Bunge la Tanzania kuanza vikao leo. Spika Ndugai awapongeza wabunge kwa kuuliza maswali mafupi mafupi

Ukitizama bunge mahiri na madhubuti kama la Marekani, halafu ukaja ukatizama bunge la Ndugai, unahisi kupata kinyaa.

Bunge goigoi, bunge butu, bunge dhoofu, bunge chefu chefu, bunge legevu, bunge tepetevu.

Tunahitaji constitutional reforms tupate bunge imara. Bunge madhubuti.

Hawa wapiga makofi hawaisaidii nchi. Wanapoteza wakati tu.
 
Bunge letu tukufu,linalowakilisha watanzania wote wakiwemo Bavicha,chini ya kiongozi imara J.Ndungai na Dr.Tulia linaanza kuunguruma Dodoma makaomakuu ya CCM na serikali.
 
Spika Ndugai amesema anawapongeza sana wabunge kwa weledi wa kuuliza maswali mafupi mafupi tofauti na wale wa bunge lililopita maswali yao yalikuwa yanajaa ukurasa nzima.

Ndugai amesema swali likiwa refu linapoteza hata maana na kuwa sawa tu na kutouliza.

Source Star tv

My take; Nimeyakumbuka maswali ya Tundu Lissu na J J Mnyika!
 
Kikundi cha wahuni kilichopitishwa na nec ,kimeenda kukutana dodoma ....huku wakigawana pesa za kodi za wavuja jasho watanzania
 
kuanzia leo naomba watanzania wenzangu tuanze kuwa tathimini wabunge wetu tulio wachagua, je? wanatusemea kero zetu au wanenda kustarehe?

Je, wanatoa njia kutatua kero zetu au wamefunga midomo?

tuwafuatilie na tutoe maksi kila siku kwa kila mbunge
Mimi sikumchagua mbunge yeyote kwa hiyo sina mbunge
Jiongeleee mwenyewe na mbunge wako uliomchagua wewe
 
hujamchagua lkn ndio mbunge wa jimbo lako, huna jinsi, hakikisha anatatua changamoto zilizopo ktk jimbo lako kwa masilahi ya ndugu zako wanao ishi huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tokea Nina akili zangu sijawahi hata siku moja kuwasiliana na hao viongozi wa kisiasa ili watatue shida zangu,
Ninafanya mambo yangu Mimi mwenyewe simtegemei sijui mwenyekiti ,mbunge , Wala Rais
Ndio maana sipigagi kura
 
Back
Top Bottom