Bunge la Tanzania na mtandao katika lugha ya kiingereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge la Tanzania na mtandao katika lugha ya kiingereza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkodoleaji, Jun 27, 2011.

 1. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani pamoja na kwamba kiingereza ni muhimu lakini kuna kushobokea kwingine kuna kera. Hivi hili bunge ni la wananchi au la nani? Sasa unakuta Bunge la Tanzania nchi ambayo wananchi wake wengi (karibu wote) wanaongea kiswahili unakuta mtandao umejaa kiingereza.
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wewe sasa umechemsha. Hivi hao wananchi unaowazungumzia wewe wana uwezon hata wa kufungua mtandao? Ukiona mtu amefikia kiwango cha kufungua mtandao huyo ameelimika na suala la lugha halitakuwa tatizo kwake. Lakini kule kwetu Ludewa issue ya mtandao ni ndoto na hiyo inammanisha mtandao ni kwa watumiaji wa nje au wale walioelimika na kujua kidhungu.
   
 3. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe sijui unaelewa unachokiongea au unataka kujifurahisha. Kama hao wananchi siyo wa muhimu inakuwaje sasa hivi serikali inahangaika na kutafsiri hizo bajeti na kuziweka kwa kiswahili au Mswaada wa Katiba kwa nini unatafsiriwa? Unajua kwenye suala la utawala bora kuna vitu vinaitwa uwazi (transparency) na ushirikishwaji (participation). Sasa kama kama unatumia lugha ambayo haieleweki kwa watu wengi unawezaje kudai wewe ni muwazi? Na pia kivipi unaweza kushirikisha watu kitu ambacho hawakielewi.
   
Loading...