Bunge la Ndugai linaziweka hatarini ndoa nyingi!

Tee Bag

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
7,200
5,553
BUNGE LA NDUGAI LINAZIWEKA HATARINI NDOA NYINGI!

KWANZA salaam Mheshimiwa Ndugai. Naomba unisikilize. Hupendi kusemwa ni kiongozi dhaifu na hutaki kusikia Bunge unaloliongoza likiitwa hivyo. Ngoja niseme hivi; wewe Ndugai ni kiongozi shupavu. Bunge lako ni imara. Si ndiyo unapenda kusikia?

Hata hivyo, ndani ya moyo wangu na kama ilivyo mapokeo ya tabaka kubwa la Watanzania wenye kutambua hadhi na wajibu wa Bunge kwa nchi, nasema kuwa Bunge la sasa, linaloongozwa nawe, ni dhaifu. Halivutii!

Na nikisema Bunge ni dhaifu, simaanishi majengo. Maana majengo hayo ndiyo yaliyotumiwa na Pius Msekwa, Samuel Sitta na Anne Makinda. Pamoja na changamoto zilizotokea wakati huo, Bunge halikuitwa dhaifu chini ya Msekwa, Sitta na Makinda.

Kumbe sasa shida si majengo bali watu. Ooh, tatizo ni uongozi. Watu wamekuwa wakitumia tafsida kusema Bunge ni dhaifu. Hawanyooshi ukweli huu, kwamba uongozi wa wako ni dhaifu na kwa dhaifu huo, Bunge limekuwa dhaifu.

Masikitiko; si kwamba hujui kuwa Bunge la sasa ni dhaifu. Kiuzoefu na kitaaluma, unaelewa Bunge chini yako halikidhi viwango. Umekuwa mwenyekiti wa vikao vya Bunge mwaka 2005-2010. Umekuwa Naibu Spika 2010-2015. Na sasa ni Spika. Nini hukujui?

Ulikuwepo bungeni nyakati za kuibuliwa wizi wa fedha Benki Kuu kwenye akaunti ya madeni ya nje (EPA). Ulikuwepo Serikali iliposhughulikiwa katika mkataba wa kifisadi wa ufuaji wa umeme wa dharura, kati ya Tanesco na Richmond.

Ulishiriki kufanikisha hoja kuhusu kashfa ya wizi Benki Kuu kwenye akauti ya Tegeta Escrow na Serikali ilivuliwa nguo. Ulikuwepo ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), iliposababisha mawaziri nane wang'oke mwaka 2012. Ulikuwepo Serikali iliposhughulikiwa na Bunge katika kashfa ya Tokomeza Ujangili.

Ndugai uliona kazi ilivyofanyika. Haikuwa rahisi lakini Bunge liliamua kujiheshimu na kusimamia maudhui ya uwepo wake ambayo ni kuwawakilisha wananchi na kuisimamia Serikali. Kama Bunge la sasa linaamua kutengeneza ushosti na Serikali. CAG ana kosa gani kusema ni dhaifu?

Tundu Lissu kapigwa risasi mchana kweupe, polisi hawajafanya chochote. Bunge limeshindwa kuunda Kamati kuchunguza. Watanzania wamepotea, wanatekwa. Mwandishi Azory Gwanda, kada wa Chadema, Ben Saanane na wengine. Maiti nyingi zilikutwa fukwe za Bahari ya Hindi na Mto Ruvu. Bunge limekosa kauli. Mauaji Kibiti, Mkuranga na Rufiji. Bunge kimya.

Bunge linaoneshwa na CAG kuwa fedha za umma zinatumika vibaya. Halifanyi kitu. Linaitwa dhaifu. Linaamua kugombana na CAG badala ya kujisahihisha. Ndugai afahamu kuwa watu wengi wanaumia. Wanapoteza nguvu. Watu wengi mioyo inapondeka.

Wapo wanaoshindwa kuhudumia ndoa zao kwa sababu wanalala hawana furaha kwa jinsi Bunge linavyoendeshwa. Mwenendo wa Bunge kwa sasa, unafanya ndoa nyingi ziwe hatarini. Watu wenye uchungu na nchi hii wengi wao hawana furaha. Hamu ya ndoa wanapata wapi?

