Bunge kuzungumzia hoja ya wapinzani kuhusu Naibu Spika

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
KATIBU wa Bunge, Dk Thomas Kashillilah leo ataeleza kinachoendelea kuhusu kusudio la Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kutaka kumwondoa madarakani Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.

Kambi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe katika migomo yake dhidi ya vikao vinavyoongozwa na Dk Ackson, iliwasilisha kusudio hilo kwa Ofisi ya Spika wa Bunge wiki iliyopita kwa maelezo kuwa haina imani naye.

Kwa mujibu wa Dk Kashillilah, ataeleza kinachoendelea leo baada ya kumaliza kupitia taratibu zote na kujiridhisha kuhusu kila hatua inayopaswa kufuatwa kuhusu suala la aina hiyo. “Nitaeleza kinachoendelea kesho (leo) baada ya kujiridhisha kuhusu taratibu zinazopaswa kufuatwa kuhusu suala hilo,” alisema.

Katika kusudio hilo lililowasilishwa na Mbunge wa Simanjiro, James ole Millya, Kambi hiyo ya Upinzani ilieleza mambo sita yaliyoisukuma kuona kuwa Dk Tulia hafai kuendelea kushika kiti cha Naibu Spika.

Mambo hayo ni upendeleo kwa wabunge wa CCM, kusimamia maslahi ya Serikali badala ya umma, kutokuwa mwanasiasa, jambo linalomfanya akose uzoefu wa kuendesha vikao vya Bunge, ubabe, unyanyasaji kwa wabunge wa upinzani na kusimamia fedha za Mfuko wa Bunge zirudishwe kwa Rais.

Millya alisema walipeleka kusudio hilo kwa Ofisi ya Spika kwa kuzingatia ibara ya 85(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayozungumzia hatua za kuchukua ili kumwondoa madarakani Naibu Spika.

Ibara hiyo inasema, “Naibu Spika atakoma kuwa Naibu Spika na ataacha kiti cha Naibu Spika ikiwa mtu huyo ataondolewa kwenye madaraka ya Naibu Spika kwa azimio la Bunge.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa ili hoja hiyo ijadiliwe bungeni italazimika kujadiliwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ambayo nayo inahitaji theluthi moja ya saini za wabunge wote.

Source: Habari Leo
 
Wabunge wasifanye makosa huyu naibu spika ameandaliwa kushika nafasi hiyo. Wajiulize ni kwa ajili ya nini? Mwalimu alisema dhambi ya ubaguzi haiishii hapo, leo wapinzani wa vyama, kesho ni CCM wanaoongea sana. Wakumbuke wao ni wawakilishi wa wananchi na siyo serikali.
 
Kile kiti inabidi awe anapewa mtu ambaye umri umeenda kidogo.
Na anauzoefu na maswala ya bunge. Hapo nahisi walifanya makosa kumtoa binti shuleni juzi tu leo amepewa unaibu spika.
Amepata wapi uzoefu?
Yule binti saizi ilibidi akae kwanza benchi ajifunze. Wakubwa wake wanavyo fanya kazi.
 
Huu moshi unao fuka udhibitiwe haraka sana maaana tunao athirika ni sisi wananchi tulio wengi,

Tuweke maslahi ya walio wengi mbele sio kumfurahisha mtu au kikundi cha wachache.

"Vita ya Tembo ziymiazo ni nyasi"
 
Kwa wabunge wa Ccm wasio jua kilicho wapeleka bungeni watapinga hiyo hoja. Hawa wabunge wa Ccm ni wanafiki na wako bungeni kwa maslahi ya chama chao na ukandamizaji kwa jamii. Sheria zote kandamizi wabunge wa Ccm ndio huzipitisha. Slow learners. Baadae ndio huja kuona wamepitisha utumbo.
 
Back
Top Bottom