Bunge kutokuwa na Kambi rasmi ya Upinzani ni ishara kuwa Wapinzani wameishiwa pumzi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,603
141,421
Moja ya kipimo cha kuimarika kwa upinzani ni uwepo wa Kambi rasmi ya upinzani na mabaraza ya madiwani yanayoongozwa na vyama vya upinzani.

Kwa sasa hapa Tanzania hivyo vyote havipo. Ni kama vile tumerudi mwaka 1992 wakati mfumo wa sasa wa vyama vingi unaasisiwa.

Ili upinzani urejeshe makali yake ni lazima wapatikane viongozi aina ya mchungaji Mtikila au Mabere Marando ambao pamoja na misukosuko mingi waliyopitia hawajawahi kukimbilia ubalozi wa Ulaya ama kuvuka mipaka kinyemela huko Namanga, walipambana ndani ya nchi yao na huo ndio uzalendo.

Maendeleo hayana vyama!
 
Uimara wa wapinzani sio kushiriki hilo bunge kibogoyo, lililopatikana kwa umwagaji damu na wizi mkubwa wa Kura.
Wapinzani ni debe tupu! tuliwaambiaa hamkusikia! Kiufupi vumilieni tu! ,demokrasia sio lazima CHADEMA ishinde ,Wananchi wamewakataa kwenye kura jipangeni hadi 2025!.
 
Hapa unakiri wazi ukiwa mpinzani lazima ukumbwe na misukosuko mingi,unadhani kwanini?
Hao uliowataja kukumbwa na misukosuko,walipigwa risasa 16?Nakwambia,hata Dr Slaa kama awamu ile ya kikwete ndio ingekuwa sasa huenda angekuwa marehemu!
This guy is sick!
 
Kuna mambo kwa kiwango chako hutakiwi kuyasema hata kama umeyasikia kwenye kijiwe cha Kahawa hapo Mitunduruni. Hii thread inapswa kuanzishwa na kina Chagu na YEHODAYA siyo wewe. You are too high to utter this shallow minded thread.
 
Hapa unakiri wazi ukiwa mpinzani lazima ukumbwe na misukosuko mingi,unadhani kwanini?
Hao uliowataja kukumbwa na misukosuko,walipigwa risasa 16?Nakwambia,hata Dr Slaa kama awamu ile ya kikwete ndio ingekuwa sasa huenda angekuwa marehemu!
This guy is sick!
Misukosuko ni sehemu ya upinzani duniani kote bwashee.

Prof Lipumba aliwahi kuvunjwa mkono akiwa kwenye harakati za kisiasa.

Kama mgombea anaiogopa dola unategemea nini kwa wapiga kura wake?

Siasa za Tanzania ni za mdomoni zaidi!
 
Yaani umeshasema 'misukosuko' halafu unashangaa wapinzani kuwa ICU. Hapo ni mgonjwa wa goti kupasuliwa kichwa wakati yule wa kichwa kupasuliwa goti!
 
Back
Top Bottom