NINA MAONGEZI MAREFU

Ngudai, nini hukijui kuhusu falsafa ya Trias Politica? Mwanafalsafa wa Ufaransa, Charles de Montesquieu akaita ni roho ya sheria (spirit of the laws). Kwamba katika kila dola, lazima kuwepo mgawanyo wa mihimili mitatu; Serikali, Bunge na Mahakama ambayo misuli yake haiingiliani.

Serikali inashughulikia utendaji na uratibu wa maisha ya watu; usalama, mazingira na ustawi wao. Bunge linawakilisha sauti za watu, linaisimamia Serikali na linatunga sheria zenye kuzingatia masilahi ya watu. Mahakama inatafsiri sheria, inachambua na kutoa haki.

Bunge kwa sababu ndicho chombo cha kuwakilisha wananchi, kuisimamia Serikali na kutunga sheria zenye kutafsiriwa na Mahakama, huonekana ni kitovu cha mihimili, yaani mothership connection au the supreme organ.

Mapinduzi ya Ufaransa mwaka 1791, yalisababishwa na uamuzi wa utawala wa Mfalme Louis XVI kutoheshimu mgawanyo wa nguvu za mihimili ya dola. Katiba ya Marekani mwaka 1789 iliandikwa kuondoa utata wa mihimili. Katiba ya Tanzania mwaka 1977, inaheshimu mihimili.

Ukishasema Bunge ndiyo kitovu cha mihimili, maana yake ni kitovu cha matumaini ya watu kwenye nchi. Hivyo ni chombo kinachopaswa kuundwa na watu makini, lakini muhimu zaidi, kinatakiwa kiongozwe na watu ambao umakini wao hautiliwi shaka.

Umakini wa uongozi wa Bunge haupimwi kwa uhodari wa kuagiza watu wanaolikosoa Bunge waende kwenye Kamati ya Maadili ili wahojiwe na kuadhibiwa. Umakini wa viongozi wa Bunge mzani wake si Spika kuongea siri za wabunge kuwa wanadaiwa fedha na kwamba wana msongo wa mawazo.

Umakini wa Bunge ni jinsi Bunge linavyosimamia masilahi ya nchi bila woga wala kusita. Bunge makini huifanya Serikali iogope. Bunge likiwa dhaifu, Serikali hulichukulia poa. Je, Serikali ya Magufuli inaliogopa Bunge la Ndugai?

Kama fedha Sh1.5 trilioni hazijapata majibu mpaka leo. Hata CAG alipofanya ukaguzi maalum wa mara ya pili, hakuridhika. Akasema zaidi ya Sh970 bilioni zimeondolewa hazina bila utaratibu wa kisheria na kikatiba. Sasa utata umefikia Sh2.4 trilioni katika mwaka mmoja wa fedha. Bunge linashindwa kuchukua hatua.

CAG aliyekagua anasema Bunge ni dhaifu, eti Bunge linaona ujanja ni kususa kufanya naye kazi. Bunge halijaambiwa limekula pesa, bali linaonesha udhaifu kuisimamia Serikali ya Rais John Magufuli ili iwe na nidhamu na fedha za umma.

Majibu ya Ndugai ni kususa kufanya kazi na CAG. Kisha, Ndugai anampokea mchekeshaji mlevi Pierre Liquid bungeni, anasema: "Magufuli yupo juu." Hii ni mpya sana. Spika anaona Bunge ni jukwaa la kumtukuza Rais. Hatari mura!

NDUGAI ANAFUNGISHA

Bunge ndiyo timu ya wananchi kuhakikisha masilahi ya watu yanalindwa. Bunge hutakiwa kukabana na Timu Serikali ili kinachoamuliwa na kutendwa na Serikali, kinakuwa ni kwa masilahi ya nchi na watu wake.

Spika wa Bunge ndiyo nahodha wa timu ya wananchi na kazi yake ni kuwaongoza wachezaji wenzake (wabunge) ili kuibana Timu Serikali. Sasa nahodha anapoamua kuwa swahiba wa kiongozi wa Timu Serikali, hapo ni dhahiri anaifungisha timu ya wananchi. Ndugai anawafungisha Watanzania.

