BUNGE LA TANZANIA ni NGONJERA.

Emma M.

JF-Expert Member
May 15, 2009
204
6
Bunge la Tanzania linafanya kazi kama wacheza NGOJERA.
Katika ngonjera, washiriki huanza kama kubishana lakini, mwishoni lazima wakubaliane.
Hakuna ngonjera inayoishia kwa kutokubaliana.
Hivyo ndivyo bunge letu watanzania lilivyo.
Hakuna bajeti yoyote itakayoachwa kupitishwa na wabunge hata kama ni uozo mtupu. Mwanzo huwa wanabishana sana na kutishia kuondoa shilingi: lakini mwishoni lazima bajeti ipite kwa maana kwamba wabunge wote wamekubaliana.
Hii ni ngonjrea tupu.
Wana jamii mwasemaje?
 
EMMA; huo ndo utaratibu, hata kwenye kahawa upo. pia unakumbuka secondari mambo ya proposer na opposers kwenye debate??
kilichoko ninachojua, pale hoja inawekwa mezani(mfano bajeti inasomwa) then wengine huruhusiwa kuchangia kwa utaratibu maaluu. kuna watakaoongea kwa msisitizo, kwa ukali, kwa maneno machafu, kwa hisia whatever ila mtu usitoke nje ya mada. pia kutokukubaliana katika hoja ndo afya ya kikao maana hizo ndo changamoto. mtu mbishi au anayekuwa tofauti na wengine kwa nia njema ni mzuri maana unaweza ukaona jambo lipo sawa kwa macho yako mawili but mwingine akaona kuna mapungufu na hii huweza kuchangiwa na udadisi, uzoefu, ujuzi nk. so kwa wabunge kubishana ni jambo la kheri na bunge ndo lina afya kuliko lile la MSEKWA before 2005.
naweza ongezea kwamba ngonjera za shuleni ndo nzuri sana katika kuwajenga watu kubishana na kuchangia mada kwa upana kwa kutafuta hoja kutoka kila nyanja.
ni hayo tu
 
Back
Top Bottom