pinda amefanya nini kwenye miaka 2 na nusu iliyopita. Atuonyeshe hata moja. Hakuna zaidi ya KUWALILIA MA-ALBINO na kujidai ni mtaalamu wa kujibu maswali ya papo kwa papo ambayo aghalabu hayana ufumbizi wowote. Meghji keshamteua. TUNASUBIRI HILO BARAZA KAMA KWELI KUTAKUWA NA BADILIKO LOLOTE. Hatoweza kuwatupa rafiki zake. Tusubiri.


  4. TAKUKURU:Amezungumzia kwa mbwembwe na kuisifia kuwa inafanya kazi nzuri kwa hiyo TAKUKURU wapewe pongezi pale wanapofanya vizuri. Je,vipi kuhusu wanapofanya vibaya na hasa kwenye maswal a nyeti ya UFISADI kama tukio la juzi la Mhe.CHENGE kumsafisha kutokana na tuhuma za RADA? Tuliona TAKUKURU walivyojitokeza mbele ya vyombo vya habari kuwa Chenge hahusiki na swala la Rada na kuwa SFO ya UK walishafunga faili. Baada ya siku mbili UK wakaja juu na KUKATAA KATAKATA kuwa si kweli Chenge ameonekana hana hatia baalikilichopo ni kwamba SFO ndiyo wanajiandaa kwa sasa kupeleka hilo swala Mahakamani!!!Hii ilikuwa ni aibu kwa Serikali ya Kikwete na Dk.Hosea alipaswa ajiuziulu mara moja,lakini sivo baada anaendelea kukalia kiti pamoja na uongo wake huo.


  5. AHADI KEMKEM: Kana kwamba ameshasahau ahadi alizowaahidi Wananchi wakti wa Kampeni za Uraisi leo tena kamwaga ahadi lukuki ndani ya Bunge. Sijui atazitekeleza vipi huyu Mkwere ukijumlisha na hizo za awamu iliyopita na hizo za kwenye majimbo. Kweli Kikwete anaonekana hayuko makini na amejaa ubabaishaji mtupu. Nashangaa hata ile ahadi yake ya KILIMO KWANZA leo wala hajagusia kabisa yaani tayari keshasahau au anafikiri Watanzania ndo tumeshasahau maana juzi Katibu wake Mkuu Makamba baada ya Uchaguzi alisema ikifika 2015 Watanzania wataipa tena kura CCM maana watakuwa wameshasahau. Kwa hiyo ni yale yale yale. Hakuna Jipya. Yetu macho.
   
 2. N

  Newvision JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Makoye asante kwa kutuhabarisha lakini umesahau mengine. Vipi juu ya madini yetu ina maana alikwisha kubali tudhulumiwe.
   
 3. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  dah,asante sana kwa uchambuzi huu!
  Binafsi kila kitu anacho fanya siku hizi nakiangalia kwa mtazamo wa kidini na hii ni kwa sababu anaihibiri out of non-existance.

  natamani kusema yaliyo moyoni ila sitapata burn,nitafungiwa totally,....i hate him
   
Loading...