Bunge kuwa Upande wa Serikali ni lazima ili tuendelee!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Hakuna nchi iliyowahi kuendelea kwa hivi vyombo viwili kutofautiana, hivyo basi ili nchi yetu itoboe na kuendelea ni lazima Bunge na Serikali viimbe wimbo mmoja na siyo kinyume chake kama baadhi wanavyojaribu kutudanganya!

Nchi zilizoendela ndiyo zina hayo mambo ya Bunge kutofautiana na Serikali na kuleta mitafaruko lkn wao walishaendelea, hivyo huku chini ni lazima Bunge na Serikali viende pamoja na nafikiri Raisi Magufuli ameshalitambua hilo rejea Hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge, ili mambo yaende fasta Serikali inahitaji Bunge lililo upande wake, na hili ni muhimu na ningeshauri yoyote atakayejaribu kukwamisha hili abomolewe kwa faida ya Tanzania!
 
Kwahoja yako ni kwamba leo Lowasa asingeitwa fisadi na wale mawaziri wote waliojiuzuru enzi za JK wangekuwa wasafi?
 
Hakuna nchi iliyowahi kuendelea kwa hivi vyombo viwili kutofautiana, hivyo basi ili nchi yetu itoboe na kuendelea ni lazima Bunge na Serikali viimbe wimbo mmoja na siyo kinyume chake kama baadhi wanavyojaribu kutudanganya!

Nchi zilizoendela ndiyo zina hayo mambo ya Bunge kutofautiana na Serikali na kuleta mitafaruko lkn wao walishaendelea, hivyo huku chini ni lazima Bunge na Serikali viende pamoja na nafikiri Raisi Magufuli ameshalitambua hilo rejea Hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge, ili mambo yaende fasta Serikali inahitaji Bunge lililo upande wake, na hili ni muhimu na ningeshauri yoyote atakayejaribu kukwamisha hili abomolewe kwa faida ya Tanzania!
Bunge lina majukumu yake na Serikali vivyo hivyo,bila kusahau Mahakama. Hawa wanashirikiana,ila sii mmoja kuwa koloni la mwenzake. Huo ni UPUMBAVU WA MWISHO! Bunge halipaswi kabisa kuwa upande wa Serikali au hata Mahakama, kila muhimili Usimame katika majukumu yake.
Tukitaka kurudi enzi za Ujima ni kuruhusu mawazo haya ya ki ccm yapate nafasi katika nchi!
Nchi zote zilizoendelea duniani ni kutokana na Uimara wa Bunge unaopelekea Serikali Kuwajibika.
Hapa kwetu Bunge linajiona ni sehemu ya serikali, very wrong! Ndio maana Magufuli kakuta madudu, na atakaemfuatia nae atakuta madudu, hii yote kwa sababu Bunge limehama kwenye nafasi yake
 
Huwo ni mfumo wa Ulaya na nchi zilizoendelea ndiyo kuna hayo mambo lkn nchi zote wkt ziko kwenye ngazi ya kimaendeleo kama tuliyonayo sisi leo hii hata Ulaya kwenyewe Bunge na Serikali zilikuwa pamoja, na hili Wazungu wamekuja kulibadilsha juzi tu baada ya kuendelea lkn kabla ya hapo ilikuwa ni kama Uchina na kwanza ndiyo maana unaona kuna tofauti kubwa ya kimaendeleo kati ya Uchina na India, Wahindi wao walikosea stepu wakachukuwa mambo ya kizungu kabla ya kuendelea matokeo yake ndiyo hayo, wanaachwa mbali sana na Uchina!
 
Hayo maendeleo mbona hayajafanyika miaka yote ambapo tulikuwa na chama kimoja na yaliyo kuwa yakisemwa na serikali ndo hayo yaliyosemwa bungeni
 
Huwo ni mfumo wa Ulaya na nchi zilizoendelea ndiyo kuna hayo mambo lkn nchi zote wkt ziko kwenye ngazi ya kimaendeleo kama tuliyonayo sisi leo hii hata Ulaya kwenyewe Bunge na Serikali zilikuwa pamoja, na hili Wazungu wamekuja kulibadilsha juzi tu baada ya kuendelea lkn kabla ya hapo ilikuwa ni kama Uchina na kwanza ndiyo maana unaona kuna tofauti kubwa ya kimaendeleo kati ya Uchina na India, Wahindi wao walikosea stepu wakachukuwa mambo ya kizungu kabla ya kuendelea matokeo yake ndiyo hayo, wanaachwa mbali sana na Uchina!

Kwa miaka 31 tz imetawaliwa na chama kimoja tuambie hayo maendeleo tuliyoyapata
 
Hakuna nchi iliyowahi kuendelea kwa hivi vyombo viwili kutofautiana, hivyo basi ili nchi yetu itoboe na kuendelea ni lazima Bunge na Serikali viimbe wimbo mmoja na siyo kinyume chake kama baadhi wanavyojaribu kutudanganya!

Nchi zilizoendela ndiyo zina hayo mambo ya Bunge kutofautiana na Serikali na kuleta mitafaruko lkn wao walishaendelea, hivyo huku chini ni lazima Bunge na Serikali viende pamoja na nafikiri Raisi Magufuli ameshalitambua hilo rejea Hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge, ili mambo yaende fasta Serikali inahitaji Bunge lililo upande wake, na hili ni muhimu na ningeshauri yoyote atakayejaribu kukwamisha hili abomolewe kwa faida ya Tanzania!

