Bunge la 2005-2010: Mhagama, Slaa ndio wachangiaji hodari. Rostam Aziz ashika mkia. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge la 2005-2010: Mhagama, Slaa ndio wachangiaji hodari. Rostam Aziz ashika mkia.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by epigenetics, Aug 17, 2010.

 1. epigenetics

  epigenetics JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2010
  Joined: May 25, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kwa kipindi cha bunge 2005-2010, Mhe. Jenista Mhagama (CCM, Peramiho) amekuwa mbunge hai (active) kati ya wabunge wote (zaidi ya 270). Katika bunge hilo (2005-2010) Mhe. Mhagama aliuliza maswali ya msingi 25, maswali ya nyongeza 65, na ya kuchangia 272 na hivyo kuweka jumla ya michango yake kufikia 362.

  Yeye anafuatiwa na Mhe. Ndugai (CCM, Kongwa) aliyekuwa na jumla ya michango 286, na nafasi ya tatu ikishikiliwa na Mhe. Dr Slaa (Chadema, Karatu) mwenye michango 265. Wa nne ni Zitto Kabwe (Chadema, Kigoma Kaskazini) aliyekuwa na michango 239.

  Mhe. Rostam Aziz ameshika mkia kwa kutokuwa na ushiriki wowote wa kuuliza maswali ya msingi, maswali ya nyongeza, au michango kwa kipindi chote cha ubunge wake (kati ya 2005-2010) . Mbunge huyu ni pekee kutofanya hivyo katika kipindi cha miaka 5 iliyopita.

  Source: Do they work for us?
   
 2. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ninampenda sana jenesta mhagama...amedhihirisha kuwa uwezo wa kuongoza anao....natamani awe spika siku moja
  mix with yours
   
 3. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ukitilia maanani kuwa alikuwa mmoja wa wenyeviti wa bunge ambaye mara nyingi alikuwa katika kiti cha spika ni wazi mama huyu ana mapenzi ya dhati na kazi ya kuwawakilisha wananchi. Hongera Mama Mhagama.
   
Loading...