Bunge la Miongozo ya Spika, Jee Mhe, Spika ni Dhaifu, Dikteta au? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge la Miongozo ya Spika, Jee Mhe, Spika ni Dhaifu, Dikteta au?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PatriotMzalendo, Feb 9, 2011.

 1. P

  PatriotMzalendo Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tangu kikao hiki cha Bunge kilipoanza, nimegundua kuwa wabunge kadhaa wa CCM ni wajinga kupita maelezo. Kwa sababu wanajua wengi wanazidiwa upeo kwa mbali na wabunge wa CHADEMA, wanaona kwamba kuingilia hoja za wabunge wa CHADEMA za mwelekeo wa kitaifa kwa kuomba mwongozo wa spika bila hoja zozote za maana na kulazimisha tafsiri za kanuni ni mbinu yao ya kuvuruga hoja hizo na kupoteza muda wa watoa hoja hao makini wa CHADEMA.

  Kwa mfano, Mbunge wa CHADEMA aliposema Rais hana uthubutu wa kubuni mambo makubwa na kutoa mifano hai, ilikera sana mbunge mjinga wa CCM alipoomba mwongozo wa spika na kutumia kanuni inayokataza mbunge kumdhihaki Rais ambacho,kwa tafsiri, hakimkatazi mbunge kuonyesha dosari za kiutendaji za Rais bali kinakataza labda kumwita bungeni Rais Mkwere, Msanii, mtu wa kuchekacheka na kadhalika.

  Kibaya ni kwamba hakuna mwongozo wa spika wa kijinga dhidi ya mbunge wa CHADEMA uliokosolewa na naibu spika tofauti na alivyokuwa akifanya Samwel 6. Hawa wabunge wa CCM na spika wao wanapaswa waelewe kuwa hii miongozo ya spika ya kijinga dhidi ya hoja zinazogusa maisha yetu inaongeza umaarufu na upendo wa wabunge wa CHADEMA kwetu na inapoteza kabisa heshima na upendo wetu kwao! Waendelee hivyo hivyo na jibu watalipata 2015.
   
 2. Muadilifu

  Muadilifu Senior Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 150
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Yani mimi wananiudhi hao CCM, hawajui tu. Dawa yao iko jikoni.
   
 3. M

  Mtemakuni JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 257
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Waache wafikiri hizi ni enzi za mwalimu...! majority ya pipoz wanaelewa everything which goes on bungeni now if hawaamini wasubiri 2015 ndo wataoona dawa yao..!!:first:
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Safari hii tutawajua tu! nani partisan na nani non-partisan debaters
   
 5. z

  zamlock JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  mimi nasema hivi mziki wa chadema uko pale pale na sisi kama wannchi atuwezi kuwa mbali na chama chetu tumeshakuwa na upana wa kimawazo kuhusu siasa chafu ya ccm na tutawaunga mkono chadema mpaka mwisho wake mpaka kieleweke kwa sababu ndicho chama makoni tulichobaki nacho tu
   
 6. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Na Assume kuna vijana 1000,000 Tanzania nzima wenye kukerwa na CCM na viongozi wake na wasingependa kuona ikitwaa uongozi wa Tanzania tena.
  Na Assume vijana hawa 1000,000 kila mmoja ana tafuta vijana wadogo wasiopungua 14 nakuwapa 101 kwa kipindi cha miaka 5 hadi Novemba 2015.

  Kila kijana mwenye uelewa akiamua kuanza kupiga Kampeni,leo hii 2011, ya kuujenga na kuimarisha upinzani dhidhi ya Mamruki CCM,na kuanisha kwa kina na kujenga ushawishi wa kwa nini mageuzi ni lazima Tanzania; kwa nini ni lazima uongozi wa nchi uwekwe mikononi mwa wapinzani, nina Imani na nina amini kwa dhati kwamba CCM watakufa kifo cha Mende ifikapo Nov 2015 kwa sababu kutakuwa na Jeshi la vijana14,000,000( mtu Millioni kumi na nne) waliojiandaa vyema kukipiga ngwala CCM come rain come sun.