Septemba 7, 2017, Rais Magufuli alipopokea ripoti mbili za kamati teule za Bunge, zilizochunguza shughuli za uchimbaji na biashara ya tanzanite na almasi, alisema kuwa Ndugai alimpigia simu alipotaka kuteua wajumbe wa kamati.

Rais Magufuli alisema kuwa Ndugai alimpigia simu kumweleza jinsi alivyo na wakati mgumu kuteua wajumbe wa kamati hizo. Hapa Ndugai alifungisha. Kiongozi wa Bunge ni mwiko kujadili na Kiongozi wa Serikali, muundo wa wajumbe wa kamati za kuikagua Serikali.

Ndugai anafahamu kuwa taasisi za Serikali na Bunge hazipaswi kutengeneza timu ya pamoja. Bunge na Serikali kuwa timu moja ni usaliti wa desturi za mifumo ya mihimili ya dola, dhambi kubwa iliyopo hapo ni kuisaliti Katiba. Ukishaisaliti Katiba maana yake umewasaliti wananchi.

Hata kama Ndugai alikuwa na nia njema kiasi gani, kitendo tu cha kubainika alimpigia simu Rais Magufuli ili kupata mawazo yake juu ya muundo wa kamati ni kushushwa heshima na hadhi ya Bunge. Ni vigumu kwa wananchi kuamini kama Bunge linatimiza wajibu wake sawasawa dhidi ya Serikali.

Ni kweli Rais anatamkwa kuwa sehemu ya Bunge, lakini Katiba imemtenganisha kabisa na shughuli za kila siku za Bunge. Rais ni sehemu ya Bunge kwa sababu kutokana na mamlaka yake ya Ukuu wa Nchi ndiye mwenye kuliitisha, kulizindua na kulivunja baada ya umri wake kutimia au dharura yoyote inapojitokeza.

Hapa pia ifahamike kuwa Rais nafasi yake ya kuliitisha, kulizindua, kulihutubia na hata kulivunja Bunge, inatokana na kofia yake ya Ukuu wa Nchi na Siyo Ukuu wa Serikali. Na kwa vile ni vigumu kutenganisha masilahi ya Rais ndani ya Serikali, ndiyo maana Katiba imemuweka mbali na shughuli za kila siku bungeni.

Mtindo mpya wa Ndugai kufanya mashauriano na Rais Magufuli, unafanya Serikali ikose hofu dhidi ya Bunge. Serikali inapokuwa haina hofu na Bunge, tafsiri yake ni kwamba Bunge ni kibogoyo. Bunge kibogoyo ni Bunge dhaifu.

Ndugai anafahamu kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni la uga mmoja tu wa mijadala (unicameral), hivyo hoja na ripoti zote za kibunge, husomwa na kuwasilishwa kwa wabunge wote, kisha wabunge kujadili na kuweka maazimio inapobidi.

Ripoti za kamati teule za Bunge zilizochunguza alamsi na tanzanite hazikusomwa bungeni, hivyo wabunge wote hawakupata fursa ya kujadili. Badala yake ripoti zikapelekwa kukabidhiwa kwa Rais Magufuli.

Ripoti za Bunge ambazo zilisababisha Rais awaondoe kazini waziri na naibu waziri hazijakudiliwa na wabunge wenyewe. Hapa bila kupepesa maneno ni kwamba Ndugai alifungisha. Yeye akiwa kiongozi wa Bunge amethubutu kuuondolea meno mhimili anaouongoza.

Niliwahi kuandika makala kumsifu Ndugai, nikamwita Solon kwa namna alivyoliunganisha Bunge la 11 katika Mkutano wa Nne na Tano, baada ya Mkutano wa Tatu kuwa na mgawanyiko mkubwa kutokana na kususiwa na wapinzani.

Solon ni mtawala wa Ugiriki ya kale ambaye ndiye mwasisi wa mfumo wa utawala kuendeshwa kwa mawazo ya wananchi walio wengi alipoanzisha Bunge la Waathens. Mfumo ambao ndiyo umeleta demokrasia ya uwakilishi kupitia Bunge, kwamba wawakilishi wa wananchi wanakuwa wasimamizi wa Serikali.

Kwa mambo ambayo Ndugai hufanya. Mara amlime vijembe Zitto Kabwe kuwa ni mbunge wa chama chenye mbunge mmoja, au Lema na madeni pamoja na namna anavyotumia nguvu dhidi ya CAG, kiukweli najikosoa kumwita Solon. Amekuwa sehemu ya Bunge kukosa makali dhidi ya Serikali.

Wananchi wanahitaji maisha bora. Wanavuja jasho, wanalipa kodi. Je, jasho lao linatumika vipi? Mapato ya rasilimali zao yanatumika vipi? Bunge ndilo linatakiwa kumhakikishia mwananchi kuwa kila kitu kipo sawa. Bunge halitimizi wajibu mpaka CAG anasema Bunge ni dhaifu. Halafu Ndugai anaitisha mapambano na CAG ambayo hayamsaidii mwananchi. Yanazidi kumuumiza.

Halima Mdee ni mbunge tangu Bunge la Tisa chini ya Sitta. Alikuwepo Bunge la 10 la Makinda. Yupo Bunge la 11 la Ndugai, anasema Bunge la sasa ni dhaifu. Badala ajitafakari kuona anajikwaa wapi, anatangaza adhabu. Ndugai anafungisha sana.

Mwaka 2012, Bunge la 10 lilisababisha mawaziri nane waondolewe kazini kutokana na ripoti ya CAG; Mustafa Mkulo (Fedha), William Ngeleja (Nishati na Madini), Dk Haji Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii), Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii), Omar Nundu (Uchukuzi) na Dk Cyril Chami (Viwanda na Biashara). Vilevile naibu mawaziri wawili, Athuman Mfutakamba (Uchukuzi) na Lucy Nkya (Afya na Ustawi wa Jamii). Bunge la sasa linagombana na CAG anayetaka Serikali iwajibishwe.

Hiyo ni mifano kuonesha kuwa Bunge la 10 lilikuwa moto. Kama utashuka Bunge la Tisa, utakuta lilikuwa na meno, kwani lilimng'oa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri wengine wawili kupitia kashfa ya Richmond, halafu Baraza la Mawaziri likavunjika.

Ukweli ni kwamba Ndugai umepwaya sana. Na namna unavyotumia nguvu kuwakabili wanaokukosoa ndivyo unavyozidi kupwaya. Unatuangisha sana Watanzania. Mbaya zaidi siku zimeisha. Mungu saidia, Bunge la 12 lisiwe nawe. Mungu akinipa uhai, nitasimulia wajukuu ubovu wa uongozi wako bungeni na jinsi ndoa zilivyoingia matatani sababu yako. Watanzania hawana furaha, hamu ya ndoa wanaipata wapi?

Ndimi Luqman MALOTO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugai anaogopa kutoalikwa Ikulu kwenye tafrija za kukabidhi report zisizoisha
 
Ukitaka kujua udhaifu wako, Tumia mtu mwingine akwambie anakuonaje? Si rahisi wewe kujijua, hata Yesu aliwauliza wafuasi wake, eti watu husema mimi ni nani? Na nyie mnasema mimi ni nani?
Kwa hiyo mh. Speaker watu wamaposema wewe/ni dhaifu, kubali na jichunguze. Umepata ushauri wa bure
 
Hakuna ulevi mbaya kama kulewa madaraka.....hivi hawa viongozi wetu wana nyama na damu kama sisi kwelii!!mbona hawaoni aibu,hawaguswi watu wanalamika kila kona ...wanabaki kusema wanatete wanyonge ......wapii hao
 
Ukitaka kujua udhaifu wako, Tumia mtu mwingine akwambie anakuonaje? Si rahisi wewe kujijua, hata Yesu aliwauliza wafuasi wake, eti watu husema mimi ni nani? Na nyie mnasema mimi ni nani?
Kwa hiyo mh. Speaker watu wamaposema wewe/ni dhaifu, kubali na jichunguze. Umepata ushauri wa bure
Ccm huwa hawakubali kuelezwa ukweli!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom