Bunge la sasa uenda likachochea kasi ya mageuzi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge la sasa uenda likachochea kasi ya mageuzi.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Feb 27, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Historia inayo mifano mingi inayothihirisha kwamba mtawala nayehuma na kupuliza hudumaza jitihada za kujikomboa;hivyo ndivyo ilivyokuwa wakati wa bunge lililopita. Bunge hilo chini ya uongozi wa Sitta, lilijijengea sifa miongoni mwa watanzania wa kawaida, ya kuwa lilikuwa limepania kweli kweli kupambana na maovu serikalini. Imani hiyo ilisababisha watanzania wengi kuwa na subira. Hivi sasa kinyume na bunge lililopita watu wengi wanaliona bunge la sasa chini ya Anna Makinda kuwa limepania kuikingia kifua serikali kutokana na lawama mbali mbali zanazo ikabili. Hisia hizo zinachochea watu wengi kujihunga na harakati za kudai mageuzi.
   
Loading...