  Si lazima uwashawishi ujengwe kwa vijana wenye umri wa kupiga kura leo hii 2010 la hasha. Ushawishi mkuu ujengwe zaidi kwa vijana wenye miaka 12 hadi 18 vijana ambao watapiga kura zao kwa mara ya kwanza November 2015. "Wapige msasa vijana wako kwa kipindi cha miaka 5 waive vizuri ili November 2015 kura yako iwe na uzao wa kura zisizopungua 14."

  Ni wazo lionekanalo jepesi lakini lenye uzito mkubwa sana ndani yake.
  Ni wazo ambalo mtaji wake ni kumvuta kijana pembeni na kuongea naye seriously na baadaye kuongea na vijana wako wote kwa mtindo wa semina ya kijiweni.

  Kama vijana wana dhamira ya kuing'oa CCM mtaji mkubwa wa kuing'oa CCM ni kuwashawishi waathiriwa wakuu wa sera za CCM,VIJANA, kuyaenzi mageuzi na kuyapa nguvu kwa KURA zao.
   
 7. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Mambo ya kuomba mwongozo wa spika is issue ya kuona kuna akili nyingi sana kwa chadema. kumbuka jana Tundu Lissu baada ya kupewa summons ya mahakama kuu na kuomba bunge liahirishwe kwa dharura ili kujadili kesi yake for national interests wakati ni kitu private ambacho alipaswa kwenda kuonana na spika ili kinga yake ifanye kazi asiende mahakamani, je huo si ujinga wakati yeye ni mwanasheria, aliaibisha wanasheria wote.

  Kimsingi mambo mengine ni ya kitoto kuyafanya ni mada kubwa na kutumia lugha ya matusi kwenye jukwaa hili, ni suala la kuonyesha kuwa uko mature tu na kuwa unaweza ku-reason.
   
 8. mundo

  mundo JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Hii assumption ni sahihi tu iwapo Tume ya Uchaguzi siyo ile tunayofahamu ambayo imejipa kazi ya kutuchagulia viongozi hata tusiowataka.
   
 10. P

  PatriotMzalendo Member

  #10
  Feb 10, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumwambia mtu mjinga (ignorant) si kumtukana bali ni kumwambia kuwa hana uelewa wa jambo fulani. Huyu anapaswa aelimishwe kuhusu yale asiyoyajua. Mfano wa mtu mjinga ni yule anayetafsiri very narrowly hoja ya mbunge aliyelalamikia kuletewa summons ya mahakamani ndani ya kikao cha bunge kwamba ni hoja ya masuala binafsi.

  Wasio wajinga wanaelewa kwamba hoja ya mbunge huyo ililenga kuliomba bunge liahirishe hoja lililokuwa linaijadili ili lijadili kitendo cha mhimili mmoja wa dola kuingilia shughuli za mhimili mwingine kinyume cha kanuni. Halikuwa suala la kibinafsi kama wajinga kadhaa walivyotafsiri. Kwa bahati mbaya sana mmoja wa wajinga hao ni kiongozi mwenyewe wa mhimili uliodhalilishwa ambaye alipaswa kulipa uzito mkubwa suala hilo.

  Mama yetu huyu angejiuliza kwa nini wakati wa Spika 6 hali hiyo haikujitokeza? Je anadharauliwa kutokana na jinsi yake? Angejiuliza zaidi kwa nini ndani ya bunge lake sasa watu wanaingilia kihuni michango ya wenzao kwa maneno kama "shut your mouth!","acha ubinafsi wewe" na mengine kwa kutumia vipaza sauti wakati hali hiyo haikuwepo wakati wa Spika 6, Msekwa wala Mkwawa?

