Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ni dhaifu,limekidhi mitindo tu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ni dhaifu,limekidhi mitindo tu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, Aug 5, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Uwepo wa bunge letu unakidhi MITINDO na kuachilia mbali uwajibikaji. Kutokana na tabia na mienendo ya Wabunge hasa wa chama tawala kujipendekeza kwa serikali ipo haja ya kufanya mabadiliko makubwa.

  Demokrasia bungeni na kazi za bunge zimekuwa na kasoro kubwa sana kutokana na kupokwa mamlaka na mhimili mwingine wa dola yaani serikali.

  Kwa mwenendo wa sasa bunge halina sababu ya kuwepo na zile gharama na fedha zinazotumika kwa shughuli za bunge zingenufaisha taifa zaidi kama zingetumika kwa kujenga mahitaji muhimu ya nchi kama vile shule na hospitali.

   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  mmmh, hivi haya maoni si yanafaa kupelekwa kwenye kamati ya maoni ya katiba mpya??
   
 3. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  • Raisi wa nchi awe na wajibu wa kuridhisha hoja za wabunge (answerable to the parliament) na aondolewe ule uwezo wa kulivunja bunge.


  • Utaratibu wa Mbunge kupita bila kupingwa wakati wa uchaguzi ufutwe, Iwapo mgombea atagombea bila kupingwa, wapiga kura wa jimbo husika waruhusiwe kupiga kura ya NDIYO au HAPANA. Jambo hili vilevile litasaidia kupunguza rushwa.


  • Mwenyekiti, makamu mwenyekiti au katibu mkuu chama kwa chama kilichoshika madaraka ya nchi wasiruhusiwe kwa pamoja na kazi hizo za chama kwa wakati mmoja wachukue kazi ya Raisi wa nchi, makamu wa Raisi au Uwaziri serikalini.


  • Zile nafasi za uteuzi bungeni zisizidi kumi na tano na ziendane na mahitaji maalum na sifa na uwezo wa mteule na kuindhinishwa na bunge. Tufute utaratibu wa viti maaalum hauna tija kwa taifa.


  • Tuwe na mawaziri wasiotokana na wabunge.


   
 4. All TRUTH

  All TRUTH JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 3,275
  Likes Received: 983
  Trophy Points: 280
  mnyika alisema
   
 5. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Are you configured...and you follow the same configuration, wewe unasemaje...
   
 6. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 866
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  hata ukiyapeleka,tume ya kuratibu katiba mpya , mwsho lazima ipeleke kwa rais ambaye naye ndo atapeleka kwenye bunge la katiba, huoni akipelekewa atahariri yale ambayo anataka?pia mteuzi wa bunge la katiba ni rais huoni kuwa atateua walewale wa "imeafikiwa" jibu NDIYO!!!!!!!!,kupitisha hata ujinga. pia ni lazima ikipitishwa na bunge lazima ipigiwe kura ya maoni kukubali au kukataa.Anayeteua tume ya kuendesha kura hii huoni ndo rais huyo huyo dhaifu?walewale watapitisha inawezekana ikawa katiba mbay kuliko hata ya sasa.na mwisho hata mkiikataa katiba hiyo, mtaendelea kutumia hii hii ambayo ndo ya bunge dhaifu.
   
Loading...