Ninailaani ccm kwa kuua elimu
 
Hata kama ni kuusaka ukuu wa wilaya kwa nguvu huwezi leta hoja kipuuzi kama hii. Hawa vijana 44 waliobaki kati ya 46 walioombewa ajira na JK wanaweza hata kutembea uchi kama itawasadia kupata UDC. Kwa taarifa yako wewe pimbi bunge ni muhimili unaojitegemea unatakiwa kuirekebisha serikali ikikosea. Magufuli na binadamu ana mapungufu tusimuache atuamulie kila kitu tuko milioni 45
 
Hakuna nchi iliyowahi kuendelea kwa hivi vyombo viwili kutofautiana, hivyo basi ili nchi yetu itoboe na kuendelea ni lazima Bunge na Serikali viimbe wimbo mmoja na siyo kinyume chake kama baadhi wanavyojaribu kutudanganya!

Nchi zilizoendela ndiyo zina hayo mambo ya Bunge kutofautiana na Serikali na kuleta mitafaruko lkn wao walishaendelea, hivyo huku chini ni lazima Bunge na Serikali viende pamoja na nafikiri Raisi Magufuli ameshalitambua hilo rejea Hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge, ili mambo yaende fasta Serikali inahitaji Bunge lililo upande wake, na hili ni muhimu na ningeshauri yoyote atakayejaribu kukwamisha hili abomolewe kwa faida ya Tanzania!

Naamini ulikuwa na point nzuri sana uliyotaka kutueleza. Ila namna ulivyoileta inafanya sisi wasomaji wako tujiulize maswali mengi. Swali la kwamba ambalo mimi nimejiuliza ni Kwamba, Hivi Mleta mada unajua majukumu ya Bunge, Serikali na Mahakama? Pili hivi kweli unafahamu unaishi wakati gani? na mengine mengi.

Ujumbe uliojificha kwenye mada yako ni kuhusu Wapinzani kuprotest hoja za serikali wasizokubaliana nazo kwa kutoka nje. Hata mimi hili linanifanya nihoji credibility wa wabunge wetu wa upinzani. Kutoka nje siyo njia sahihi ya kupata suluhu ya kile wasichotaka kifanyike au siyo suluhu ya matatizo. Nadhani hii tabia ya wabunge wetu wa upinza ya kutoka nje ya bunge imefanya hata serikali ishindwe kusikiliza hoja zao na kuwachukulia hao ndivyo walivyo. Hata sisi wananchi huku nje tunawaona kama watoto. Mfano mdogo wa jinsi gani wabunge wetu wa Upinzani wanajidharaulisha na Serikali kuwapuuza kwa vitendo vyao vya kila mara kutoka nje ya ukumbi wa bunge, unaweza kufananishwa na mtoto kwenye familia yeye kila analoambia ni kulia tu. Wazazi mwishowe wanamchukulia huyo ndivyo alivyo, muache alie akichoka atanyamaza.
Wabunge wetu wa upinzani badilikeni.. It is too much kila wakati mnatoka nje lakini wabunge wa CCM wanaendelea na vikao na hoja zinapita na nyie hamfanyi lolote tena. It is useless kuprotest kila mara kusiko leta matunda chanya.

NB: Mwandishi ungewakilisha point zako kwa uwazi tu siyo uzunguke.
Hata sisi wabunge wa upinzani wameisha tuchosha kuprotest kila siku kwa kutoka nje kusikokuwa na impact chanya yoyote
 
Hakuna nchi iliyowahi kuendelea kwa hivi vyombo viwili kutofautiana, hivyo basi ili nchi yetu itoboe na kuendelea ni lazima Bunge na Serikali viimbe wimbo mmoja na siyo kinyume chake kama baadhi wanavyojaribu kutudanganya!

Nchi zilizoendela ndiyo zina hayo mambo ya Bunge kutofautiana na Serikali na kuleta mitafaruko lkn wao walishaendelea, hivyo huku chini ni lazima Bunge na Serikali viende pamoja na nafikiri Raisi Magufuli ameshalitambua hilo rejea Hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge, ili mambo yaende fasta Serikali inahitaji Bunge lililo upande wake, na hili ni muhimu na ningeshauri yoyote atakayejaribu kukwamisha hili abomolewe kwa faida ya Tanzania!
Huu nao wendewazimu .nchi gani hiyo unayosema !!!!??
 
Wakati wa kuomba kura za Rais ...zilombwa kura za ubunge na udiwani pia
 
dahhhh akili zingine hizi...mhh
wacha ccm itawale milele,.bure wee jamaa
unajua kaz za bunge????????
 
Huwo ni mfumo wa Ulaya na nchi zilizoendelea ndiyo kuna hayo mambo lkn nchi zote wkt ziko kwenye ngazi ya kimaendeleo kama tuliyonayo sisi leo hii hata Ulaya kwenyewe Bunge na Serikali zilikuwa pamoja, na hili Wazungu wamekuja kulibadilsha juzi tu baada ya kuendelea lkn kabla ya hapo ilikuwa ni kama Uchina na kwanza ndiyo maana unaona kuna tofauti kubwa ya kimaendeleo kati ya Uchina na India, Wahindi wao walikosea stepu wakachukuwa mambo ya kizungu kabla ya kuendelea matokeo yake ndiyo hayo, wanaachwa mbali sana na Uchina!
Hoja zako nyingi unazitoa pasipo kufanya reference na Sheria mbalimbali zilizopo so in most cases ni very Irrelevant. Mfano ni hii hoja ambapo wewe una advocate Katiba ivunjwe kukidhi mahaba yako kwa chama chako. Kikatiba kamwe bunge haliwezi kufanya kazi za serikali coz kila mihimili una roles zake.
 
Back
Top Bottom