Bunge laahirishwa kumuenzi Spika mstaafu Samuel Sitta

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,961

Bunge Limeahirishwa leo hadi kesho kumuenzi Samuel Sitta amabaye alikuwa spika wa bunge hilo

Wabunge wengi wamemzungumzia kwamba alipokuwa spika alisimamia vizuri bunge bila kujali itikadi za chama na bunge halikuingiliwa na mihimili mingine ya dola
 
Wajaribu kutafakari sura mbili za Sitta.Kwanza alipokuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Pili alipokuwa Spika wa bunge la Katiba.Wakumbuke kwa Mungu utakwenda peke yako kutoa hesabu ya Maisha yako wewe mwenyewe bila kusindikizwa na wapambe hivyo tuige yale mema aliyofanya na tuyapuuze yale mabaya aliyofanya kwa ajili ya kufurahisha nafsi yake au rafiki zake.
 
Alikuwa spika bora kabisa kuwahi kutokea, namsamehe kwa kuchafua katiba mpya na namuombea kwa Mungu amsamehe makosa yake RIP sitta
Alikuwa kinyume chake, alifanya kazi kuegemea maslahi yake binafsi, ya kisiasa na chama chake. Hajawahi kunivutia hata siku moja. Sitaki kuwa mnafiki!

Je,hao wabunge walioahirisha kikao cha leo kwa ajili ya kumuenzi, hawatachukua posho la leo? au ndio dili/janja ya kuongeza posho kwa kujiongozea siku moja zaidi bungeni?
 
Mkuu hauko serious kabisa...!!
Hauna uwezo wa kumuombea kwa Mungu
asamehewe makosa yake
ingekuwa hivyo basi wote tungeenda mbinguni
Atafahamu mwenyewe kama alikuwa na dhambi Jehanamu lazima
Kama alitubu kabla ya kufa basi Mungu atampokea
 
Alikuwa kinyume chake, alifanya kazi kuegemea maslahi yake binafsi, ya kisiasa na chama chake. Hajawahi kunivutia hata siku moja. Sitaki kuwa mnafiki!

Je,hao wabunge walioahirisha kikao cha leo kwa ajili ya kumuenzi, hawatachukua posho la leo? au ndio dili/janja ya kuongeza posho kwa kujiongozea siku moja zaidi bungeni?
Swali la kilofa!
 
Hivi kwenye siasa nae unategemea uende peponi imekuwa tena hivyo wabongo mnarahisisha yaani badala ya kusali miskitini na makanisani nyie mmekazania oohh tumuombee waislamu tuna msemo SALI kabla HUJASALIWA utahukumiwa kulingana na ibada uliofanya hapa duniani sio fiksi za EYENA IYENA
 
Bunge Limeahirishwa leo hadi kesho kumuenzi Samuel Sitta amabaye alikuwa spika wa bunge hilo
Wabunge wengi wamemzungumzia kwamba alipokuwa spika alisimamia vizuri bunge bila kujali itikadi za chama na bunge halikuingiliwa na mihimili mingine ya dola

Waacheni wafu (CCM) wazike wafu wenzao sisi tuendelee na mijadala.
 
Alikuwa kinyume chake, alifanya kazi kuegemea maslahi yake binafsi, ya kisiasa na chama chake. Hajawahi kunivutia hata siku moja. Sitaki kuwa mnafiki!

Je,hao wabunge walioahirisha kikao cha leo kwa ajili ya kumuenzi, hawatachukua posho la leo? au ndio dili/janja ya kuongeza posho kwa kujiongozea siku moja zaidi bungeni?
unataka kuwaudhi makamanda kuhusu posho
 
wabunge waache uvivu wanaahirisha bunge kwa sababu gani, ninkweli marehemu aliwahi kuwa spika na mbunge wa bunge la muungano ila wajue hapo wanaongeza mzigo wa kodi za watanzania isitoshe marehemu bado yuko nje ya nchi
 
Sie ni waja wa Mola na kwake tutarudi na kukuta hesabu zote za hapa duniani, unapokuwa na dhamana tetea wananchi usitetee utawala wa wachache.
 
Wajaribu kutafakari sura mbili za Sitta.Kwanza alipokuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Pili alipokuwa Spika wa bunge la Katiba.Wakumbuke kwa Mungu utakwenda peke yako kutoa hesabu ya Maisha yako wewe mwenyewe bila kusindikizwa na wapambe hivyo tuige yale mema aliyofanya na tuyapuuze yale mabaya aliyofanya kwa ajili ya kufurahisha nafsi yake au rafiki zake.

Sitta alikuwa na nia nzuri, kumbuka kuna watu walimuwekea majungu ndani ya CCM ili wamuondoe kwanye u spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alipoteuliwa bunge la katiba akawa kanyong'onyea maana alikuwa anajua adhabu aliyopewa na chama chake. Hivyo akawa hana namna, ikabidi bunge la katiba awe mtumwa wa watawala. Mimi naamini kama angekuwa huru hasingekubali rasimu ya Warioba ichafuliwe
 
Anayejua ukweli wa yote ni Mungu lakini alijitoa sana,Nakumbuka mpaka aliwakaripia wapakwa mafuta wa Bwana.
 
Kila mtu ana haki ya kumkumbuka Samuel Sitta kivyake. Wengine tulimueka daraja la mbele sana hadi pale alipo achia makada walichukue bunge la katiba na kuleta mtafaruku mkubwa kitaifa. Miaka yake ya uadilifu, uaminifu na uzalendo yalimalizikia na katiba pendekezwa vyenginevo angeliondoka kama mheshimika katika sayari ya siasa ya tanzania,
Nawapeni pole wafiwa wote, watoto, ndugu na marafiki. Tulikupenda na Mungu kakupenda zaidi.
 
Back
Top Bottom