BUNGE LA TANZANIA HALINA MAMLAKA YA KUHOJI UTENDAJI KAZI WA RAIS
KATIKA ANDIKO HILI NIMELENGA KUELEZA YAFUATAYO;
Kwanza nitaeleza kuwa Bunge la Tanzania halina mamlaka ya kuhoji utendaji kazi wa Rais katika mambo ambayo hayapelekei kuwepo kwa hoja ya kumuondoa Rais Madarakani kwa mujibu wa kifungu cha 46A Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Pili nitaeleza sababu za kwanini Bunge la Tanzania halina mamlaka ya kuhoji Utendaji kazi wa Rais wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba yetu. Na Tatu nitaonesha utofauti wa Mamlaka ya Mabunge ya Africa Kusini na Kenya juu ya Mamlaka yao juu ya kuhoji utendaji kazi wa Rais katika nchi hizo. Na Mwisho nitatoa Mapendekezo yangu juu ya nini kifanyike.
Hivi karibuni tumeshuhudia baadhi ya Wabunge wakihoji sana utendaji kazi wa Rais kuhusiana na baadhi ya hatua za kimageuzi ambazo zilikuwa kilio cha muda mrefu sana kwa Watanzania. Eneo moja la mfano ambalo Rais amelichukulia hatua katika mamlaka yake yeye Kama Rais wa Nchi ni Kujua usahihi wa kiasi cha dhahabu kilichomo katika mchanga unaosafirishwa nje ya nchi ambapo awali Wawekezaji walitueleza ni Kilogram 2.8 – 4.0 kwa Kontena lakini Kamati iliyoundwa na Rais imegundua ni karibu Kilogram 28 kwa Kontena moja na ni wastani wa Makontena 2000-3000 kwa mwezi yalikuwa yanasafirishwa nje ya nchi.
Wabunge hasa wa Upinzani wameibuka na hoja ya kukosoa njia iliyotumika kuzuia mchanga huo na wengine wakikosoa hatua hizo alizochukua Rais wa Nchi kuzuia uwizi wa dhahabu yetu kama taifa. Sitaki kueleza wajibu wa mamlaka katika kukamata wezi. Napenda kujiuliza ni wapi hasa Bunge limeyatoa mamlaka ya kukosoa utendaji kazi wa Rais kiasi kile hadi inafikia hatua Wabunge wanavunjiana heshima zao huku wakiwa wanajadili jambo ambalo kisheria hawana mamlaka nalo? Je, ni kwanini Viongozi wa Bunge wanaruhusu mijadala ya kujadili utendaji kazi wa Rais bila kueleza wanatoa wapi mamlaka hayo katika sheria zetu za Tanzania? Niseme mapema kuwa siwalengi wabunge kukosoa utendaji kazi wa Rais wakiwa nje ya bunge kama Raia wa kawaida, lakini nahoji mamlaka ya Bunge kama mhimili wa Mamlaka ya Dola wameyatoa wapi mamlaka hayo?
TUELEKEE KWENYE KATIBA YETU: Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 pamoja na mabadiriko yake kupitia kifungu cha 4 imegawanya mamlaka ya Kiutawala kwa Mhimili wa Serikali, Mamlaka ya Kutunga sheria kwa Mhimili wa Bunge na Mamlaka ya Kutafsiri sheria kwa mhimili wa Mahakama. Rais Wa Jamhuri wa Muungano ndiye kiongozi wa Mmhili wa Serikali kwa mujibu wa Kifungu cha 33(2). Na hata viongozi wengine wote wa serikali wanapotekeleza majukumu yao wanafanya hivyo kwa niaba ya Rais lakini tuu kwa namna ambavyo Rais ameruhusu wayatekeleze majukumu hayo. Hivyo Viongozi wote wa Serikali uwajuao wanamuwakilisha Rais katika utekelezaji wa majukumu yao kwa mujibu wa kifungu cha 35. Katiba ya Afirca ya Kusini ya 2010 nayo inaeleza kuwa Rais ndiye kiongozi wa Serikali kwa mujibu wa kifungu cha 83(3) na Kenya mamlaka hayo amepewa Rais kupitia kifungu cha 131 (Katiba ya 2010). Katika Uongozi wa Nchi kwa mataifa haya matatu mamlaka waliyopewa Viongozi wa nchi yanafanana sana. Tofauti yao ipo kwenye uwajibikaji wao juu ya mamlaka waliyopewa viongozi hao kama itakavyoelezwa hapa chini.
Kwa upande wa Tanzania msisitizo wa Mamlaka ya rais wa nchi katika kusimamia na kutekeleza majukumu yake ya kiserikali umeelzwa tena kupitia kifungu cha 53(2) ambacho kinaeleza kuwa serikali ya muungano ipo chini ya mamalaka ya Rais ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera ya serikali kwa jumla. Kwakuwa Rais hawezi kutekeleza majukumu yake yote, Katiba inaweka utaratibu kwa Rais kupitia kanuni atakazoweka, kutoa amri na maagizo ya utekelezaji wa majukumu kwa viongozi wengine atakao wateua.
Kimsingi; Ukimuondoa makamu wa Rais, Watumishi wengine wa serikali waliokasimiwa mamlaka ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali na Rais akiwemo Waziri Mkuu pamoja na mawaziri wao utendaji kazi wao wa utekelezaji wa majukumu waliyopewa na Rais unaweza kuhojiwa na Bunge kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Lakini Mamlaka aliyobaki nayo Rais, au Rais anapoamua kutekeleza jambo lolote alilo na mamlka nalo basi katiba haitoi mwanya kwa chombo chochote kumhoji utendaji kazi wake. Kifungu cha 53 (2) kinaeleza moja kwa moja kwamba Waziri Mkuu pamoja na Mawaziri ndio watawajibika kwa Bunge kuhusu utekelezaji wa shughuri za Serikali ya jamhuri wa Muuungano wa Tanzania.
Ikumbukwe pia chini ya kifungu cha 52(2) Waziri Mkuu ndiye mwenye madaraka juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuri za serikali ya jamhuri ya Muungano. Swali, je Waziri mkuu anamadaraka juu ya Kazi za serikali azifanyazo Rais (kazi ambazo Rais hajampa kiongozi yeyote azifanye au Rais ameamua kuzifanya yeye mwenyewe kama hili la kuzuia Makontena ya Mchanga)? Jibu ni Hapana. Na ni dhahiri kuwa kazi za serikali ambazo Waziri Mkuu anamadaraka nazo ya usimamiaji na udhibiti na utekelezaji ndio hizo alizokasimiwa na Rais wa Jamhuri na ndizo hizo ambazo chini ya kifungu cha 53(2) Bunge linaweza kumuwajibisha yeye Waziri mkuu na Mawaziri kwa pamoja. Ni muhimu kueleza hapahapa kwamba Katiba ya Tanzania haielezi kazi za kimamlaka za Rais Kama mkuu wa nchi ambazo hakuzikasimu kwa Viongozi wa chini yake au kaamua kuzitekeleza yeye mwenye atawajibika kwa nani. Hivyo chombo chochote kumhoji Rais Utendaji wake wa Kazi Kikatiba sio sahihi. Kwamaana nyingine utendaji kazi wa Rais Unahojiwa kwa Sanduku la Kura tuu katika uchaguzi Mkuu.
Katiba ya Afrika Kusini imeeleza wazi kabisa kwamba “Baraza la Mwaziri” la nchi hiyo litawajibika kwa Bunge juu ya utekelezaji wa majukumu yao kwa mujibu wa kifungu cha 92. Rais na Makamu wa rais wa nchi hiyo ni wajumbe wa baraza la mawaziri la nchi hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 91 na hivyo Rais anawajibika kwa Bunge kama ambavyo waziri Mkuu wa Tanzania anawajibika Kwa Bunge. Pia Kwa Nchi ya Kenya, katiba yao kupitia kifungu cha 95 (5) (a) kinaeleza ya kwamba Bunge la nchi hiyo (National Assembly itakuwa na wajibu wa ku-review (kukagua/kuhakiki/kupitia) mienendo ya ofisi ya Rais na makamu wa Rais na watumishi wengine wa Serikali hiyo. Pia, Kifungu cha 95(5)(b) kinaipa Mamlaka Bunge la nchi hiyo mamlaka ya ku-Oversight (Kusimamia/uangalizi) wa mihimili miingine ya Dola. Haya ni mamlaka makubwa sana kwa Bunge la Kenya juu ya Mihimili mingine ya Dola ambayo kwa Bunge la Tanzania hayapo.
Kwa maelezo hayo ya namna Mabunge ya nchi hizi mbili yalivyo eleza kiuwazi juu ya mamlaka ya Bunge kuhoji utendaji kazi wa Marais katika mataifa yao ni dhahiri kuwa kwa nchi hizo kitendo chochote ambacho Rais wa Nchi angekifanya au atakifanya Mbunge anaweza akainuka na kuhoji moja kwa moja utendaji kazi huo wa Rais. Hili ni Tofauti na Tanzania ambapo Rais sio Tuu hapaswi kuhojiwa utendaji wake na Bunge, Bali Katiba ya Tanzania inaeleza zaidi ya Kwamba RAIS WA TANZANIA NI HURU. Yako mambo ambayo sheria na Katiba ambayo yanaweza kumtaka Rais afanye jambo kulingana na ushauri alio pewa, lakini Kwa ujumla wake Rais Wa Tanzania anapewa mamlaka na Katiba ya Tanzania Kutolazimika kufuata ushauri anaopewa na chombo chochote likiwemo na Bunge katika eneo la utekelezaji wa majukumu yake.
Jambo la msingi ni kuwa Katiba ya jamhuri wa Tanzania ilitungwa kwa namna ambayo Rais wa Nchi anapaswa kuwa huru katika utekelezaji wa majukumu yake na hivyo kumuepusha na ushwishi wa kishabiki wa chombo kama bunge ambapo mijadala mingi hutawaliwa na hisia za kisiasa kuliko mahitaji halisia ya nchi na watanzania. Hivyo kwa kipindi chote ambacho baadhi ya wabunge wamekuwa wakitumia jukwa la Bunge kuhoji utendaji kazi wa Rais wamekuwa wakivunja katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Na Viongozi wa Bunge Spika na Naibu Spika kwa Kipindi chote ambacho wameendela kuruhusu Wabunge Kumhoji Rais juu ya Utendaji kazi wake Wamekuwa wakiendekeza uvunjifu wa Katiba na hivyo kupelekea Bunge kutotekeleza majukumu yake ipasavyo yaliyopo kikatiba.
Kwakuwa ni dhahiri Bunge La Tanzania halina Mamlaka ya Kumhoji Rais Wa Tanzania isipokuwa tuu pale imeletwa hoja ya kumuondoa Rais Madarakani chini ya kifungu cha 46A, ni ushauri wangu kwa Uongozi wa Bunge na Serikali kwa ujumla ya kwamba.
Mijadala yote inayohusu utendaji kazi wa Rais isitishwe na isiruhusiwe ndani ya Bunge kwani inakinzana na utaratibu uliowekwa na Katiba chini ya Kifungu cha 37(1) 53(2) cha Katiba.
Kamati ya Bunge iliyoundwa kuchunguza swala la Mchanga halina uhalali Kikatiba kwa Kuwa Bunge halina mamlaka kuchunguza au kuhoji jambo lolote alilolitenda Rais wa Nchi kama nilivyoeleza katika andiko Hili. Zaidi, fikiria nini iitatokea endapo Kamati ya Bunge ikija na matokeo tofauti na Yale ha tume za Rais mbili ambapo ya kwanza ishatoa matokeo na ya pili inataraji kutoa matokeo hivi karibuni? Sioni umuhimu wa Kamati hiyo na ni ishara ya kwamba hawamwamini Rais na Tume yake. Na zaidi Natambua mamlaka ya Bunge kuunda Kamati kuchunguza jambo lolote linalohisiwa kuhitaji kuchunguzwa lakini sio sahihi kikatiba Bunge kuunda kamati Kuchunguza jambo ambapo Rais ameishaanza kulifanyia kazi kwakuwa itakuwa ni kumchunguza Rais au kumhoji Rais kitu ambacho bunge halina mamlaka nayo. Ingekuwa sahihi kabisa ikiwa Bunge lenyewe ndio lingeanza kuchunguza kabla ya Rais.
Spika na uongozi wa Bunge kwa jumla usimamie kanuni zao na Katiba kwa weledi mkubwa ili kurudisha Bunge katika njia nyoofu ya kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.
Kwakuwa ni dhahiri Awamu ya Tano ni awamu ya mabadiriko makubwa ya kuiwezesha nchi kujikomboa kiuchumi na hivyo ni dhahiri minyororo mingi ya unyonyaji inaendelea kukatika ili nchi ijikomboe na kwa kuwa wamiliki wa minyororo ya unyonyoji hiyo wapo na wanapingana na hatua hizi za kiserikali na kwakuwa tayari katika hatua moja wapo hii ya kuzuia mchanga wa madini usisafirishwe nje ya nchi imepelekea mjdala makali sana bungeni kiasi cha baadhi ya wabunge kushutumiana kwamba wapo wabunge waliopewa rushwa na baadhi ya wamiliki wa minyororo ya unyonyaji, basi Serikali na Bunge kwa haraka wafanye yafuatayo;
Yainishwe maeneo ambayo Rais Wa Nchi atayasimamia yeye Mwenye ili Bunge lisiweze kujadili kwa kuwa vita tuliyonayo ya ukombozi wa kiuchumi ni kubwa kiasi cha kuweza kuwepo na baadhi ya viongozi wanaoweza kutumika kutuvuruga kwa kushirikiana na wenye Minyoyoro ya unyonyaji (Political and economical Puppets)
Maeneo hayo ambayo yatakuwa chini ya mamlaka ya Rais moja kwa moja yainishwe na yasijadiliwe na bunge kabisa hadi pale Rais wa nchi atakapotaka yajadiliwe kwa adidu atakazokuwa ameelekeza
Kwa wakati huu wa mpito, zitungwe kanuni za Bunge ambazo zitaeleza namna ambavyo wabunge watajiepusha kujadili mambo ambayo yanalenga kukomboa nchi kiuchumi na kwamba wataweza kujadli kwa namna ambavyo Rais ataweza kuelekeza.
Bunge lijiwekee utaratibu wa kutoa Tamko la kimamlaka kuunga mkono jitihada au hatua za Mamalaka ya Rais katika maeneo ya Kujikomboa kiuchumi ili lijitofautishe na wale ambao wanadaiwa kuwa puppets wa Wamiliki wa Minyororo ya Unyonyaji.
Bunge Lieleze wazi Kwamba Harakati za Kujikomboa kiuchumi ni jambo mahususi na la kipaumbele Kwa taifa na halihitaji kudhihakiwa wala kubezwa na Wabunge na adhabu kali zitolewe kwa Wabunge watakao kiuka hili wakiwa nje au ndani ya Bunge.