  Leo mhimili mmoja wa dola unaleta summons ndani ya kikao cha mhimili wake kwa kumdharau yeye lakini anasema suala hili ni la kibinafsi na halina maslahi kwa umma! Inabidi ieleweke kwamba mihimili hii ya dola ipo kwa kuhudumia umma.Inapodharauliana na kuamsha chuki miongoni mwao, umma ndiyo utakaoathirika kama mambo yataharibika. Hii mihimili ya dola ipo kwa ajili ya umma na si kwa ajili ya waliomo ndani yao. Kwa hiyo ugomvi wowote baina yao unauhusu umma wote na si suala la kibinafsi kwani utendaji wao ukiathirika kwa ugomvi huo,umma ndiyo utakaoathirika.

  Mtoa hoja alikuwa sahihi kuomba suala hilo lijadiliwe ili likomeshwe kwani kesho anaweza kuletewa arrest warrant spika mwenywe au naibu wake akiwa kazini! Hii inaweza kutokea kutokana na kulilea tatizo la leo kwa kuliita la kibinafsi. Likishughulikiwa kibunge baada ya kumgusa spika au maslahi yake yoyote, litakuwaje wakati huo suala la maslahi ya umma wakati suala hilo ni lile lile linaloitwa leo kuwa la kibinafsi?

  Naomba nikurudishe darasani. Mtu akiambiwa mjinga (ignorant) hatukanwi bali anaambiwa hajui kitu na hivyo ajifunze.Labda akiambiwa mpumbavu (stupid) ndiyo atakuwa ametukanwa. Nadhani nimepunguza kidogo ujinga wako wa kutojua ujinga ni nini.
   
 11. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #11
  Feb 10, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mimi nimesomea mambo ya uhasibu hizo asam'sheni zimenikumbusha kwenye FM na Economics ila kuna somo la Mercantile Law humo mzee wangu hakuna mambo ya assumption na "LAW" ndio inayoongoza katika kila maswala ya utawala watu/sheria inataka facts haitaki assumptions!
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,467
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Tangu kuanza kwa kikao cha bunge juzi Jumanne, hili limekuwa ni bunge lililogubikwa na miongozo ya Spika.

  Leo Madam spika amefikia uamuzi, hataki tena miongozo ya spika, bila kujua ni kanuni gani, kwa maoni yangu, spika hana mamlaka hayo ya kusema hataki tena miongozo, 'hili sio bunge la miongozo', naitafsiri kauli hii kama ya udikteta!.

  Nimekuwa nikifuatilia uendeshaji wa vikao vya bunge tangu hiyo juzi, jinsi Mhe. Makinda anavyoliendesha bunge, napata mashaka kidogo kuhusu uwezo wake ambao nautafsiri kama udhaifu fulani.

  Natolea mfano wa leo, katika kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu, Mhe. Pinda ameliambia bunge kuhusu kilichotokea kwenye uchaguzi wa meya wa Arusha kulikopelekea Chadema kufanya maandamano.

  Kusema ukweli Mhe Pinda alijieleza vizuri, kwa lugha ya staha bila ushabiki wa kisiasa, na Chadema kama wana akili, ujumbe umewafikia.

  PM Pinda alitahadharisha kuwa maelezo hayo anayoyatoa, ni kwa mujibu wa maelezo aliyopewa.

  Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, akaomba muongozo wa spika inapotokea mtu mkubwa kama Waziri Mkuu analidanganya Bunge, ni hatua gani mbunge anaweza kuchukua?.

  Mhe. Spika, Mama Makinda alipanic kwa hamaki na kumjia juu Lema kuwa mtu mkubwa kama Waziri Mkuu anaweza kusema uongo?, yaani alidanganye bunge?, hapo hapo akamshauri Lema alete madai hayo kwa maandishi huku unamuona kabisa Spika yuko emmotional. Huu ni udhaifu!. Kwani PM ni nani mpaka asiweze kusema uwongo, JK mwenyewe anasema mauwongo mara kibao, itakuwa Pinda!?.

