Bunge la Taifa lizungumzie kitu gani?

Huduma

Member
Jan 26, 2008
68
1
ZIPO hisia kuwa imefikia wakati wa kuchambua na kunyambua ni nini hasa wabunge wa Bunge linaloitwa la Taifa wawe wanazungumza wanapokuwa wanalipwa posho nono wakati wa vikao muhimu vya kitaifa.

Mtu ana haki ya kuzungumza lolote lile analotaka mahala popote hapa nchini. Lakini sivyo, au sivyo inavyotakiwa katika Bunge la Taifa. Bunge la Taifa linatakiwa lizungumzie masuala muhimu na mazito ya kiuchumi, kijamii, kitamaduni, kiteknolojia na kisiasa katika ngazi ya taifa na sio mkoa, wilaya au tarafa au jimbo eti!

Hali iliyopo hivi sasa inahitaji REDET au wajanja wengine wale kwa kulishauri NCHI juu ya mustakabali wa kile kinachostahili kufanywa na wabunge wabunge la taifa. Inavyoonekana kuna masuala ya Uwakilishi kwa vikundi vya washikadau mbalimbali-basi tuangalie wa kuwa na uwezekano wa bunge linaloweza kutumia masaa kadhaa kuzungumzia posho na maslahi ya watu. Hii sio nchi ya kijamaa tena jamani au sio au ndio? Vipi? Unashangaa? Hata wao wenyewe hawajui ni wajamaa au ni watu gani?
Sembuse iwe mimi?

Kama kuna masuala ya Kimkoa mkoa, jamani, wabunge wa mkoa husika labda mkichanganyikana na mangi meza kadhaa na wawakilishi wengine muwe na bunge lenu myazungumzie huko. Jamani ambulensi wilayani kwenu au jenereta kwenye shule wilayani kwenu hili ni jambo la kuzungumziwa na Bunge la taifa. Au kwa akili yetu hatujui kuwa MUDA ni RASILIMALI pia. Na muda tofauri na rasilimali nyingine haina salio?

Ili kuwatanabaisha na wanaobabaika katika kutofautisha lipi lizungumzwe na Bunge la Taifa na yepi yazungumzwe na Mabunge ya Mkoa au Bunge la Uwakilishi kutokana na shughuli au kazi watu wanazofanya nawapeni mifano hii hapa chini:


Mshauri sikiliza hoja hizi toka bungeni kisha tupe ushauri zinafaa mahala hapo:

HOJA 1
Spika: Mheshimiwa Mbunge wa Njaakali yeye ana maswali mawili Kwa Naibu, Naibu Waziri, karibu mheshimiwa.

Mbunge Njaakali: Hospitali ya Jimbo langu wanakula wali mara moja tu, je, Wizara husika ina mpango gani wa kuongeza siku za wali na ikiwezekana pilau na briani?

Mshauri: Hii ni hoja iliyotakiwa kutolewa katika Bunge la Mkoa [kama lingekuwepo na sio Bunge la Taifa-tena taifa la nchi mbili zisizounganika sawasawa!]

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
HOJA 2
Mbunge 1: Askari hawalipwi mishahara [kama yetu?] sasa hawa watu wanatulinda basi wapande mabasi bure!

Mbunge 2: Nauli hizi zinawatosha kabisa wenye daladala wao kazi yao ni uroho tu ndio maana wanadai zaidi.

Mbunge 3: Madaktari na manesi wanadai rushwa kwa kuwa mishahara yao ni kidunchu! Waongezewe mshahara angalau uwe nusu ya mshahara wangu!

Mbunge 4: Walimu ndio baba na mama zetu kiakili. Tusipowaangalia nani atawaangalia?

Mbunge 5: Sera ya vijana basi iboreshwe iwe hivi au vile vijana wapate ajira jamani eee! Na kina mama wawe na Baraza la Kinamama eee? Na Wazee wawe na Baraza la Wazee heee? Na watoto wawe na Jumuiya ya Watoto eeehe!
Watu wote, yaani, makundi yote wawe na mabaraza yao eeee! Maana ndio demokrasia eehhe! Sasa kila chama kikiwa na Baraza lake la hawa au wale kweli hatutaendaga upandege wa Burundi na Rwanda eee?

Mshauri: Hoja hizi ingelifaa kutolewa katika Bunge la Wawakilishi ambapo wabunge wake wangelikuwa wakichaguliwa kutokana na tarafu au kazi zao. Kungekuwa na walimu, madaktari, wanajeshi, polisi, maprofesa, wahandisi, wenye mabasi ya mikoani, wenye ndege, wenye meli na mashua, wakulima, wenye daladala, vibarua na wanaojiajiri.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

HOJA 3

Mbunge 1: Mkongo wa taifa lazima uwepo ili kuhakikisha maendeleo yetu hayakwamishwi na mitapanyo ya njia za kutoa na kupokea mawasiliano.

Mbunge 2: Mapato yanayotokana na Migodi ya madini ichangie maendeleo ya pale ilipo na ya taifa zima kwa ujumla.

