Bunge la Jamhuri ya Muungano limepitisha muswada wa sheria unaotamka kuwa kukutwa na bangi, mirungi sasa ni kosa la jinai

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
4,078
2,000
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardius Kilangi aliwasilisha muswada huo bungeni jana Jumanne Septemba 7, 2021 ambapo muswada umeongeza uzito wa bangi na mirungi kwenye makosa yanayosikilizwa katika Mahakama Kuu na mahakama za wilaya.

Profesa Kilangi amesema awali sheria haikutamka kama ni kosa la jinai ingawa ilizuia kitendo hicho bila kutamka jinai.

Mirungi na bangi ni miongoni mwa dawa za kulevya ambazo Serikali imekuwa ikipambana kukomesha vitendo hivyo kama ilivyo kwa dawa zingine.

"Lengo la marekebisho haya ni kupunguza mrundikano wa kesi mahakama za wilaya zinazosubiri kupelekwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa," amesema Kilangi.

Amesema mbali na marekebisho ya vifungu vya 15 na 15A katika kuongeza uzito huo, kifungu cha 17 kinarekebishwa ili kufanya kuwa kosa la jinai kitendo cha kukutwa na au kutumia kiwango kidogo cha dawa za kulevya.

Amesema kwa sasa, sheria inazuia kitendo hicho bila kutamka kuwa ni kosa la jinai jambo lililoonekana kuwa na upungufu wa kisheria wakati wa kutoa haki.

Wabunge waliotoa maoni yao kwa kukubaliana na pendekezo la Mwanasheria Mkuu hivyo wanasubiri saini ya Rais ili kuwa sheria kamili.

Mwananchi
 

THE LOST

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
1,638
2,000
Watanzania ni wehu hata bila ya kuvuta bangi, sasa na matumizi holela ya bangi taifa limekuwa na watu wa hovyo kweli.
 

Kavirondo

JF-Expert Member
May 2, 2020
427
1,000
Mentality za kijamaa zimetuathiri sana..
Wakati Kenya inapata takribani $ 17mill kwa Mwezi kwa biashara ya Miraa,sisi tunazidi kutengeneza mazingira ya kuharamisha..
Kwenye cannabis ndio sitaki kugusa kabisaa maana tunazidi kuonekana kituko.. Nafahamu vyote vina madhara,lakini ni suala la kutengeneza mazingira bora ya namna vitakavyo tusaidia kiuchumi..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 

Spider

JF-Expert Member
Feb 13, 2011
1,626
2,000
Mbona mnamsumbua bwana Job Ndugai Kwa kumuita AG Profesa!Anasumbuka sana akisikia jina la mtu likianzia na profesa,wakili msomi,injinia,dokta,CPA-T.
Tafadhali msimsumbue Mtaalamu wa kilimo(mwanasayansi) Job Ndugai.
Agriculturist Job Ndugai,atambulike Kwa fani yake pia.
 

TsafuRD

JF-Expert Member
Sep 29, 2013
2,008
2,000
Huu ni miongoni mwa muswada mbovu sana kupitishwa.
Muswada huu unainyima nchi fursa ya kupata mapato ambayo yangetokana na kilimo na uuzaji wa bidaa hizo pendwa duniani.
na Pili tunaongeza mzigo kwa Mahakama kuu bila sababu za msingi. Maana yake sasa hata yale mateja ya pale River Side na Ubungo Terminal n.k yanatakiwa kesi zao za misokoto njaa itolewe uamuzi Mahakama kuu.
 

TsafuRD

JF-Expert Member
Sep 29, 2013
2,008
2,000
Mbona mnamsumbua bwana Job Ndugai Kwa kumuita AG Profesa!Anasumbuka sana akisikia jina la mtu likianzia na profesa,wakili msomi,injinia,dokta,CPA-T.
Tafadhali msimsumbue Mtaalamu wa kilimo(mwanasayansi) Job Ndugai.
Agriculturist Job Ndugai,atambulike Kwa fani yake pia.
Bwana Job Ndugai ni Afisa wanyama Pori. Ndo maana wakati mwingine tabia zake zinafanana za Nyati.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom