Bunge la sasa lina hoja dhaifu, kama alivyosema Prof. Assad

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Ndugai asiposikia tena hili ndo basi tena. Sauti ya leo ni sauti ya mwisho na asipoelewa atakuwa na tatizo la akili. Wananchi wamesema kwa muda mrefu, wataalamu wamesema, viongozi wa dini wamesema. Lakini ni kama ameweka pamba masikioni. Sasa amezungumza raia namba moja. Ndugai achague kusuka au kunyoa.

Bunge la sasa limepoteza mvuto. Ukiondoa wabunge wachache ambao bado wanaheshimika, wengi wanajadili majungu na kufanya personal attacks. Wapo busy kumjadili Mbowe, kujadili nguvu za kiume, kujadili ‘legacy ya mwendazake’ na kusahau hili ni bunge la bajeti, wanapaswa kujadili bajeti ya nchi kwa maendeleo ya taifa letu.

Lakini mbunge anatumia dadika 20 kuzungumzia nguvu za kiume na Ndugai badala ya kumrudisha kwenye mstari anatilia vionjo kunogesha soga. Kama amekutana na wala chips wasio na nguvu, si atafute tunaokula ugali, aone kama hatatoa ushuhuda akiwa ICU.

Bunge la 2015/20 Ndugai alikuwa anawaita kwenye kikao cha nidhamu wabunge wanaotweet mambo asiyoyapenda. Yani Lema akitweet jambo, kesho yake anaitwa kujieleza. Unajiuliza huyu ni Spika wa bunge au Spika wa Twitter?

Wiki hii bunge liliacha kujadili bajeti, likaanza kujadili 'legacy’ ya mwendazake. Wakanyukana wao wa wao. Hadi Nape alipofunga mjadala, kwa kusema 'legacy' haitetewi bali inajitetea yenyewe. Kama aliacha alama nzuri kwa watu watamkumbuka kwa mazuri, na kama aliacha alama ya maumivu, watamkumbuka kwa maumivu hayo. Lakini watu wote wasilazimishwe kumkumbuka kwa mazuri.

Ndugai akataka watu wakumbushwe madaraja na barabara alizojenga mwendazake. Anadhani hiyo ndio legacy. Anasahau Mwalimu Nyerere ameacha legacy kubwa lakini hakuna anayemkumbuka Nyerere kwa madaraja wala barabara, japo alijenga nyingi. Hata Mandela hakumbukwi kwa kununua ndege au kujenga airports. Ndugai hajui maana legacy .

Bunge la Ndugai limeacha kujadili bajeti linamjadili Mbowe, Kigogo na Nguvu za kiume. What a shame?

Bunge la Samwel Sitta halikuwa hivi, wala bunge la Makinda halikuwa hivi. Yalikua ni mabunge 'principled' yaliyoacha legacy kubwa sana, na hadi leo yanakumbukwa kwa namna yalivyochochea mijadala yenye maslahi mapana kwa taifa.

Prof.Assad aliwahi kutoa ripoti inayoonesha ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma. Ikapelekwa bungeni kujadiliwa, lakini hakuna hatua iliyochukuliwa. Assad alipoulizwa, akasema mwenye mamlaka ya kuchukua hatua ni bunge. Kama bunge limekaa kimya basi ni dhaifu.

Ni kama kiranja akimripoti mwanafunzi anayevuta bangi. Anayepaswa kumfukuza shule ni Headmaster. Ikitokea Headmster amepewa ushahidi wote na bado akashindwa kumfukuza shule basi huyo Headmaster ni dhaifu. Hiki ndicho alichosema Prof.Assad. Yeye ameibua 'madudu' na ushahidi upo, lakini kama bunge limeshindwa kuchukua hatua basi bunge ni DHAIFU.

Ndugai kusikia hivyo 'mapepo yakapanda’ akamuita Assad akajieleze kwanini ameliita bunge dhaifu. Prof.Assad (a man of proven intergrity) akatinga bungeni na akarudia kilekile alichosema awali. Akawaangalia usoni bila tashwishwi, kisha akasema "mabunge yote yaliyopita yalikua yanafanyia kazi ripoti za CAG na kuchukua hatua. Kama nyie mmeshindwa kuchukua hatua basi ni DHAIFU"

Wakamwambia omba radhi, akasema siwezi kuomba radhi kwa sababu udhaifu sio tusi, udhaifu ni SIFA kama ilivyo urefu na ufupi. Huwezi kumuita mtu mrefu halafu akakuambia omba radhi. So udhaifu ni sifa na bunge hili linayo sifa hiyo. Akamaliza akaondoka zake.

Kwa miaka 6 bunge la Ndugai limeshindwa kuibana serikali kama mabunge yaliyopita. Ndege zimenunuliwa bila bunge kuapprove. Ingekuwa bunge la Samwel Sitta pangechimbika. Hakuna anayekataa kununua ndege lakini sheria inasema bunge lazima lielezwe mpango, liujadili na litoe approval.

Lakini bunge la Ndugai hawakuletewa mpango wa kufufua ATCL, hawakujadili wala hawakupitisha bajeti ya kununua ndege. Walishtukia tu ndege hizi hapa. Na wakafyata mkia. Halafu bunge likiitwa dhaifu Ndugai anafura .

Leo Mama amerudia alichosema Prof.Assad kwamba bunge la Ndugai ni DHAIFU. Tofauti ni kwamba mama amechoma sindano halafu akapuliza. Hii ndio sifa ya mama. Lakini ukweli unabaki palepale kwamba bunge la Ndugai ni DHAIFU SANA.

Sasa Ndugai achague kusuka au kunyoa. Aamue kuendeleza mijadala ya nguvu za kiume, au afanyie kazi ushauri wa Raia namba moja wa kujadili mambo yenye tija kwa taifa. Kupanga ni kuchagua.!
malisa_gj_20210419_105847_0.jpg
 
Na hii yote ni kwa sababu bunge hili liliundwa litoke upande mmoja kwa mkakati maalum.Haikuwa bahati mbaya. Jiwe alitaka liwe dhaifu ili asihojiwe kwa plaz zake fulani fulani
 
Back
Top Bottom