Bunge la vijana Tanzania limeanza Dodoma

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,629
34,172
unnamed-8.jpg

Spika wa Bunge la Vijana Ndg. Edgar Israel kutoka chuo cha St. John akiingia Bungeni

BUNGE la Vijana Tanzania limeanza vikao vyake jana mjini hapa, huku wakijikita kujadili changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu nchini.

Akiongea na waandishi wa habari jana nje ya ukumbi wa bunge hilo, Spika wa Bunge, Reginald Massawe kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha, alisema wabunge wake ni kutoka vyuo mbalimbali vilivyopo nchini lengo likiwa ni kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya kibunge. ‘Lengo la sisi kukutana hapa ni kujipa uzoefu kuhusu masuala ya kibunge pamoja na kujifunza kuongoza wengine ,ifahamike kuwa bila uzoefu huwezi kuongoza wengine vizuri’.alisema

Pamoja na hayo alisema katika Bunge hilo watajadili mambo yanayohusu sekta ya elimu ikiwemo bajeti ya Wizara ya Elimu na changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo.

Kwa upande wake Mbunge kutoka Chuo cha Mtakatifu Augustine (SAUT) Mwanza, Rashid Muziru, alisema Bunge hilo ni moja ya elimu ya kuwafanya waweze kujenga hoja na kubadilishana mawazo juu ya mambo mbalimbali kuhusu maendeleo ya Taifa.

Hata hivyo alisema katika bunge hilo wamejielekeza katika sekta ya elimu kutokana na kukabiliwa na changamoto kwa kuwa wao ni wadau kwenye sekta hiyo. Aliongeza kuwa serikali inatakiwa kuweka misingi bora ya elimu kwa vijana ili waimarike na wahamasike kutambua umuhimu wao katika jamii.

Naye Kiongozi wa kambi ya upinzani katika Bunge hilo, Boniface Mbando kutoka Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini(IRDP), alihoji Wizara ya Elimu pamoja na kuwepo na elimu bure je serikali imefanya utafiti na kujua tatizo la elimu ni ada kwasababu wao kama kambi wamebaini tatizo ni ubora wa elimu na si ada. Kutokana na hayo, Rais wa Bunge la Vijana, Owen Mwandumbya, alisema Ofisi ya Bunge, kupitia Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano imejiwekea mpango mahsusi wa kutoa elimu kwa umma ili kujenga uelewa mpana kwa jamii wa masuala mbalimbali ya Kibunge ikiwemo vijana.

Rais huyo wa Bunge la vijana alibainisha kuwa elimu hiyo itawawezesha vijana wengi kujifunza namna ya kujadiliana na kupitisha masuala mbalimbali bungeni ikiwa ni pamoja na uwezo wa kujenga hoja. Mbali na hayo alisema elimu hiyo itaamsha ari ya vijana kulipenda na kulifuatilia Bunge, kuimarisha sifa za uongozi ndani ya vijana ili kushiriki midahalo ya Kitaifa na Kimataifa ili kupata viongozi wa baadae.

Akihitimisha Mwandumbya alisema,ni wajibu wa serikali na jamii kwa ujumla wakiwemo vijana kuwa mstari wa mbele kushiriki kikamilifu shughuli zinzzoliletea taifa maendeleo ili kuifikia Tanzania mpya.
 
Back
Top Bottom