Bunge la Ulaya(EU) lajadili hali ya kisiasa Tanzania na kukamatwa kwa Freeman Mbowe

Ulitazama mjadala wote? Mbona Samia wako kapigwa nyundo za usoni. Kaambiwa amwachie Mbowe mara moja. Sikiliza hapa.
 

Attachments

  • Voice 002_sd.m4a
    2.4 MB · Views: 1
Mpasuko katika nchi huwa unakomaa kwa namna hii hii. Taratibu wananchi wengi hasa wanaoumia wanaona ni bora kutoa support kwa mataifa au taasisi za nje zinazowasemea.
Mwisho mataifa/taasisi hizo zikiingia nchini zinapewa support ya kutosha na wananchi.

CCM na Serikali acheni kushupaza shingo, hili taifa ni letu sote. Tafuteni umoja wa kitaifa, rudisheni imani, tendeni haki, ili watu wetu wawe na moyo wa kutetea na kulipenda taifa lao.
 
Kwani Tanzania ni koloni la mataifa ya ulaya inaingiliwaje mambo yake ya ndani au sio nchi huru?
We unatumiwa pesa ya kujazia bajeti, na wewe unatuma pesa ya bajeti katavi sasa ww sio kiranja tu kwa hao kaka wakuu kama alivyosemaga Jk Nyerere? Pesa ndio inadhihirisha uhuru wako, bado wapo hao,
 
Lisu hadi leo anasubiri tz ipigwe ban toka 2010
Najua wewe hujui maana ya kupigwa ban.

Ulishapigwa ban siku nyingi ila wewe hujitambui.Ban ya hapa karibuni sana,ili upate misaada,kubali kuwa corona ipo na onyesha takwimu.

Lilipofanyika hili,ukapewa mkopo wa mamilioni,ban nyingine ambayo kwa wewe mwenye akili ndogo hukuweza kuona ni kitendo cha Denmark aliyekuwa mshirika mkuu Tanzania kwa miaka mingi kufunga ubalozi na kuukimbizia Nairobi.Wakubwa wakatudanganya eti kama ni huduma tutazipatia Nairobi kana kwamba Nairobi ni hapo Upanga.

Hapo ulipigwa ban ya kimya kimya.Yapo mengi.
 
Kutumia externals kama sehemu ya majumuisho ya kupambana na dola binafsi sikubaliani nalo. Mara mabalozi kuwa mahakamani inakua topic ya chama mara kujadiliwa EU. Oppositions na wanaharakati lazima wajikite kama nationals binafsi nitaelewa harakati ila si hizi sarakasi
Lazima tuamke bila NGOs nk tunaweza kusonga
Nani kakudanganya wewe, kwa asilimia kubwa tunaendeshwa na ngos tafuta taarifa uelewe,achana na hizo channel zinazojisifia na kujiita channel za taifa.

Ajira nyingi za wasomi wetu zimetolewa na NGOs.Wasomi wengine baada ya kukosa ajira na ikaonekana ni bomu litakalolipuka kesho,wakapewa vibali vya 20000/- ambavyo sasa hivi vime expire watafute pa kwenda.
 
Labda mimi ndo sio mfatiliaji,

Mambo kama haya ya upinzani kuwekwa rupango yakitokea huko Rwanda mboma huwa ni kimya sana kana kwamba hakuna kinachotokea?

Wapinzani nchini urusi pia wanapitia wakati mgumu kama vile kukamatwa na kufunguliwa kesi. Mbona sisikii kelele za kuomba waachiwe.

Sasa kama kuna watu hawawezi kuwakemea basi ni bora wakae kimya tu.

Niko Tayari kuelimishwa
Kesi za hawa, sio za kubambikizwa,wanakamatwa na ushahidi ukiwepo.Wewe utamtetea mwalifu ali hali ametenda uhalifu unaoonekana na wenye ushahidi wa wazi kama huu wa Sabaya wa CCT Cameras ,si utaonekana na wewe ulishiriki?

Kesi kama hizi tunazozifuatilia (ahsante sana mawakili na wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,kama msingechachamaa walipotaka kuwapiga ban kusikiliza mwenendo wa kesi ya Mkiti wenu mkakomaa wakalegea leo hii tusingepata mwanga huu tulioupata mpaka tukajua kwamba wengi wanaojiita wanalinda mali za raia na kuwakamata wahalifu,hawajui PGO mwongozo wa utekelezaji wa kazi zao za kila siku.Sasa hata sis tumefahamu) mtu anaambiwa mahakamani alikuwa anakwenda kukata magogo kuziba barabara,hujamkamata hata na chain saw au basi hata msumeno wa mkono.Haya anakwenda kulipua vituo vya mafuta,hivyo vilipuzi mlivyomkuta navyo viko wapi nk.lazima kelele za kutafuta haki zitakuwepo tu.Kubali usikubali ni hivyo.

Hapa ni ubambikiwaji wa makosa ambayo ni wazi aliyepewa hausiki ila amebambikiziwa ili kumkomoa.Au we hukusikia kuwa aliambiwa, tutakufungulia mashtaka ya uhujumu uchumi yale ambayo hayana mdhamana.Yule mwingine kule hai alimwakikishia mgombea kuwa watahakikisha hashindi ubunge.

Na kweli wakafanya walilofanya ikawa hivyo.Kundi hili linaloonewa hivi ndilo linalopigiwa kelele na mabaraza ambayo Tanzania imeahidi kulinda na kutenda haki kwa watu wake na kutia saini na kukubaliwa kuwa mwanachama,

Unapokwenda kinyume sasa na kujifanya ni nchi huru ndio sasa wanakufuatilia na kukushauri ubadilike.Usipofanya hivyo ban inakuhusu.

Haya yanayoonekana kuwa hayajatendeka kwa haki,ni lazima kelele ziwe nyingi sana,na zitaendelea mpaka haki itendeke kwa kupenda ama kwa kulazimishwa kwa njia ya makelele.
 
Back
Top Bottom