JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,441
- 55,018
Mkuu Joka Kuu, kwenye hili mimi naungana na serikali yetu kuwa Tanzania is a sovereign state, tutaamua mambo yetu wenyewe bila kuingiliwa au kupangiwa na mataifa ya nje.
Natolea mfano wa mradi wa Kamba Samaki, shrimp farming kwenye Rufiji Delta, ulipitishwa vizuri tuu, lakini kabla ya utekelezaji, mashirika ya kimataifa ya mazingira yakaja na EIA nyingine, tukapigwa stop mradi ukafa. Hoja ya wanamazingira ni kilimo kile kingeathiri uoto wa asili wa mikoko.
Ukiangalia cost benefits na value benefits za mradi na faida za mikoko, mikoko are nothing compared.
Kama ulifuatilia issue ya Kihansi Hydro Electric Project, mradi ulichelewa sana kwa hoja ya vyura wa Kihansi hadi Marekani walipokubali kuwa relocate wakahamishwa, mradi ulipokamilika wakarudishwa. Ukiangalia faida za nchi inayohitaji umeme na faida ya vyura ni nothing compared.
Sasa kwenye Stieglers ni vile vile wanataka kutupangia, kule nyuma waliweza kwa sababu fedha walikuwa wanatoa wao. Kwa Stieglers, watakwama kwa sababu this time around fedha ni zetu.
Hili jambo niliisha lizungumza sana humu
P
..mimi ningependa u-argue your case bila kuingiza masuala ya Soveregnity.
..nadhani hoja ya sovereugnity huwa inaibuliwa ili kufukia-fukia hoja zinazotakiwa kujibiwa kitaalamu.
..Wajerumani wametu-challenge kuhusu suala la MAZINGIRA ya Selous na bonde la mto Rufiji.
..Sasa unatakiwa uje na counter-argument za jinsi ya kudhibiti hayo madhara waliyosema yatatokea.
..Kwa upande wa Kihansi naona mambo yalifanyika vizuri. Zilitolewa sababu za kimazingira na wataalamu wakaja na mbinu za kujibu hoja na tahadhari zilizotolewa. At the end of the day tulipata mradi wa umeme, na vilevile tulitunza hao viumbe ambao walikuwa ktk hatari ya kutoweka. Everybody "won" in that case.
..Mimi ninachopendekeza ni serekali iweke wazi tahadhari za kimazingira za mradi huu. Pia tupewe alternative/options za sites nyingine zinazofaa kwa uzalishaji umeme. Na zaidi serekali ieleze hatua itakazochukua kudhibiti madhara kwa mazingira.
NB.
..bonde la mto Rufiji linagusa maisha ya WAKULIMA na WAVUVI. Je, tumefikiria mustakabali wa maisha yao?