Tanzania ina uzoefu wa kuwa na Bunge la chama kimoja, lkn pamoja na kuwa na bunge la chama kimoja kulikuwa na mijadala mikali na hoja nzito zilizojadiliwa ukiwamo ule wa kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika uliotokea kwenye miaka ya 1990 al maarufu kama G55.
Wabunge wa CCM wa wakati huo kina, Njelu Kasaka, Jenerali Ulimwengu, Philip Marmo na wengine, walikuwa ni watu waliojiamini waliojengwa kwenye chama na ambao walikuwa tayari hata kufukuzwa ndani ya chama.
Tofauti ya mabunge hayo ya nyuma na linalotarajiwa kuwa Bunge la sasa ni historia ya watakaounda kundi hilo.
Kwenye bunge la awamu iliyopita ukiwaondoa wabunge wa upinzani, kazi kubwa ya wabunge wa CCM ilikuwa ni kuitetea serikali, matusi ya akina Lusinde yalielekezwa kwa wapinzani, Spika alimalizia hasira zake kwa kuwafukuza wapinzani.
Kwenye bunge la awamu hii Serikali itakuwa inajitetea yenyewe, spika atakuwa anawafokea wanaCCM wenzake wabunge wa CCM watakuwa wanaihoji Serikali na kwa kufanya hivyo lazima kutatokea kupishana kati ya utawala na wabunge na kati ya serikali na baadhi ya wabunge wa CCM, baadhi yao wataonekana kama wasaliti wanaofanya kazi ya upinzani, na hapo ndipo tunaweza kupata kundi lingine kama la G55 ndani ya bunge la chama kimoja.
Wakati wa G55 zisingekuwa busara za Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kukemea CCM ingepasuka vipande viwili, safari hii bahati mbaya hatuna kiongozi wa kalba ya Nyerere, ukitokea mgawanyiko ndani ya Bunge la chama kimoja sioni mtu sahihi au kiongozi anayeweza kuwaunganisha pasipo kuwaumiza.
====
Zaidi, soma: Kundi la G55 walioidai Tanganyika mwaka 1993...