Bunge kuwaka moto, Kambi Rasmi ya Upinzani Kufutwa?

Kuna hali ambayo inaelekea kukupoteza nguvu chama cha siasa cha cdm
baada ya kunyimwa nguvu za kuongoza kambi ya upinzani bungeni
mopka sasa chacha kinatembelea kwenye wheelchair kina hali mbaya:llama::llama:


any source?

if not, this is the best crap of the week
 
Kwa mujibu wa kanuni za sasa, wabunge walio nje ya kambi rasmi ya upinzani bungeni hawaruhusiwa kuingia na kuongoza kamati za kudumu za usimamizi wa fedha ambazo ni za mashirika ya umma, serikali na mitaa na ile ya hesabu za serikali.

Baada ya mabadiliko hayo kamati hizo tatu za kudumu za Bunge nafasi zake zitagombewa na vyama vyote vya upinzani.

My take:

Kama nafasi hizo zitagombewa bado Chadema wana nafasi kubwa ya kuzichukua kwa vile wako wengi ukilinganisha na vyama vingine vya upinzani.

Hata hivyo sioni sababu ya Chadema kuwa na wasiwasi kwa vile bado kiongozi wa upinzani ana nafasi kubwa ya kumwajibisha M/kiti yeyote wa kamati atakayekwenda kinyume na maazimio ya kambi.

Binafsi nafikiri ni mabadiliko mazuri tu kama yamefanywa kwa kuzingatia faida ya wananchi na si kuwanufaisha wachache wenye uchu wa madaraka.

Faida ya wananchi wapi mkuu? toka lini (mda mrefu sana) umesikia ccm wamefanya maamuzi kwa kuzingatia maslahi ya umma wa watanzani?? wao wanaangali maslahi yao na namna ya kuendelea kubaki madarakani hata kama kwa kuvuruga amani kama wanavofanya sasa na agenda yao ya UDINI.

Mi nasema cdm wawe macho na wasikubali upuuzi wa aina yoyote kwani waao ndo tegemeo pekee lilibaki kwa watanzania maskini walio wengi hata kama hao watanzani hawwalijui hilo.
 
Kuna hali ambayo inaelekea kukupoteza nguvu chama cha siasa cha cdm
baada ya kunyimwa nguvu za kuongoza kambi ya upinzani bungeni
mopka sasa chacha kinatembelea kwenye wheelchair kina hali mbaya:llama::llama:
Kwani kuibua UFISADI kunahitaji kanuni..........???? HIVI NGUVU YA CDM ILIPATIKANA WAPI...........??? Ilikopatia nguvu CDM itaendelea kuzipata hizo nguvu huko huko...............
 
Si Mnyika pekee........... Tumenyukwa wote na DOWANS, na tumefulia wote na EPA, tumekapwa wote na RICHMOND, tumekwetekwa wote na MEREMETA, tumesekwa wote na MAFISADI, tumepindwa wote na KIWIRA, tumefanywa makinda wote na BUZWAGI, tumesitishwa wote na MIKATABA HATARI, tumefungwa makamba wote na ALIYEANZISHA ISHU YA UDINI, tumelowasika wote na KUJILIMBIKIZIA MALI, tumesisiemishwa wote KUUZA LOLIONDO, etc.................etc...............etc


hapo ndo utajua nguvu ya serikali
sisi hatutaki vurugu za katiba mpya mara dowans mara blah blah.....

pole mnyika
 
Tunashukuru kwa taarifa vipi hizo kamati zimesha chaguliwa kulingana na kanuni zilizo badilishwa na je uchaguzi wa wenyeviti wa hizo kamati huchaguliwa ndani ya kambi ya upinzani au kwa wabuge wote kutia ndani wa ccm
naomba kujuzwa
Wenyeviti watachaguliwa kwa kupigiwa kura chini ya kiongozi wa kambi ya upinzani bila kuwashirikisha wabunge wa CCM.
 