Mbunge 3: Tuna uwezo wa kuwa na shule bora za msingi na sekondari hasa kwenye mikoa ya mipakani pamoja na vyuo vya taaluma mbalimbali na taasisi hizo zikavutia takriban wanafunzi 200,000 kwa mwaka kutoka nje.
Ruksa kuajiri walimu toka nje ili waongeze ubora wa elimu yetu na walimu wetu wakasome tena nje ili wapande na ikiwezekana wapate kazi nchi za nje watutumie fedha za kuwalipa hawa wa kigeni hapa nchini.
Mkitaka kufanya jambo eti sawa na nchi zingine za Kiafrika zinavyofanya basi hamna ushindani na mtaishia papo hapo wanapoishia wao kama sio chini zaidi!

Mbunge 4: Ndugu Waziri wa Afya kama hospitali zako zikiendeshwa vyema nina hakika zaidi ya kupokea Wakomoro na Washelishlei hata na sisi tutaweza kutibiwa papa hapa nchini.
La muhimu ni kuhakikisha tunajipinda tutengeneze mashine zetu wenyewe na kuajiri madaktari wanaolipwa vyema toka ndani na nchi ya nje. Hili halina tofauti na kuwekeza maana mawaziri na wabunge toka nchi nyingine za Kiafrika watakaokuja kutibiwa hapa watalipa kiasi cha kutosha kurudisha gharama zote za uwekezaji. Tufungueni macho jamani haya ndio majibu sahihi kwa utandawazi.

Mshauri: Wallahi, hizi ni hoja
za kitaifa kwa hiyo zinafaa kuwepo kwenye bunge la Taifa na sio mabunge ya mikoa au yale ya uwakilishi.


Wenye akili watanielewa, wababaishaji katu hawatakaa wanielewe! Wana-jamii nanyi toeni HOJA ZENU. NAOMBA KUTOA HOJA!
 
Hadi hii leo sijaona kinachojadiliwa cha maana hapo bungeni zaidi ya kulipana mishahara minono na wengine wakidai waongezewe posho.

Mabunge ya nchi nyengine ni sehemu ya kiti moto na waziri au raisi anaweza kupoteza hadhi yake bila ya kutegemea.Kwani Bunge ni kama moyo wa Nchi au Taifa ,hivyo kila kinachojadiliwa hapo lazima kiwe ni tiba kwa Taifa na si kulindana.
 
BUNGE, MASHANGINGI NA ZIGO KWA WALALHOI!


HIli linahitaji sayansi ya utafiti kidogo.

Kuna maswali kadhaa ya kujibiwa hapa. Kwa mfano, mashangingi leo yanagharimu kiasi gani hadi linakuwa barabarani.


KWA jinsi serikali yetu ilivyo nina hakika wanaweza wakawa hawaweki factor ya kwamba gari ni sawa na gari+ petroli/dizeli kila siku= ndio gari kamili!

Piga hesabu za unywaji mafuta na fleet nzima ya serikali [ ni magari mangapi?]

Halafu njoo tafuta productivity ya mtumiaji gari na kama gari kweli linatumika kwa kile kilichokusudiwa.

Usisahau magari ya ziada yanayowapeleka sokoni nyumba kubwa na ndogo. Kisha magari ya kuwapeleka princes na princesses [sio kina Kayumba] shule!

Hayo mabilioni utakayoyapata ndio mafuta Watanzania wanayokaangwa nayo !

Bei ilikuwa 650/- leo lita hiyo hiyo ni 2,000/-. Piga hesabu vizuri hapa maana unaweza ukakuta mabosi uchwara serikalini sasa hivi wanatumia laki 2 hadi 4 kwa wiki kwa mafuta. Hii na kama kitu laki nane hadi milioni 1.6 kwa mwezi. Mshahara wako?

Gari limenunuliwa shilingi milioni 200? Kama tungelikuwa tunapendwa kila shangingi linazaa nyumba nne nzuri tu kwa walalahoi watakaolipa kwa kuuza mboga mboga au mamantilie kwa kutulisha ubwabwa kwa dhiki na taabu!

Wangelikuwa na akili hawa sasa hivi wangeliita TATA wawape KIBAHA nzima bure ili watengeneze magari ya bei rahisi kama TATA NANO na hayo hayo ndio yawe na vifoo wili vidogo ili vitumiwe na wakubwa wetu. Kinachobaki kinauzwa nje na kuingizia TATA faida kubwa na serikali kodi ya haja lakini pia magari ya kutumia bila kufanywa dagaa kikaangoni na Wajapani!

Mtaacha kuwa samaki kweli nyie? Heee, hebu jibuni kama mnalo jibu!

ASANTE BUBU-ATAKA-KUSEMA

Magari ni 40,000

Kwa bei ya milioni 200 kila gari ni kwamba Watanzania wananyiwa na Wajapani trilioni 8 kumaintain fleet hiyo!

