Bunge la CCM, siku zote litatetea ufisadi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Posted Date::6/7/2008
Richmond: Kundi la wabunge lajipanga kutetea bungeni
*Nia ni kuonyesha waliotuhumiwa wameonewa
*Laweka mkakati kutaka kumng'oa Spika

Na Midraji Ibrahim
Mwananchi

MZIMU wa Kampuni iliyopewa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond Development, unatarajia kuibuka kwa kasi mpya kwenye Kikao cha Bunge cha Bajeti kinachotarajia kuanza Keshokutwa.

Kuibuka upya kwa suala hilo, inaelezwa ni kutokana na kuibuka kwa baadhi ya wabunge waliobadilika ghafla na kuanza kutetea kampuni hiyo inayolipwa, huku wengine wakisubiri utekelezaji wa maazimio ya Kamati ya Bunge iliyochunguza mchakato wa ushindi wa zabuni hiyo.

Pia, suala la Spika Samuel Sitta linatarajiwa kutawala mjadala, huku kukiwa na kundi linalotaka kuwasilisha hoja binafsi ya kutaka kumng'oa madarakani kwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

Imeelezwa kundi hilo la wabunge lililoibuka kutetea Kampuni ya Richmond, linadaiwa kutumia mamilioni ya shilingi kuwashawishi wabunge kubadilisha msimamo wao, ili wasimame kutetea watuhumiwa wa Richmond kuwa wanaonewa.

Kundi hili ambalo linaundwa na baadhi ya wabunge wakongwe na wenye ushawishi mkubwa, lilikuwa limejiandaa kuwasilisha ajenda kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wabunge wa chama hicho, kilichokuwa kifanyike Alhamisi katika Hoteli ya White Sands, jijini Dar es Salaam.

Richmond iliuzwa kwa Kampuni ya Dowans ambayo inalipwa Sh152 milioni kila siku, licha ya uzalishaji wa umeme hivi sasa kurejea katika hali ya kawaida. Dowans ndiyo inayolipwa fedha za mitambo hiyo.

Taarifa kutoka Wizara ya Fedha, zinabainisha kuwa mmoja wa wafanyabiashara amekuwa akifuata hundi za malipo hayo kila mwezi, huku akidiriki kuwa mkali pindi malipo yanapocheleweshwa.

Katika hoja ya kundi hilo, linadai Richmond licha ya kutajwa kwenye Kamati ya Mwakyembe iliyochunguza kashfa hiyo haijawahi kulipwa hata senti moja, lakini imekuwa ikisakamwa bure.

''Nakwambia kwenye Bunge la Bajeti mtashangaa, kuna watu wamebadilika. Kuna kundi la wabunge ambalo limeandaliwa na lilikuwa liwasilishe hoja ya Richmond kwenye kikao chetu cha CC (kamati kuu) na wabunge kule White Sand, baada ya kuahirishwa tangu juzi (Jumanne) wanatapa tapa," kilisema chanzo chetu.

Inadaiwa kundi hilo pia limeanzisha kampeni ya kujijenga kisiasa na limeapa kumpata mrithi wa Rais Jakaya Kikwete mwaka 2015 baada ya kumaliza ngwe yake.

Uchunguzi wetu unaonyesha kuwa kundi hili la wabunge limekuwa likifanya mambo mbalimbali likijipanga na sasa limefanikiwa kumega wabunge katika suala la Richmond.

''Wamefanya vikao vingi na vyote serikali inavifahamu, baada ya kuona wameanza kujulikana, walivipeleka kwa mbunge mmoja (jina tunalo) kule Mikocheni na wanamwaga fedha kweli kweli,'' kilisema chanzo kingine.

Kundi hilo linadaiwa kufanikiwa kushawishi baadhi ya viongozi wa juu wa CCM na wabunge ambao walikuwa na mtazamo tofauti awali, lakini hivi sasa wanaliunga mkono.

Chanzo chetu cha habari kilisema, wiki hii kuwa kundi la wabunge ambalo 'limenunuliwa' lilikuwa limejiandaa kupeleka ajenda mbili kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CCM na wabunge.

''Moja ilikuwa hiyo ya kutetea Richmond na nyingine ya kutokuwa na imani na Spika. Kwa sababu gani? Spika ndiye ameruhusu hoja mbalimbali ambazo zimewasilishwa bungeni, mojawapo ni hiyo ya Richmond,'' kilisema chanzo hicho na kuongeza:

''Pia, kundi hilo lilikuwa limeandaliwa ukikumbuka wakati wa kesi ya Adam Malima na Reginald Mengi, lakini busara ya Spika ikaliacha linahangaika. Aliyeandaliwa kutoa hoja ya kutokuwa na imani na spika alikasirika akatoka nje.''

Inadaiwa kundi hilo hivi sasa linajenga hoja kuwa, katika mazungumzo yake na wahariri wa habari, Sitta alitamka kanuni za bunge zimempa madaraka makubwa yeye na naibu spika, ndio maana anapitisha hoja za kukandamiza CCM.
 
Ama kweli yule jamaa aliyeandika kitabu cha The Shacked Continent (Africa), nakubaliana nae kabisa kwa sababu ya madudu haya ya viongozi wa kiafika
 
Wote wanaoturudisha nyuma ni kuwaweka alama.
Dawa ya kuwatema 2010 iko jikoni inatokota.
 
Yaliyotokea EPA, Richmond na BoT yalikuwa ni matatizo ambayo chama cha mafisadi ingeyatumia ili kujisafisha na kurudisha credibility yake kwa wananchi, lakini wamelewa madaraka na kuwa na kiburi cha kupindukia ndio maana bado wanataka kuwatetea mafisadi wa Richmond, kumtupia lawama Ballali kwenye EPA n.k. Tatizo lingine kubwa tulinalo bado Watanzania hatujaona chama ambacho kinaweza kutuondolea kero kubwa kwa kuiondoa CCM madarakani. Vyama vilivyokuwepo pamoja na kuwa vimefanya mengi mazuri lakini haviko tayari kuyashughulikia mapendekezo ya Watanzania waungane ili waunde chama kimoja chenye nguvu.
 
Ama kweli yule jamaa aliyeandika kitabu cha The Shacked Continent (Africa), nakubaliana nae kabisa kwa sababu ya madudu haya ya viongozi wa kiafika

Kwa Tanzania kuna dalili ya madudu haya kufikia ukingoni kama Watanzania tutaendelea kushika uzi huu huu wa kuwashinikiza mafisadi waliokuwa madarakani na kuwaambia bila woga wala aibu kwamba tumechoka na ufisadi wao unaoingamiza nchi.
 
WAsubir tutapandana nao 2010 kwani ni mbali? dawa yao iko jikoni!

Itakuwa ni raha iliyoje kukiondoa chama cha mafisadi madarakani. Itakuwa ni sawa na kupata uhuru kwa mara ya pili kama ule ambao Tanganyika iliupata December 9, 1961. Lakini mafisadi yamejizatiti vya kutosha kwa kuvinunua vyombo vyote vya dola hivyo si ajabu kabisa kuona karibu na uchaguzi wanachama na viongozi wa upinzani wakitishwa, kunyanyaswa na hata kupigwa na kama kama unavyojua kule Visiwani baadhi walipoteza maisha yao kwa kuwa upande mmoja na wapinzani na hadi hii leo hawajetendewa haki yoyote na sirikali.
 
Back
Top Bottom