Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,279
- 25,857
Nikiwa kama mtanzania,nami najitokeza kuchangia katika mjadala wa kitaifa kama matangazo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yarushwe moja kwa moja au la. Zipo pande mbili katika mjadala huu. Upande unaopinga kurushwa moja kwa moja na ule unaounga mkono matangazo ya Bunge kurushwa moja kwa moja.
Mimi binafsi,kama mtanzania nisiye mwanachama wa chama chochote cha siasa hapa nchini na kwingineko,naunga mkono Bunge kurushwa moja kwa moja. Upande unaopinga unaoongozwa na viongozi wa Serikali na chama tawala-CCM una hoja zake. Waziri mhusika Nape Nnauye alizitaja Bungeni. Nazikumbuka mbili. Ya kwanza,ni kwamba TBC hawana bajeti ya kutosha kurusha moja kwa moja. Ya pili,Waziri Nape alisema kuwa wananchi wengi hawafuatilii matangazo hayo ya moja kwa moja. Ikasemwa kuwa wananchi huwa kwenye pilikapilika zao za kimaisha wakati Bunge likiendelea.
Upande unaounga mkono kurushwa matangazo hayo moja kwa moja unakosea jambo moja. Upande huo huuponda upande wa Waziri Nape badala ya kuujibu kwa hoja,kuusifu na kuuonyesha umuhimu wa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge. Binafsi,naamini kuwa Bunge ndiyo ukumbi au uwanja wa kuonyesha siasa kwa viongozi wa kisiasa. Bunge ni sehemu ya kujidai na kujitamba kama chama tawala na hata upinzani juu ya umahiri wa kujenga hoja na kuonyesha mafanikio.
Serikali hii inayotajwa kama inayofanya kazi na kuwajibika ipasavyo na hata kuupotezea hoja na nguvu upinzani,haina haja ya kuogopa kurushwa moja kwa moja na kutaka matangazo ya Bunge yahaririwe kwanza. Serikali na chama chake tawala ilipaswa kutamba live Bungeni na wananchi kushuhudia. Kama mambo yako vizuri na yanapendwa,uoga unatoka wapi?
Wa upande wetu tunapaswa kuwaelimisha wa upande ule na hata kuwasifu kwakuwa bila hayo hatutafanikiwa. Bunge litumike vyema huku likionekana kujenga,kujibu na kuwasilisha hoja za Serikali na chama tawala na hata upinzani. Hakuna haja ya wapiganaji kuukimbia ulingo.