Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sasa linatawala nchi

President Elect

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Messages
690
Points
195

President Elect

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2011
690 195
Baada ya Rais Jakaya Kikwete kushindwa kuchukua maamuzi magumu, hususan dhidi ya vitendo dhahiri vya ubadhirifu na uporaji wa raslimali za nchi yetu, hatimaye bunge letu tukufu limeanza kushika hatamu za utawala.

Leo asubuhi, naibu spika ameitisha kikao cha kamati ya uongozi ya bunge, ili kuamua juu ya hoja ya kusitisha shughuli za serikali bungeni.

Serikali ijirekebishe haraka, la sivyo itaanguka polepole!

Kashfa ya D. Jairo inahusika, bunge limedhalilishwa sana!
 

President Elect

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Messages
690
Points
195

President Elect

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2011
690 195
Zainabu Vullu: Luhanjo amekiuka katiba.

Ole Sendeka: Luhanjo ameingilia uhuru wa bunge. Iundwe kamati teule ya bunge kuchunguza ya Jairo na Luhanjo.

Naibu spika ameridhia! Haiwezekani Luhanjo amdharau Waziri mkuu na bunge likae kimya!
 

mikogo

Senior Member
Joined
Jul 24, 2011
Messages
175
Points
195

mikogo

Senior Member
Joined Jul 24, 2011
175 195
Mambo Ya Bungeni yanaleta matumaini. Bwana Luhanjo naye pamoja na kujisifia uzoefu wa utendaji kazini, Inasikitisha kwa kulikoroga. Tuwape jina gani hawa ? inaumaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 

Marcossy A.M

Verified Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
61
Points
95

Marcossy A.M

Verified Member
Joined Aug 21, 2008
61 95
Ndugai, ndugu yangu yuko hoi: alipelekewa vimemo tisa ndani ya dakika nne. Alisoma kimoja tu akaendelea na hoja zake kuhitimisha hoja ya Zitto na Sendeka: SASA AMEITWA PEMBENI KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI HAIJAANZA HADI SASA..... Sijui kama atalala leo.
 

Gama

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
10,481
Points
2,000

Gama

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
10,481 2,000
Dhana ya utawala bora imekiukwa kwa kiasi kikubwa sana.
.

Imekiukwa vipi MKUU,! bunge lilikubali serikali ichunguze, majibu ya uchunguzi yanatoka wewe unasema siyo utawala bora?!, kama hawakutaka majibu ya nje ya bunge kwanini walitaka vyombo kusiaka vichunguze?!, BTW, umeona hitimisho la mjadala wa hoja ya Jairo?!. Mkono ameomba mwongozo-amefungwa mdomo. Alikuwa anauliza kwamba je ni halali bunge kutoa hukumu bila kumsikiliza mtuhumiwa?!. Hapa wenye mawazo kama yako imekula kwenu .
 

Ngareni3

Member
Joined
Dec 4, 2006
Messages
32
Points
0

Ngareni3

Member
Joined Dec 4, 2006
32 0
N

ionavyo mimi kitendo alichokifanya Katibu Mkuu Kiongozi Bwana Philemon Luhanjo ni dharau. Ni dharau kwa Waziri Mkuu; Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni; ambaye kwa uchungu mkubwa, akiwa na dhamira safi uamuzi wake ulikuwa kumtimua kazi Bw. Jairo hata kama alikuwa na nia njema lakini nje ya utaratibu. Sote tunakumbuka sauti na maneno aliyotumia Waziri Mkuu siku ile bungeni akikiri kuwa ni kwa sababu tu mamlaka ya uteuzi ya makatibu wakuu anayo Rais. Pinda alionyeshwa kukerwa. Sote tunaamini kuwa Waziri Mkuu alipata taarifa za kiinteligensia mara baada ya kuipata taarifa ya Bw. Jairo, na kwa uamuzi wake alidhirika kuwa kuna ndivyo sivyo katika hilo. Lililotokea baada ya kukerwa huku ni hadithi nyingine. Ni dharau kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Suala hili lilianzia kwa wabunge ndani ya Bunge, hoja na udhibitisho ulikuwapo inakuwaje liishie kwa Waandishi wa Habari, na wabunge pamoja na Waziri Mkuu wasikilise maamuzi katika vyombo vya habari? Taarifa hizi zingerudishwa bungeni pale zilipoanzia. Huku ni kuonyesha kuwa chombo hiki cha kutunga sheria hakina ukakika na kinachoongelewa ndani ya bunge hilo na kuingia ndani ya hansard. Ni dharau kwa Mheshimiwa Shelukindo aliyeibua barua ya Bw. Jairo bungeni na wabunge wote waliomuunga mkono. Ni dharau ya wazi kwa wananchi wao. Ni dharau kwa wananchi ambao wanawakilishwa na wabunge. Mbwembwe alizoonyesha Katibu Mkuu Kiongozi kuwa yeye ndo mwenye dhamana ya nidhamu kwa makatibu wakuu na kumpa Bw. Jairo likizo ya malipo ilhali wananchi wakijua kuwa huyu kwa namna moja au nyingine ametumia vibaya fedha za wananchi. Wananchi wanaoshindia mlo mmoja, hakuna huduma za afya; zipo hospitali bila dawa; madarasa bila vitabu wala waalimu. Leo Wizara moja inachangisha; hata hizo milioni mita tano kwa ajili ya kupitisha bajeti. Ni dharau kwao.
 