  Godbless naye bado ule uchalii wa AR haujamtoka na kumuingiza kwenye uheshimiwa, bado personalty change toka mtoto wa kijiweni mpaka mhe Mbunge haijamvaa kisawasawa, PM kasema taarifa zile kapewa, yeye anasema PM kasema uwango. The right forum ya kutumia ili kulinda heshima ya Waziri Mkuu, alitakiwa aombe muongozo wa spika kwa kusema kwa vile Waziri Mkuu kapewa taarifa ambayo sio sahihi (bila kuiita ya uwongo), jee kuna utaratibu gani wa kusahihishwa kwa taarifa hiyo isiyo sahihi. (Ukimwambia Mkuu, samahani hauko sahihi, ni lugha ya staha zaidi kuliko kumwambia wee muongo!)

  Udhaifu wa Mama Makinda. haukuishia hapo, bali baadaye akaibuka na vifungu vya kanuni vikiambatana na vitisho mpaka kutishia kumtimua Lema Bungeni na kwa jazba akamsimamisha Lema athibitishe papo kwa hapo vinginevyo shoka la spika limshukie.

  Ndipo Mbunge mwingine akaokoa jahazi, kwanza akamzodoa spika kuwa kanuni aliyoileta na vitisho vyake, sio muongozo Lema aliyouomba, pili akamsaidia spika kwa kanuni sahihi na kinachotakiwa kufanywa, Mama Makinda hakuwa na jinsi zaidi ya kunywea na kumtaka Lema awasilishe maelezo yake kimaandishi siku ya Tarehe 14, Asubuhi.

  Hili ni moja tuu la leo, maroroso ya juzi na jana nyote mliyaona ikiwemo ukumbi wa Bunge kugeuzwa ni kijiweni au uwanja wa mipasho na msuto!.

  Ndio maana nauliza kuhusu uwezo wa Spika wetu, ni udhaifu, udikteta, lack of confidence, emmotional etc etc.

  Angalizo: Mhe. Anna Makinda ndio Spika wetu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo anastahili heshima yake kama kiongozi mkuu wa moja ya mihimili ya dola, naomba tujadili hoja hii kwa heshima na lugha ya staa huki tukiondoa any personal attacks, tujadili speakership as an institution na sio Mhe. Anna Makinda as an individual.

  Naomba kuwasilisha.

  Pasco.
   
 13. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #13
  Feb 10, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,462
  Likes Received: 1,336
  Trophy Points: 280
  Naona ipo siku mh. spika huyu atasababisha ukumbi wa bunge utumike kama ulingo wa ndondi, kanuni sawa ila pale busara inahitajika sana...
   
 14. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Anna Makinda kaba hadi penati :clap2::clap2::clap2::clap2::coffee:
   
 15. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #15
  Feb 10, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  mmh!ntarudi baadae.....
   
 16. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #16
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  .....mie naona hatuna spika Bungeni!!!
   
 17. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #17
  Feb 10, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Spika anna anafanya kazi nzuri big up
   
 18. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #18
  Feb 10, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  niliangalia bunge jana yani sio chombo kikuu cha kutunga sheria tena...!!! ni kama club ya pombe za kienyeji na saloon ya kutengeneza nywele za kinamama pale mwananyamala kwa kopa.. yani ni full mipasho! watu wachache sana wanaongea substance wengine ni kuzodoana tu.. tena kwa ushabiki wa vyama, wabunge hawajali maslahi ya taifa kabisa sijaelewa tatizo ni nini?
   
 19. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #19
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Pasco.

  Mheshimiwa Spika Anna Makinda kapewa nafasi kubwa kuliko uwezo wake lakini nadhani itawasaidia zaidi wapinzania iwapo watajipanga vizuri hasa namna ya kucheza na kanuni za Bunge.

  Kuhusu mheshimiwa Godbless Lema mbunge wa Arusha I reserve my comments msimamo wangu unajulikana kabla hajawa mbunge sasa ni mbunge wangu hata kama sikumpa kura si vizuri nikaendelea kushika bango.
   
 20. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Haya ndio madhara ya kuchagua kiongozi kwakufuata "jinsia na si uwezo"
   
Loading...