Bunge la Ulaya: Uchaguzi wa Uganda ulikuwa ‘Operesheni ya Kijeshi’—EU yapendekeza vikwazo vya viza, kufungia mali

Bunge la Ulaya: Uchaguzi wa Uganda ulikuwa ‘Operesheni ya Kijeshi’—EU yapendekeza vikwazo vya viza, kufungia mali

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,879
Reaction score
16,311
Bunge la Ulaya limeuita uchaguzi wa Uganda uliofanyika Januari 15, 2026 kwa jina la 'Operesheni ya Kijeshi' ya kukandamiza upinzani pekee wenye nguvu ya ushawishi. Vyombo vya usalama vilitumika si kulinda wapiga kura, bali kutisha, kuua, kuwakamata na kuwaweka kizuizini, kutesa, na kunyamazisha wapinzani wa kisiasa.

Katika tamko lake, Bunge hilo limesema vikosi vya usalama vilitumika si kwa lengo la kulinda wapiga kura, bali kuwatishia, kuwatia mbaroni, kuwatesa na hata kuua baadhi ya wapinzani wa kisiasa. Kwa mujibu wa kauli hiyo, mazingira ya uchaguzi yalitawaliwa na hofu, ukandamizaji na vizuizi vilivyolenga kuzuia ushindani wa haki wa kisiasa.

Bunge la Ulaya limezitaka Umoja wa Ulaya (EU), nchi wanachama wake pamoja na washirika wa kidemokrasia kuchukua hatua madhubuti dhidi ya wahusika wa vitendo hivyo. Hatua zilizopendekezwa ni pamoja na kuweka vikwazo vinavyolengwa, marufuku ya viza, kufungia mali za wahusika, kusimamisha ushirikiano wa kiusalama, na kupitia upya misaada inayodaiwa kuendeleza au kuhimili ukandamizaji.

Screenshot 2026-02-12 091858.png
 
Back
Top Bottom