timbilimu

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2010
Messages
4,808
Points
1,250

timbilimu

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2010
4,808 1,250
Wabunge na hasa wa CCM wajiulize ni kwanini watendaji wa serikali wanawadharau... Kama hawana jibu,basi waendelee kuzomea na kugonga meza na kupitisha miswaada ya hovyo kwa kura zao za ndiooo...!
 

Mwendabure

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2011
Messages
2,143
Points
2,000

Mwendabure

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2011
2,143 2,000
Binafsi bado sijapata pa kupumulia kwa hakika!! Filamu ya jairo inaendelea, kinachofuata ni vikao vya wabunge wa magamba kupeana vitisho. Natamani niwe macho usiku na mchana mpaka siku magamba wanaondoka madarakani. Waingie wengine na sarakasi mpya...Loh!
 

Shenkalwa

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2011
Messages
580
Points
170

Shenkalwa

JF-Expert Member
Joined May 3, 2011
580 170
Baada ya Rais Jakaya Kikwete kushindwa kuchukua maamuzi magumu, hususan dhidi ya vitendo dhahiri vya ubadhirifu na uporaji wa raslimali za nchi yetu, hatimaye bunge letu tukufu limeanza kushika hatamu za utawala.

Leo asubuhi, naibu spika ameitisha kikao cha kamati ya uongozi ya bunge, ili kuamua juu ya hoja ya kusitisha shughuli za serikali bungeni.

Serikali ijirekebishe haraka, la sivyo itaanguka polepole!

Kashfa ya D. Jairo inahusika, bunge limedhalilishwa sana!
Hata hilo bunge halina chochote. Ili mradi wabunge wa magamba ndiyo wengi humo ndani usitegemee zaidi ya Ndiyooooooooooo, siyoooooooooooooooo ambazo hazina tija kwa maendeleo ya nchi hii zaidi ya kulindana, kuuza nchi kwa masilahi yao, kuendelea kuwaona watanganyika ni mazuzu.
 

Akami

Member
Joined
Sep 18, 2009
Messages
83
Points
0

Akami

Member
Joined Sep 18, 2009
83 0
Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza mheshimiwa Ndugai kwa kutumia busara kukubali hoja ya Mheshimiwa Zito na vile kukubali iundwe kamati ya kuangalia suala hilo kwa undani.Lakini tukirudi nyuma,yeye mwenyewe naibu spika kwa maneno yake amesema,''Bunge haliwezi kuona Waziri mkuu amedharauliwa kiasi hiki likakaa kimya.''TAFSIRI YAKE NI KWAMBA,NI KWELI WAZIRI MKUU NA BUNGE KWA UJUMLA WAMEDHARAULIWA.Sasa mheshimiwa Pinda anasubiri nini?Naamini Watanzania wote watamuunga mkono kama hatasubiri ripoti ya tume.akachukua uamuzi wa kujiuzulu,atabaki na heshima yake na heshima kwa bunge na Watanzania wote kwa ujumla!

Jipumzikie mzee Pinda,serikali yenyewe hii ya kisanii,wakati wewe ni mchapa kazi!
 

Forum statistics

Threads 1,356,356
Members 518,895
Posts 33,130,999
Top