Bunge la tisa likiongozwa na hayati Samuel Sitta(Speed and Standards)

satininus

Senior Member
Feb 11, 2021
135
171
Katika mabunge ambayo yalisisimua sana katika historia ya nchi yetu ni bunge la tisa likiongozwa na hayati Samuel Sitta(Speed and Standards).

Watanzania wengi tulikuwa tukilifuatilia sana na hata kambi ya upinzani ilikuwa imara.Lakini kilichotokea ni mnyukano mkubwa wa maslahi ndani ya CCM ukapelekea spika Sitta asiteuliwe kwenye bunge la 10,ndipo tukampata Anne Makinda.

Kimsingi modality iliyotumika kwa kiasi kikubwa ilishusha sana usimamizi wa mhimili wa bunge kama wajibu wake kikatiba kuisimamia serikali.

Abraham Lincoln alishawahi kusema "You cannot strengthen the weak by weakening the strong" pia "You cannot help the poor by destroying the rich".Hoja yangu hapa ni je bunge la 12 linauwezo wa kurejesha ukali wa mijadala chini ya usimamizi wa spika wa sasa daktari wa sheria Tulia Acson?

Na je chemistry ya wabunge zaidi ya 95% wakiwa ni CCM dhidi ya minority ya upinzani na huku kukiwa na utata wa covid 19?

Nini ufanisi wa bajeti hii ya 2022/2023 chini ya usimamizi wa bunge la 12?
 
Baada ya bajeti kupitishwa utekelezaji wake unaweza kuwafikia wananchi kwa ufanisi?Maana kazi mojawapo ya bunge ni kuishari na kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi.Mama amejitahidi sana kuifungua nchi na kuweka mazingira wezeshi kwa sekta za umma na binafsi hivyo kufanya utekelezaji wa bajeti kwa upande wa serikali kutokuwa na vikwazo vingi.Wasi wasi wangu ni je bunge linaweza kufuatilia kwa karibu?
 
Hatuwezi tukawa na bunge la kutegemea mpaka wawepo wabunge wa upinzani ndipo bunge lishauri na kusimamia serikali. Tunalalamika uchaguzi uliyopita na kilichotokea ila ukweli huwa wabunge wa ccm ndio huwa wengi na huutumia huo wingi wao kupitisha mambo yao.

Ukiacha huu uchaguzi ulipita,swali la kujiuliza kwanini bado wabunge wa ccm ndio huwaga ni wengi?
 
Back
Top Bottom