Katika hali ambayo tulitegemea watanzania walio wengi baada Raisi kutoa muongozo wake kuhusu katiba mpya

hatimaye mnyika kanyukwa
kafulila kafulia :msela::msela:

Hivi wewe ni Mtanzania kweli? Kama ni mtanzania basi utakuwa na mtindio wa ubongo na kama huna mtindio basi umetumwa na akina RA au ELyaani wewe KICHEFUCHEFU
 
wandugu, mpaka muda huu kuanzia saa nane mchana leo tarehe 07/02/2011 Spika wa bunge kwa kutumia kanuni za Bunge ambazo zinampa mamlaka ya kuunda kamati ya kanuni za Bunge na hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 115 (3) imempa mamlaka ya kuteua kamati ya kanuni za Bunge na kanuni hiyo imetamka kuwa yeye ndio atakuwa mwenyekiti, yaani anateua kisha anaongoza !

kutokana na hilo leo ameteua kamati hiyo na mpaka sasa wapo kwenye kikao , lengo ni kuhakikisha kuwa wanafuta neno kambi rasmi ya upinzani Bungeni ---ili eti kuwe na kambi ya upinzani ili kila mmoja aweze kuunda kambi.

Ubishi ni mkubwa sana kwani hata sheria iliyounda bunge inatambua uwepo wa kambi rasmi , ila wanaendeleza Ubabe.

upande mwingine anafanyia kazi barua ya CUF iliyoandikwa kwa spika decemba 13 ,2010 wakimtaka spika kufuta neno kambi rasmi .

lengo lingine ni kuhakikisha kuwa zile kamatio za bunge za kusimamia matumizi ya fedha za umma wanapewa watu wao kama ifuatavyo;
1. Mashirika ya umma (POC) - Hamad Rashid
2.Fedha za serikali (PAC) John Cheyo.
3. Serikali za Mitaa (LAC) -David Kafulila ... ila huyu bado hawajakubaliana naye kwani wamempa sharti ambalo anapaswa kulitimiza kwanza kuhusu hoja yake juu ya dowans.

Hivyo kama mapendekezo yakienda kama ambavyo wanataka ni kuwa sasa bungeni kutakuwa ama na kambi mbili za upinzani ama kusiwepo na kambi ya upinzani kabisa.

Nitawaletea taarifa zaidi pindi kikao kikimalizika, waliopo humo ni pamoja na Hamad Rashid, Anna Makinda, Job Ndugai, Tundu Lissu, Mustafa Akoonay,Freeman Mbowe, Andrew Chenge,George Simbachawene, Nimrod Mkono etc.

Nitawajuza zaidi hapo baadaye , kwani bado kikao kinaendelea .

hii ndio kazi ya kwanza ya Anna Makinda akiwa spika , je? inaashiria jambo gani?
Bunge hili litaenda ama ni malumbano kila kukicha?
Kwanini wanaihafia CHADEMA?
Je? wanataka tuwe kama zanzibar ambako waliondoa kambi rasmi ya upinzani kwenye baraza la wawakilishi?

once a Traitor always Traitor!
Umeajiriwa kufanya hilo shame on you! Bunge ni chombo cha kuheshimiwa kwa nini wanaajiri wasaliti kama wewe? maadili ya utumishi yako wapi? je kila mtu akitoa taarifa za kazini kwake humu hii itakua forum ya great thinkers kweli? shame on you! najua kuna watu wa aina yako wataanza kuporomosha matusi ila to this is real immoral!
 
Nitafurahi kama kweli ccm na cuf wakifuta neno kambi rasmi bungeni. Nitafurahi sana! Kama chadema hawana uchu wa kugawana madaraka, nategemea nao wafurahi. CCM na CUF wakifanya hivyo, watakuwa wamethibitishia umma hisia kwamba Bunge na Serikali havipo kwa maslahi ya wananchi bali kwa maslahi ya viongozi. Hapo ndipo Chadema wanatakiwa kurudi kwa wananchi na kujiimarisha, kutumia nguvu ya umma kuwaondoa hao wakoloni madarakani (serikali na wabunge)
 
