figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,486
Wabunge wa Upinzani wasababisha bunge la asubuhi kuahirishwa hadi Jioni. Mapema baada ya Maswali na Majibu, Waziri wa Fedha Dokta Philip Mpango, alisoma Muelekeo wa mpango wa Serikali wa Maendeleo wa mwaka 2016/2017.
Baada ya kumaliza kusoma, Zitto Kabwe na Tundu lissu, Wakaomba Muongozo wakieleza kwamba, Waziri wa Fedha amesoma muelekeo wa mpango wa maendeleo wa Mwaka mmoja badala ya miaka mitano, hivyo kavunja katiba, sheria na kanuni za Bunge.
Mwenyekiti wa Bunge alikua Andrew Chenge, akatoa mwongozo wake kwamba swala hilo atalitolea ufafanuzi baadae baada ya kukutana na Uongozi wa Bunge.
Alivyo maliza kutoa muongozo, akamuita Msemaji wa Kambi ya Upinzani, ambapo Mh. Davidi Silinde, alisimama mbele ya bunge na kusema hawezi kusoma muelekeo wa Mpango wa maendeleo wa Mwaka 2016/2020 wakati Serikali haijasoma Mpango wake, akaitaka Serikali isome kwanza mpango wake kama kanuni na desturi ya bunge kisha Msemaji wa Upinzani afuate.
Silinde akasema sisomi, akaenda kukaa.
Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge, akaamua kuahirisha Kikao cha Bunge hadi jioni.