Kama kila gari linakunywa kwa wiki lita 100 za mafuta hii ni sawa na shilingi laki mbili. Fleet nzima ya serikali kwa hiyo itakuwa inakunywa bilioni 8 za kitanzania kila wiki au bilioni 32 kwa mwezi. Je, utashangaa serikali ikikosa fedha za kulipa watendaji wake mishahara?

ILI kupunguza pia matumizi makubwa katika usafiri na uchukuzi na kuhakikisha kuwa kila kanda au mkoa unanufaika na mapato yanayotokana na kuwepo kwa serikali kuu mahala fulani ni muhimu kuwa na decentralization ya wizara kwa kuzigawa wizara katika kanda au mikoa ambayo kwamba huduma zake zinahitajika zaidi au jambo hilo linaweza kuwa chachu ya maendeleo ya haraka zaidi ya kanda au sekta na taifa kwa ujumla!

Wazo la serikali kununua magari kila baada ya miaka 7 ni la kiwizi kama sio la kijinga kwa sababu gari likishakaa zaidi ya miaka 3 gharama za spea zinakuwa kubwa kupita kiasi na haimeki sense kuendelea kuwa nalo labda kama wewe mwenyewe una duka la spea!
 
TUSIOGOPE UWAKILISHI?


HIVI unajua uwakilishi wa kisiasa, kidini na kijamii umedhoofika sana Tanzania katika miaka ya hivi karibuni?
Hii sio tu kutokana na kuongezeka kwa tofauti na matakwa ya watu bali pia kutokana na ukweli kuwa nchi imekuwa na mambo mengine yaliyokuwa yakizungumzwa ngazi za juu yanapaswa kushushwa chini na kuzungumzwa katika ngazi za chini zaidi-ambako maslahi na athari kwa jamii zinaonekana haraka zaidi.

KWA MAONI yangu upo umuhimu sasa wa kuwa na Bunge au mabunge zaidi ya hili moja tulilo nalo.

KWANZA, tunahitaji bunge la mkoa ambalo pamoja na wabunge wa kitaifa patakuwa pia na wawakilishi kulingana na sekta zilizopo na matakwa ya wakazi wa mkoa husika.

Bunge hili litamaliza mijadala yote inayohusu mkoa hapo hapo mkoani. Kitachobakia ni kile tu kweli chenye sura ya kitaifa na sio vinginevyo.

PILI, tunahitaji bunge la sasa liwe la kitaifa zaidi badala ya kuzungumzia maendeleo ya ndani lianze kuzungumzia pia na maendeleo ya nje.

Kwa mfano, Tanzania ikienda kumsaidia Kabila hatutaweza kunufaika kama wezi wa Mugabe wanavyofanya sasa hivi.

Baada ya Daraja la Msumbiji kuwa tayari je, tufanye nini kuongeza udugu na biashara kati ya nchi dada hizi?

Tuzisaidie vipi nchi za Kiafrika zenye matatizo. Mathalni, je, tuitawale Burudni kwanza kwa miaka 5 wakipata amani tuwaachie nchi yao.

Je, Bandari ikijengwa Mtwara na sio Bagamoyo tutapata hasara au faida gani?

Je, majeshi ya Tanzania yanaweza kurudi madarasani baadhi yao wakafundishwa uhandisi na ujenzi wa barabara tena kwa lugha ya kiswahili? Au wengine wakaanza kutengeneza pampu za maji? Au matrekta ya Kitanzania au mali ghafi zote zinazohitajika katika ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu?

Je, jamaa wa JKT badala ya kuwakongori ndugu zangu wa Maramba wanaweza kwenda kutoa huduma za usafi au ustawi wa jamii au kuwarekebisha wavuta bangi? Na mambo kama hayo!

Yaani, nanihii, ninachosema hapa tuanze kufikiria masilahi yetu kwanza kama vile MAREKANI wanavyofanya na wala tusione haya kabisa katika kutanguliza NI NINI TUTAKACHOKIPATA kama tukiwasaidia watu hawa hivi au vile. Somo la Afrika Kusini haliko mbali sana tumeona tulivyowasadia Wasauzi kisha wakaja ua ndugu zetu, tumeona tulivyowasaidia Wazim nao hawakuwa makini wala wazima na sasa wameishusha nchi yao kwenye jehanamu la dunia. Laiti kama tungelifaidika na kile tulichowafanyia tusingelikuwa na mengi ya kujijutia.

Ninadhani hata wale ndugu zangu Wasomali wenye asili ya Handeni wataniunga mkono kwamba twendeni Somalia pia tukaisaidie kuwa na amani kisha tuwafunze Kiswahili na kiswahili kisikike toka Maputo hadi Brava na Kismayu!
 
NAOMBA Bunge letu tukufu liwe linaheshimu sala lya Ijumaa. Je, wabunge ambao ni Waislamu mnaburuzwa au ndio walewale ambao wanauonea aibu Uislammu wao. Hivi nyie mnamuogopa Mungu kweli au ni wanafiki!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom