Bunge la EALA laanza kwa kishindo cha Ukata

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Bunge la Nne la Jumuiya ya Afrika Mashariki EALA, limeanza kikao chake cha kwanza cha mwaka 2019/20 kwa kuangazia masuala mbalimbali ikiwemo kuzagaa kwa silaha ndogo ndogo kwa nchi za jumuia hiyo pamoja na nchi wanachama kutolipa michango yao kwa wakati .

Hatua ya kusuasua kwa michango ya nchi wanachama, kumesababisha ukata kwa wabunge wa EALA ,kuchelewa malipo ya posho zao kwa zaidi ya wiki tatu tangu kuanza kwa vikao vya Bunge vikitanguliwa na kamati mbalimbali na kupelekea kukosa fedha za kujikimu.

Mmoja ya wabunge wa bunge hilo dkt, Abdulah Makame amesema kuwa bunge hilo litapokea na kujadili taarifa ya kamati ya kanda inayosimamia masuala ya usuluhishi wa migogoro juu ya kuzagaa kwa silaha ndogo ndogo katika nchi wanachama.

Dkt.Makame amesema kuwa hoja nyingine itakayojadiliwa ni kusudio la kuomba baraza la mawazili wa jumuiya ya Afrika mashariki kuleta taarifa ya utekelezaji wa itifaki ya umoja wa forodha na soko la pamoja kwa ukamilifu wake baada kubaini kuwa bado Kuna masuala hayajatekezwa ipasavyo.

"Pia tunataka baraza la mawaziri watueleze kwanini baadhi nchi wanachama zisichukuliwe hatua kwa kushindwa kuchangia michango yao ipasavyo"

Hoja nyingine ni nchi wanachama kushindwa kuchangia michango yao ipasavyo na kusababisha kukwamba kwa baadhi ya masuala ya maendeleo ya jumuia hiyo na taasisi zake ikiwemo mishahara ya wafanyakazi kutolipwa kwa wakati.

Naye mbunge wa EALA nchini Tanzania Mh, Habibu Mnyaa amesema kuwa changamoto kubwa inayoikabili jumuiya hiyo ni kwa baadhi ya nchi wanachama kushindwa kulipa michango yao kwa wakati kama utaratibu na sheria za jumuiya hiyo zinavyoelekeza.

Mnyaaa amedai kwamba hali hiyo imesababisha hata posho zao kutolipwa kwa wakati kwani katika kipindi cha wiki tatu walichoketi katika vikao vyao vikitanguliwa na kamati mbalimbali hawajalipwa chochote jambo walilodai linawawia ugumu kuendesha maisha yao ukizingatia wanalala hotelini.

Amesema katika nchi wanachama ,nchi ya sudani kusini ndio nchi pekee ambayo tangu ijiunge na jumuiya hiyo mwaka 2016 imechangia kiasi kidogo sana na kwamba hadi hivi sasa inadaiwa zaidi ya dola za kimarekeni milioni 15 ikifuatiwa na nchi ya Burundi ambayo imejitahidi kupunguza madeni yake.

Hata hivyo ,Mnyaa amekanusa nchi ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi ambazo zinasuasua kulipa michango yao na kudai kuwa Tanzania ,Kenya na Uganda zimekuwa zikilipa vizuri michango yao ndio maana hadi sasa jumuia hiyo inaweza jujiendesha.

Ends.....


images%20(1).jpeg
 
Back
Top Bottom