Bunge la Uganda laanzisha Viti Maalum vya wazee

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,009
9,874
Bunge la Uganda limepitisha muswada unaoidhinisha kuanzishwa kwa viti vitano vya wawakilishi wazee, lakini sharti mmoja awe mwanamke.

Uwakilishi wa wazee bungeni kama kundi maalumu, pamoja na kuandaa mpango wa kuchaguliwa kwao kupitia mabaraza maalumu, ni takwa la katiba.

Umri wa mwakilishi mzee ni kuanzia miaka 60 kwenda juu.

Muswada wa Uchaguzi wa wabunge 2020, uliwasilishwa na waziri wa sheria na katiba, Ephraim Kamuntu, Jumane jioni, ili pawepo sheria ambayo itaiwezesha serikali kushughulikia matakwa ya wazee.

Chini ya muswada huo kila mkoa utakuwa na mwakilishi mmoja mzee aliochaguliwa na baraza la wazee.

Ingawaje, mbunge mwanamke mzee atachaguliwa na Baraza la Kitaifa la Wazee, wajumbe wakitoka mikoa yote.

Tayari harakati za uteuzi wa wawakilishi mbalimbali ziko mbioni kwa uchaguzi mkuu wa 2021.

Sasa muswada huo utapelekwa kwa Rais Museveni kuuidhinisha, na kisha kuchapishwa katika gazeti la serikali kwa muda wa siku 14, kabla ya kuanza kutumika kama sheria kamili.

Kuna wabunge wachache waliopinga muswada huo wakidai kwamba tayari matawi yote matatu ya serikali yamejaa wazee wa miaka 60 au zaidi.
 
Wangeanzisha na huku kwetu atlist mzee wtu Wassira angepata pa kutokea maana anatia huruma
Yeye alikuwa serikalini miaka yote hiyo kama hakujiandaa jioni ndiyo hii karibu na mida ya kulala
 
Back
Top Bottom