Bunge la Tanzania kuanza vikao leo. Spika Ndugai awapongeza wabunge kwa kuuliza maswali mafupi mafupi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,776
2,000
Mkutano wa pili wa Bunge la 12 unatarajiwa kuanza leo Februari 2 hadi Februari 12 mwaka huu jijini Dodoma.

Taarifa ya Ofisi ya Bunge imeeleza kuwa katika mkutano huo shughuli zitakazofanyika ni pamoja na maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu yanayotarajiwa kuulizwa na wabunge.

Pia, wabunge watapata fursa ya kujadili hotuba ya Rais ya ufunguzi rasmi wa Bunge la 12 na kujadili na kushauri kuhusu mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2021/2022.

--
Spika Ndugai amesema anawapongeza sana wabunge kwa weledi wa kuuliza maswali mafupi mafupi tofauti na wale wa bunge lililopita maswali yao yalikuwa yanajaa ukurasa nzima.

Ndugai amesema swali likiwa refu linapoteza hata maana na kuwa sawa tu na kutouliza.
 

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
1,983
2,000
Kuanzia leo naomba watanzania wenzangu tuanze kuwa tathimini wabunge wetu tulio wachagua, je? wanatusemea kero zetu au wanenda kustarehe?

Je, wanatoa njia kutatua kero zetu au wamefunga midomo?

Tuwafuatilie na tutoe maksi kila siku kwa kila mbunge.
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
22,397
2,000
Ni Mbunge ama kikundi cha wana CCM wachache waliojichagua wenyewe kwa wenyewe kwa kutumia Tume yao ya uchaguzi kuhalalisha matokeo ya uchafuzi

Tunaambiwa wanakwenda kumwongezea baba yao miaka ya kutawala - Kweli kabla ya kufa tutashuhudia mengi nchi hii - cha kwanza kinaweza kuwa hiki -
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom