Bunge la Tanzania ambalo si bunge (halina mashiko) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge la Tanzania ambalo si bunge (halina mashiko)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by King Suleiman, Jul 8, 2011.

 1. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Salaam wana JF,
  nimekua nikifuatilia bunge letu la JMT kwa muda mrefu sasa mwaka huu na kuja kugundua kwamba Bunge letu kumbe si bunge kwa tafsiri halisi kama chombo cha kuwakilisha wananchi na badala yake wabunge wamekua watetezi wa vyama vyao na sio maslahi ya taifa

  kuna baadhi ya wabunge wanajitoa ufaham na akili zao na bila aibu wana pinga hoja za msingi kisa zimetolewa na mbunge wa chama ambacho si chake, kwa hakika ni aibu kwa taifa kuona tuna wabunge wa namna hii ( tena wengine wana umri mkubwa) lakini wana act kama watoto kwa kujitoa ufaham kisa ulaji wa vyama vyao ni aibu kubwa sana, wanashangilia upuuzi na wakati mwingine kutetea mambo binfsi.

  yote tisa, kumi ni spika na naibu wake, wasanii kupitiliza, wanakandamiza wengine wazi wazi na kutetea chama chao, wanatoa miongozo ya kipuuzi kabisa ( kama huyu naibu Ngugai anafurahia kabisa wabunge kutukanwa kwamba wanapenda show za kuonekana kwenye TV), kwa hakika hawa si marefa wazuri bali ni watetezi wakubwa wa walio waweka hapo.

  kwa sasa ni bora kuangalia hata mchezo wa kuigiza kuliko hili bunge la Tz ambalo usanii wake umezidi, maana hamna wanachojadili kwani kila kinachopangwa na serikali kina pita bila kupingwa, ni aibu sana kwa taifa letu kua na bunge la namna hii lisilo na tija wala faida kwa wananchi walio wachagua hao wawakilishi.

  poleni sana watanzania kwa kuchagua wabunge wengi vimeo wanao tetea maslahi yao binafsi na ya vyama vyao badala ya kuwatetea nyie mlio watuma, NATUMAI HAMTAFANYA FANYA KOSA HILI TENA.
  MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 2. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  wabunge wengi wapo tayari kujidhalilisha utu wao kwa kutetea mslahi ya chama na kuishia kupiaga kelele za Ndiooooooooooooooooo, na kuziumiza meza za bunge kwa kuzipiga na kushangilia ushambenga wa kipuuzi, ni aibu sana kwa taifa letu.

  NAMUOMBA MUNGU SIKU MOJA NIONE BUNGE LENYE TIJA NA FAIDA KWA NCHI YETU, hili la sasa si bunge ni kijiwe cha kwenda kupoteza muda na kupigishana story huku maamuzi yakiwa tayari yameshafanywa na watu wengine, inaumiza sana
   
 3. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Ndio maana tunahitaji kuzidisha nguvu na shinikizo la kupata katiba mpya. Ni katiba mpya pekee itakayoweza kubadilisha utamaduni huu wa kishenzi ambao tumeufikia. Bila katiba mpya tujiandae kuendelea kuangalia sinema ya bure, no sio sinema ya bure bali sinema ambayo tumelazimishwa kuilipia (kodi zetu ndizo zinawaweka katika jumba hilo la maigizo). It's sad
   
 4. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  nakuunga mkona Mpiga zeze, kwa kweli tunahitaji katiba mpya kukomesha huu upuuzi ambao kwa hakika una ligharimu taifa letu, hakuna wanachofanya pale dodoma zaidi ya kufanya maigizo, ni wabunge wachache sana wapo serious, wengi wao mm nawaona wapoa kama ze komed na wasanii wengine sema tofauti yao wao badala ya kutuburudisha wana tuletea kero kwa maamuzi yao yasiyo na faida kawa taifa, kazi kula kuku tu wakati nchi ipo gizani, shame on them
   
 5. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Hiyo Red nimeipenda sana ndugu. Wabunge wa chama kile akiongea mtu ambaye si wa chama chake wanawasha MIC kinyemela wanatumbukiza maneno ya vijembe kama kwenye taarabu.....Kaka usiumize kichwa kabisa mbona 2015 hao hao ndio wanapitishwa tu kutokana na sisi wenyewe kuendelea kulala tu.
   
 6. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  kwa hakika ndg yangu, lakini inabidi tupambane kwa kuwaelimisha ndugu zetu wengine na watanzania wengi hasa wa vijijini wanaorubuniwa kwa kanga na kofia na pesa za pombe kwa mwezi mmoja mateso miaka mitano, la sisvyo huu upuuzi utaendelea kututesa sana na maigizo wanayofanya kule Dodoma kama vile hawana la kufanya
   
 7. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  I support you, hili bunge limekaa kimipasho sana.
   
 8. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2011
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 1,826
  Trophy Points: 280
  Waunge wa CDM msife moyo endeleeni hivyo hivyo sisi wananchi tunaona hayo yote yanayoendelea bungeni. Jana nilikua sehemu moja ya public naangalia bunge kwa kweli yale majibu ya Ndiyooooooooo yalikua yanawakera sana wananchi kuna watu walipatwa na hasira na walikua wanatamani hata kuvunja TV. Acheni waendelee na ndiyoooo zao kwenye mijadala ya maslahi ya Taifa wananchi wanaona na wanazidi kupatwa na hasira sana. nadhani siku wafanye utafiti waje wakae kwenye public waangalie mijadala inavyoendeshwa then waone reaction za wananchi nadhani wanaweza kubadilika vinginevyo wanazidi kuwapa mtaji mkubwa sana CDM.
  Nilimpenda sana Tundu Lissu na Mnyika walikua wanakazania kua hatutoi shilingi for the records. mibunge ya CCM hata haikushtukia kua hilo ni bomu maana hizo records tutaletewa wananchi tuone jinsi gani watu wanavyozidi kutukandamiza.
   
 9. khayanda

  khayanda JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 248
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Msitugombanishe na serikali yetu kama tulijua ni mbaya tusingeichagua, tuliambiwa hatukusikia, tuliona hatukuamini sasa matokeo yake tuyakubali, nchi imeshikwa na wasanii watupu wacha wale tuombe wapasuke matumbo kabla hawajamaliza vyetu. Ila tujipange sawasawa kwa 2015 tujiandikishe kupiga kura, tukapige kura na tusiondoke vituo vgya kupigia kura hadi tuambiwe matokeo yote ya kura zetu.
  Msishangae kuona Lowasa ndiye changuo lao
   
 10. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Na wewe ni mmoja wao, mbona unajitoatoa wakati na wewe ni mtanzania? Pamoja na kwamba maumivu tunayasikilizia wote tulifanya kosa moja kubwa kwa kutowakataa walioingia madarakani kwa nguvu ya kuchakachua.

  Kwa taarifa yako, watanzania hawakuwapigia kura za kutosha bali walijitangazia ushindi na sisi tuka kaa kimya bila kuwatimua kwa nguvu. kosa hilo ndolo linalotughalimu. Tukiendelea hivi wataendelea kuchakachua na kubaki madarakani hata kama hawatapata kura japo moja! Cha msingi kama wakijitangazia ushindi tufanye kama Ivory Coast!

  Serikali na wabunge wake hawana cha kufanya zaidi ya usanii kwani hawakuchaguliwa na wananchi bali tume ya uchaguzi.
   
 11. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #11
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  asilimia ya watu wengi wananagalia bunge kwa sababu ya hao wachache wapinzani maana wanatoa hoja zenye mashiko lakini so hawa vibaraka wa ccm.kina wasira .....
   
 12. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #12
  Jul 9, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45

  ni kweli Anko, hata mm ni mmoja wao, bt roho inanniuma sana kuona jinsi tunavyofanyiwa usanii sana palle Dodoma, ni heri hata bunge lingekua linakaa kwa siku mbili tu kuliko wiki nyingi huku hakuna kinachofanyika zaidi ya usanii na upuuzi tu, huku wakijisifu kwa mbwembwe KWA MASLAHI YA TAIFA ni heri hata waseme kwa maslahi ya chama tungeaelewa kdg
   
 13. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #13
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,093
  Likes Received: 505
  Trophy Points: 280
  Maadui wakubwa wa taifa letu ni hawa wabunge wa aina hii! They real let us down.Mungu awalipe sawa na stahili zao.
   
 14. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #14
  Jul 9, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  ni kweli mkuu wana liangusha taifa hili kwa manufaa yao binafsi na kwa taasisi zao za siasa
   
 15. m

  menny terry Senior Member

  #15
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mimi huwa nikisikia saa ya mnyika au Peter msigwa kutoa mada ndo huwa na kaa kusikiliza.
   
 16. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #16
  Jul 10, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Bunge halina mshiko ukiwa na maana ya fedha? Au mashiko ukimaanisha hoja?
   
 17. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #17
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nilipo RED.

  Hayo sio mambo ya kugundua bali kwa mujibu wa katiba ya JMT. Kila mbunge anawakilisha chama chake na sio wananchi waliomchagua. Niliandika kwenye bandiko langu moja hapo awali bandiko lililonena kuwa wabunge wa JMT wanawakilisha vyama vyao si wananchi kwa kuichambua na kuisasambua katika kufanua hilo.

  Nafikiri wakti muafaka kwa WaTanganyika kudai katiba mpya ili kumfanya mbunge kumwakilisha wananchi aliyemchagua na sio chama chake cha siasa.

  Hongera kwa kuliona hilo.
   
Loading...