Bunge la chini la Brazil laidhinisha kuenguliwa kwa rais Rousseff

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
20160418211949519_81299.jpg


Baraza la chini la bunge la Brazil limepiga kura ya kuidhinisha kuenguliwa madarakani kwa rais Dilma Rousseff.


Idhini hiyo imepitishwa na wabunge 342 ambao ni theluthi mbili ya wabunge wote. Hii inamaanisha kuwa sasa bunge la juu litapiga rasmi kura ya kumwondoa rais madarakani katika wiki kadhaa zijazo.

Kama katika duru ya kwanza kura za ndiyo zitakuwa chini ya nusu ya kura zote, bunge la juu litachukua hatua na rais Rousseff atalazimika kusimamishwa kazi kwa siku 180, wakati ambapo makamu wa rais Michel Temer ndio atakuwa kaimu wa rais.

Lakini kama kura za ndiyo zikizidi theluthi mbili ya kura zote katika duru ya pili, rais Rousseff ataondolewa kabisa madarakani na Temer atashika madaraka.

Rousseff anatuhimiwa kwa kuvuruga bajeti kabla ya uchaguzi wa mwaka 2014 lakini anasema hana makosa yoyote ila tu anasingiziwa kisiasa ili kumwondoa madarakani.


Chanzo:CRI
 
Back
Top Bottom