Chivundu
Platinum Member
- Dec 17, 2012
- 7,562
- 6,511
Bunge la tatu la Afrika Mashariki linamaliza muda wake Juni mwaka huu na tayari mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yamepewa taarifa kuhusu kutakiwa kufanya uchaguzi wa wabunge kabla ya Juni mwaka huu.
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, ameliambia gazeti la Raia Mwema kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa wamekwisha kupokea barua ya kuwataka waanze mchakato wa kupata wabunge na tayari vyama vya siasa vimearifiwa.
“Sisi, kama mambo yote yataenda kama yalivyopangwa, tunatarajia kufanya uchaguzi wa wabunge wa EALA Aprili mwaka huu wakati wa Bunge la Bajeti.
“Muda si mrefu tutakutana kwa ajili ya kufanya makubaliano ili kujua idadi ya wabunge kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wa kutoka Upinzani. Tanzania ina nafasi tisa na zinatakiwa kuzingatia vyama, jinsia na Muungano” alisema Ndugai.
HOJA YANGU: Kufuatia umuhimu wa Bunge hilo hasa ukizingatia kwamba Bunge linalokuja linaweza kuwa ndilo lenye kukamilisha suala la kuundwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki (East Africa Federation),ni wazi kuwa tunahitaji mjadala mpana wa mambo yafuatayo kuelekea kuwapata Wabunge wetu hao na Mwenendo wa Bunge husika.
Kwa kuwa Mchakato wa kuwapata Wabunge wa bunge la Afrika mashariki huwa unagubikwa na Kujipendekeza na Itikadi vya vyama,hali inayopelekea kupata wabunge wenye ambao hawawezi tuwakilisha vyema.
Tuwe na mjadala wa wazi hapa JF tujadili mchakato inayoanzia ndani ya vyama na tupaze sauti na kushauri kuelekea mchakato mzima wa Upendekezaji toka vyama vya siasa na Uchaguzi utakao fanyika Bungeni.
"Diplomasia ya Afrika Mashariki ni uchumi na uwakilishi mzuri ndio nyenzo yetu ya kunufaika na shirikisho hilo"