Bunge la kumi chini ya Makinda na Ndogai ni bomu tupu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge la kumi chini ya Makinda na Ndogai ni bomu tupu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Byendangwero, Mar 15, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kabla ya kuanza kwa kikao cha bunge lililopita, iliandaliwa semina elekezi inayodaiwa ililenga katika kuwapatia wabunge hao ujuzi unaohitajika katika kutekeleza jukumu lake la kusimamia utendaji wa serikali. Cha kushangaza semina hiyo ilisimamiwa na viongozi wa juu wa serikali. Jambo hilo liliwafanya wengi kujiuliza, inakuwaje yule unayetakiwa kumdhibiti ndiye akufundishe namna nzuri ya kumdhibiti? Vivyo hivyo, wakati bunge linajiandaa kwa kikao cha April, hivi sasa wabunge wako kwenye semina wakifundishwa na serikali jinsi ya kuifanyia marekebisho sheria ya manunuzi ili kuruhusu serikali kununua mitambo mtumba ya Dowans. Hali hiyo inatufanya baadhi yetu tujiulize, hivi kunu haja gani ya kuteketeza matrilioni ya fedha kugharimia bunge ambalo linafanya kazi kwa maelekezo ya serikali!
   
Loading...