Tunaomba update mlio karibu na Tv kuhusu yanayo endelea huko bungeni leo
 
Wakuu wenye kanuni za bunge tunaomba mtu wekee hapa hasa kwenye kanuni za huwepo na kambi ya upinzani nafikiri ingekuwa vema na sisi tukazijua then tuwe rahisi kutoa maelezo na mikakati mapema inaonekana CUF NA CCM WALIJIPANGA MAPEMA NDIYO SABABU WAKAINDIKIA OFISI YA BUNGE MAPENDEKEZO YA KUFUTA KIPENGELE CHA KAMBI RASMI

NA NIONAVYO MIMI INAONEKANA CCM WATATUMIA KANUNI KUIDHOOFISHA CDM NI VEMA TUKAZIPATA HIZO KANUNI ZA BUNGE NA SISI TUZIJUE TUONE TUNAWEZA KUSAIDIAJE

Ni maoni yangu wana JF
 
Mama Makinda alisha wahi kusema na kunukuliwa na vyomba vya habari kadhaa kwamba Bunge lake litakuwa bunge la kujali maslahi ya wananchi... na kwa haya yanayolipotiwa sijui maslahi ya wananchi yako wapi kwa kuwa au kutokuwa na Kambi rasmi ya upinzani...

Nime-conclude... she is a total hyprocite and opportunist kwa kubadirisha kanuni ambazo walijiwekea wenyewe katika mabunge yaliyopita na kanuni hizo Kuendelea kutumika hata katika Bunge la 9... kuna umuhimu gani kuzibadili kanuni kwa sasa? kwa nini wasime tu ok tutabadili kanuni hizi na zitakuwa effective katika Bunge la 11 na sio hili la kumi maana wakati wanafanya kampeni na wakati wanachaguliwa wabunge hawa walizifahamu kanuni hizi na sikusikia hata mmjoa wao akizipigia kelele kwamba hazikuwa fair... iweje leo baada ya uchaguzi waseme kwamba tunataka upinzani wa wote...

Tangu lini mtu akalazimishwa kupatana na mtu ambaye amekwisha weka msimo wake waziwazi kwamba CUF WAMO SERIKALINI na wanawapigia kura miswaada yote ya ccm ili GVU iweze kuwaendelea ulaji na kwa NINI CUF watake kuonana na kila Chama...? Kwani kuoana na CCM haitoshi mpaka wote yaani CDM, CUF ,TLP NCCR wajiunge pamoja ndio kitaeleweka? mbona mambo haya ya kuungana hawakuyafanya kabla ya uchaguzi?

Nafikiri mtu mwenye kuchanganya akili zake na za kupewa atajua tu kwamba CUF wako kimaslahi zaidi na wajue wahenga walisema mtaka yote kwa PUPA....WATAMALIZIA NA KUJIJUA...
 
Bunge hili ni usanii mtupu hakutakuwa na chochote cha maana zaidi ya usanii. Wanaostahili kuunda kambi ya upinzani ni CHADEMA lakini huyo mama wa chama cha mafisadi ameamua kutumia ufisadi ili kuwapora CHADEMA haki yao baada ya kupata viti vingi kuliko chama kingine chochote kile.

Spika aliyewekwa na Rostam, Chenge, Chiligati, Makamba, JK na rafiki yake Lowassa - sisi watanzania tunajua kila kitu. haka ka mama katatumiwa kupitisha ufisadi wote na ndiyo maana Mijadala ya maana haijadiliwi. Watanzania tuna safari ndefu sana - ee mwenyezi mungu tusaidie.
 
Bunge laanza kukata makali ya Chadema

Monday, 07 February 2011

f.mboye.jpg

Kiongozi wa Upinzani bungeni, Freeman Mbowe

Waandishi Wetu, Dodoma

KAMATI ya Kanuni ya Bunge jana iliridhia mabadiliko ya kanuni kwa kufanya kambi rasmi ya upinzani kubeba vyama vyote na sio Chadema pekee.

Hatua hiyo ya Kamati ya Kanuni tayari imelalamikiwa na Chadema kwamba ina lengo la kukidhofisha chama hicho.


Katika kikao leo Bunge leo linatarajia kufanya marekebisho ya baadhi ya kanuni ikiwamo ya tafsiri mpya ya kambi rasmi ya upinzani.


Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Kamati ya Kanuni ambayo pia Kiongozi wa Upinzani bungeni, Freeman Mbowe alihudhuria baada ya mabadiliko hayo, kamati zote za kudumu za usimamizi wa fedha zitagombewa na vyama vyote vya upinzani.


Lakini, jana Mkurugenzi wa Masuala ya Bunge na Halmashauri ya Chadema, John Mrema wamepokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda inayoeleza nia ya Bunge kuondoa neno kambi rasmi ya upinzani bungeni ili kufanyia marekebisho.


"Tumepata taarifa kuwa Spika wa Bunge kwa kutumia nyongeza ya (8) ya kanuni chini ya kanuni ya 115 "kamati za kudumu zisizo za sekta" kifungu cha 3 (1) kinachompa mamlaka ya kuunda Kamati ya kubadili Kanuni za Bunge aliunda kamati hiyo yenye lengo la kufanya marekebisho ya Kanuni za Bunge,"alisema Mrema.


Mrema alisema Chadema kimegundua kuwa miongoni mwa sababu za kuundwa kwa kamati hiyo ni kutaka kufanyia mabadiliko kipengele hicho ambacho kitapunguza nguvu ya upinzani bungeni na zaidi nguvu ya Chadema ambacho ndicho chama chenye sifa za kusimamia na kuhoji Serikali.


Alisema kwa mujibu wa utamaduni wa mabunge ya Jumuiya za Madola, chama kikuu cha upinzani ndicho chama mbadala wa chama tawala na kina sifa za kusimamia na kuhoji Serikali juu ya mambo mbalimbali hasa kwenye kamati tatu za Bunge zinaofahamika kama Kamati za Kudumu za Bunge.


Kwa mujibu wa kanuni za sasa, wabunge walio nje ya kambi rasmi ya upinzani bungeni hawaruhusiwa kuingia na kuongoza kamati hizo tatu za Bunge ambazo ni za mashirika ya umma, serikali na mitaa na ile ya hesabu za serikali.


"Mara baada ya Uchaguzi Mkuu kumalizika wa mwaka 2010, Chadema tulipata wabunge wengi ambao walikiwezesha chama kuwa na haki ya kuweza kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa mujibu wa Kanuni za Bunge kifungu cha 14 kifungu kidogo cha 3,"alisema Mrema.


Mrema alifafanua kuwa mabadiliko hayo ya kanuni yanafuatia barua ilioyoandikwa na vyama vingine vya upinzani vikiongozwa na CUF kwenda kwa Spika na kutaka neno kambi rasmi ya upinzani bungeni lifutwe.


Alisema lengo la vyama hivyo ambavyo kwa sasa havikuwa na sifa ya kuunda kambi ya upinzani bungeni na havikushirikishwa kwenye kambi iliyoundwa na Chadema ni kutaka kuwa na haki ya kuunda umoja wao unaojulikana kama minority camp.



Wakati chama hicho kikitoa maelezo yake hayo habari za uhakika zilizopatikana kutoka ndani ya vikao vya vyama vya siasa na kuthibitishwa na baadhi ya wabunge zilisema kuwa moja ya kanuni zitakazorekebishwa ni ile inayotambua uwepo wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.


Kanuni hiyo inatoa nafasi kwa chama cha upinzani kinachofikisha asilimia 12.6 ya wabunge kuwa kambi rasmi ya upinzani ambapo kwa sasa ni Chadema yenye wabunge takribani 70.


Hali hiyo iliviacha kando vyama vingine vya CUF, NCCR, TLP, UDP vyenye wabunge wachache vikilalamika kutoshirikishwa katika kambi hiyo hivyo kuzua mvutano vikiitana kuwa na kambi yake ndogo ya upinzani.


Iwapo mabadiliko hayo yatatokea vyama vya upinzani vitakuwa vimefungishwa 'ndoa' ya lazima baada ya kulumbana kuhusu nafasi ya kambi yao.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/9105-bunge-laanza-kukata-makali-ya-chadema#
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom