Bunge la pitisha ufisadi na ujangili kwa mgongo wa haki za binadamu

gwacha

Member
Mar 5, 2011
37
8
Hivi ni kwa nini watu wengi kiasi hiki,wenye elimu za kutosha,wenye hekima na busara,kuchezewa mchezo mchafu ulio andaliwa(planed) kiufundi na watu wachache,wasio ipendea mema nchi hii,WAMETUINGIZA KWENYE KILENGEO.Tanzania Tanzania..........!seaching.............
 
Attachments

  • IMG-20131209-WA0001.jpg
    IMG-20131209-WA0001.jpg
    20.7 KB · Views: 266
Hivi ni kwa nini watu wengi kiasi hiki,wenye elimu za kutosha,wenye hekima na busara,kuchezewa mchezo mchafu ulio andaliwa(planed) kiufundi na watu wachache,wasio ipendea mema nchi hii,WAMETUINGIZA KWENYE KILENGEO.Tanzania Tanzania..........!seaching.............

Hamna operations zisizo na kasoro . Na Labda watendaji walizidisha makali ili kumhujumu Kagasheki .
Mimi kama Kikwete namrudisha huko huko Maliasili, labda kama nae kahongwa !!
 
acheni siasa kwenye mambo ya msingi.....kumsukumia chupa ya soda....mwanamke sehemu za siri...hapo unazuiaje ujangili...?
 
Hamna operations zisizo na kasoro . Na Labda watendaji walizidisha makali ili kumhujumu Kagasheki .
Mimi kama Kikwete namrudisha huko huko Maliasili, labda kama nae kahongwa !!

wasiwasi wangu wabunge ni sehemu ya watuhumiwa wa ujangili, wizi wa posho, wake za watu, uuzaji wa pembe za ndovu, ulevi, matumizi mabaya ya ofisi zao ikiwepo swala la rushwa hivyo kwa mada iliyopo mezani kwao kuwa fair na independent (objective) ni ngumu hivyo utaona tu jaziba na kuwa upande mmoja
 
acheni siasa kwenye mambo ya msingi.....kumsukumia chupa ya soda....mwanamke sehemu za siri...hapo unazuiaje ujangili...?
sidhani kama walifanya hivyo, naingiwa na mashaka, huenda kilichokuwa presented sio ukweli
 
wasiwasi wangu wabunge ni sehemu ya watuhumiwa wa ujangili, wizi wa posho, wake za watu, uuzaji wa pembe za ndovu, ulevi, matumizi mabaya ya ofisi zao ikiwepo swala la rushwa hivyo kwa mada iliyopo mezani kwao kuwa fair na independent (objective) ni ngumu hivyo utaona tu jaziba na kuwa upande mmoja
Aisee majangili kutumia wenzao bungeni wamefanikiwa kumgeuzia kibao kagasheki. Walimtisha na alivyoonyesha ujasiri wametekeleza. Issue ya majangili bye bye. Hii ndio serikali ya nambari wani eeeeh!
 
kilichokua presented ni kweli 100%.

swali?hayo yalifanywa kwa msukumo wa nani.mawaziri wenyewe .majangiri au Askari wenyewe

Unaelewa maana ya collective responsibility?tuanzie hapo kwanza
 
Iwe iwavyo,
Maovu waliyo fanyiwa wananchi ni makubwa kuliko hiyo nia ya hiyo operation. Hivyo, hao mawaziri wang'ooke. Atakayekuja naye aendeleze huo mradi. Wizara ya Mali Asili ni wizara mbovu kuliko unavyo ielewa. Haihitaji mtu yeyote mwenye tamaa.
Mh. Rais, mteue Felix Kilahama, awe mbunge umpe hiyo wizara
 
Hili ni tatizo la Watanzania kama wenye nchi kutojua nini tunachokisimamia kama maslahi ya TAIFA. Wenzetu wako radhi vita dhidi ya kulinda maslahi ya taifa lao zipiganwe nje ya nchi zao wao wabaki salama sisi hatujiwelewi. Kwa masilahi yao wako tayari kuua raia wasio hatia maelfu ili kumpata gaidi mmoja anaehatarisha usalama wao nahaiwapi shida sie tunavimba mishipa kupoteza mtu mmoja kuokoa rasrimali za Taifa. Operation ni vita na vita haina macho mradi malengo yamefikiwa kumtokomeza adui. Siasana uanagharakati hautatufanya tushinde vita. Lazima utiifu wa sheria uwe ndio msingi wa maisha ya wa Tz. Wafugaji wanaopoganiwa watii sheria na sote kwa ujumla. Kwa wenzetu wachache wanaopoteza maisha ni wahanga wa vita maadamu Maslahi ya Taifa yamezingatiwa sisi majingu na kuzuia utekelezaji wa ulinzi na usalama wa maslahi yetu. MAJANGIRI WATASHINDA SIKU ZOTE.
 
Ngoja tu nirudie post yangu niliyopost kule kwenye ile breaking news maana naona hapa ndio mahali pake.Hivi kuna nini na mienendo hii ya askari wetu kule Mtwara,Arusha,operesheni ujangili,kimbunga etc?Matukio haya ya ubakaji na uchafu yanaashiria nini?kwani Kagasheki ndiye aliwatuma askari hawa kutesa raia au wanamhujumu makusudi kuacha traces ambazo leo zimetumika kumharibia kazi?The same applies to Chiza na Malima nao wanatafutwa wakomolewe kwa kuzibia watu mirija kwenye wizara ya kilimo.Najiuliza sana,wabunge wetu hapa wanatutetea sisi kwa upendo wa dhati,au wanatumikia mafisadi kwa kutumia malalamiko yetu yatokanayo na tatizo lililotengenezwa kwetu makusudi ili kuwaharibia kazi mawaziri ambao wametekeleza wajibu wao kwa maslahi ya umma na kuwavuruga mafisadi?kwa nini makada wa ngazi za juu wa CCM wamekuwa mstari wa mbele kuwapiga vita mawaziri ambao kwa mtu mwenye jicho la tatu atagundua kuwa ndio mawaziri wanaotekeleza wajibu wao kwa usahihi?narudia tena,hii skendo ni nzito sana.Nchimbi na wenzie ni sehemu ndogo ya tatizo.Naomba vyombo vya usalama vya nchi vichunguzwe na hapa natilia mkazo usalama wa taifa ngazi ya mkoa na wilaya(RC na DC inclusive),majeshi yote jw,polisi na magereza,watendaji wa wizara ya ulinzi na mambo ya ndani na taasisi zote za usalama.Nimeonelea nishauri hivi kwa uzoefu wangu wa ripoti za mambo ya ujangili hasa kwenye research za nchi nyingine na naona trend ya mambo hapa nchini inaenda vile vile haswa namna askari wetu walivyoharibu hii operation kwa makusudi kabisa.Pili,ni lazima CCM nayo ichunguzwe kwani shutuma nyingi za ufisadi zinaelekezwa kwa viongozi wake wa kichama na wameonekana kuanzisha vita ya maneno na mawaziri na watendaji wa serikali walioonekana mwiba kwa mafisadi.Kagasheki,Chiza,Malima na Mathayo ni mfano mzuri.Ukizingatia viongozi wengi wa chama hiki kuwa na background za taasisi za usalama kama majeshi,na mwenendo wa mambo niuonavyo,wanaweza kuwa na influence kubwa ndani ya taasisi hizi.nasema lazima CCM ichunguzwe tena si kwa hili la ujangili tu,bali na mengineyo kama EPA etc.Nina wasiwasi suala la kutimua watendaji wa serikali kama mawaziri sasa si pure political responsibility bali ni political responsibility based on political wars!
 
acheni siasa kwenye mambo ya msingi.....kumsukumia chupa ya soda....mwanamke sehemu za siri...hapo unazuiaje ujangili...?

kwa nini hawazikamati meli za kinana zenye pembe za ndovu mpaka wanaanza kuwatesa wanyonge?
 
acheni siasa kwenye mambo ya msingi.....kumsukumia chupa ya soda....mwanamke sehemu za siri...hapo unazuiaje ujangili...?

Nani alishuhudia? mnathibitishaje stori za kusimuliwa? Chupa chupa kwaushahidi gani? Lemaamesingiziwa kwa picha za photoshop tumethibitisha lugha kama hizi tunathibitishaje? Mnainjikiwa na wafugaji nanyi mwakubali, wafugaji ambao hawaoni hasara kuhonga ng'ombe nne mradi malengo yao yafanikiwe. Walijuaje leo itasomwa taarifa (ambayo ilikuwa siri) ya bunge wakajazana? Wakulima bungeni na nguo nyeusi? Wakulimawanaonyanyaswa na wafugaji mbona hawakutonywa? MCHEZO MCHAFU unachezwa Watanzania
naingia MKENGE.
 
Back
Top Bottom