Bunge la tanzania lageuka jumba la sanaa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge la tanzania lageuka jumba la sanaa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by manuu, Jul 11, 2012.

 1. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Ukijaribu kufuatilia shughuli za bunge zinazoendelea kule mjengoni utakubaliana na mimi hata POSHO na hizo SITTING ALLOWANCE wanazolipwa ni bure kabisa na ni matumizi mabaya ya pesa zetu sisi walipa kodi.
  Kwa nini nasema hivi unakuta wakati muswada wa bajeti ya Wizara fulani unapojadiliwa wachangiaji wote bila kujali itikadi ya vyama vyao wanaonyesha ukali juu ya bajeti iliyo mbele yao kwamba haikizi vigezo na haiwezi kumsaidia mwananchi.
  Wengi wao inafikia wanatoa kauli kali sana juu ya serikali yao kitendo kinachorudisha imani kidogo kwetu sisi wananchi kwamba kweli hapa hii bajeti haitapitishwa.
  Balaa sasa inakuja kwenye kuhitimisha hiyo bajeti Mbunge yule yule aliyesema bajeti hii haiwezi kumsaidia mwananchi wake Unamsikia akisema naunga mkono bajeti asilimia mia moja(100%).
  Huwa napata wakati mgumu sana kuweza kuelewa wabunge wale wapo kwa maslahi ya nani pale,
  Kwa nini anapitisha kwa 100% bajeti ambayo tayari wameshaona ina mapungufu mengi na si yakumsidia mwananchi.

  Wito wangu kila wananchi tujaribu kuwabana hawa wabunge wanaporudi majimboni walau watueleze kwa nini walipitisha bajeti ambayo tayari walishajua si ya kumsidia mwananchi na haina maslahi na mwananchi.
  Ni matumani yangu tukianza kuwabana kwa maswali pindi warejeapo majimbini kikao kijacho kitakuwa cha maslahi kwetu sisi wananchi.
  WANAOUNGA MKONO HOJA WASEME NDIYO.
  WASIYOUNGA MKONO HOJA WASEME SIYO.
   
 2. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Ni sawa tunaweza kuwabana wabunge hawa kwa huo usanii wao wakirudi majimboni, lakini sasa kuna majimbo kadhaa hii haitawezekana mfano Tabora mjini , mbunge wao msomali ADEN RAGE tangu awaingize mjini wakampa ubunge huwa harudi jimboni , yeye na timu ya simba tu je! sasa watamhoji wapi? mtoa mada naona tutafute mkakati mwingine wa kuwabana , majimboni baadhi hawarudi kama huyu RAGE
   
 3. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Hao ndio design ya wabunge wa ccm(choo cha makuti).wanapinga mwisho wanakubali upumbavu walio upinga awali,,,,,,,,majanga nchi hii mengi wakiwamo hao wabunge wa mabwepande kama stela manyanya
   
 4. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mimi naona wanapoteza muda na kodi zetu tu. Inabidi watanzania tubadilike sana kuwachangua hawa Wabunge, hawana tija kabisa!
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,199
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi mpaka nisikie ni mbunge wa CDM anachangia na kidogo NCCR lakini wengine nabadilisha channel mithili ya mwendo wa mwanga
   
 6. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mpaka chama cha mabwepande kiondoke madarakani ndo tuanze upya.Kwa sasa hakuna lolote
   
 7. Clarity

  Clarity JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 6, 2010
  Messages: 811
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 80
  Napata wakati mgumu mbunge anajadili hotuba ya bajeti ya wizara Fulani huku akikosoa mambo mengi sana
  mwisho wa majadiliano utamsikia naunga mkono 100%
  ???????!!!!!! agh upuuzi mtupu
   
 8. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #8
  Jul 11, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Haya ni matokeo ya ku-invest ujinga kwenye vichwa vya wapiga kura...
   
 9. L

  Lugeye JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 1,078
  Likes Received: 1,378
  Trophy Points: 280
  hawa wabunge wa mabwepande ndo wanaharibu utamu wa BUNGE
   
 10. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  Si kweli tumeinvest kwenye ujinga, bali hila ni nyingi mno kwenye uchaguzi , ambapo dola, TISS, tume ya uchaguzi(NEC) wamekuwa wakitumika sana kuhakikisha CCM inashinda chaguzi katika majimbo mengi.Si kweli kuwapiga kura ni wajinga kiasi hicho, mfano uchanguzi wa 2010, majimbo ya tandahimba, kibaha,shinyanga mjini,magu, majimbo haya ccm ninauhakika walipoteza, lakini kwa kutumia dola, ccm ikashinda wakishinikiza (NEC) kuwatangaza wagombea wa ccm.Kwahiyo , ni jambo la msingi sasa kuendeleza kuonyesha kuwa ccm ilishinda kwa hila kwa kuzionyesha hila hizo kama kuwa na wabunge wanaokubali bajeti mbovu huku majimbo yao wakisurubika na janga la maisha mabovu kwa matatizo ya ardhi, maji, umeme, bei ndogo za mazao, elimu duni, afya duni hasa afya ya msingi n.k
   
 11. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Haya ni Matokeo ya CCM Dhaifu ndiyo imeleta haya yote wao ndiyo wanaongoza kwa Ndiyoooooooooooooooooooooooo na Kuunga mikono na Miguu 200%. Mi sina haja ya kumbana mbunge wangu coz aliongea tuliyomtuma ila waliowengi(CCM Dhaifu) wakaona kuwa wao ndiyo wanalipa $ kodi.
   
 12. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  We kijana utakua wa TBR wewe, alituhadaa kwa kijiredio chake. Nadhani kinapoteza mvuto sasa kwa ujio wa redio tofauti tofauti. Mtu wa fitna sana yule ndo kinachompa jeuri ila 2015 I will stand against him in public, ntatangaza chama in days to come.
   
 13. cmoney

  cmoney JF-Expert Member

  #13
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 1,224
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Jamaa walipokuwa wamesimamia sera za jembe na sururu walikuwA watam sana sema sijui Kwanini walijisahau
   

  Attached Files:

 14. Ston Merchant

  Ston Merchant JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 395
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hayo ndo matokeo ya kuotesha chumvi........!
   
 15. D

  Dabudee Senior Member

  #15
  Jul 12, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 156
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nasikia huwa wanaimba wimbo wa "DANGANYA TOTO JINGA MASIKIO KAMA POPO" na kiitikio chake huwa ni poa tu wengi mnakifahamu I believe.
   
 16. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mwenzangu weye....
   
Loading...