Bunge Kupokea Maoni ya Wadau Kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Fedha wa Mwaka 2022

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,799
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imepanga kupokea maoni ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Fedha wa Mwaka 2022.

Mkutano wa kupokea na kusiikiliza maoni ya wadau utafanyika siku ya Jumanne tarehe 20 Septemba, 2022 saa 4:00 asubuhi katika ukumbi wa Pius Msekwa, Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma.

Kamati inawaalika watu wote wenye maoni kuhusu muswada huo kufika na kuwasilisha maoni yao kabla haujapelekwa hatua nyingine.

photo_2022-09-19_14-05-01.jpg
 
Mbona wanashtukiza hivi?

Wadau watawezaje kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutoa maoni?
 
Yaani wanapitisha wenyewe sheria za kiouuzi, halafu wanataka tena watu wajitokeze kutoa maoni!!! Hovyo kabida. Mimi siwezi kujitokeza kwenye upuuzi kama huo.
 
Cha ajabu watajazwa Makada waliovalia kiraia hapo ndio mambo yanapoharibika.

Kila kitu kinafanywa siasa Nchini Puerto Rico.
 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imepanga kupokea maoni ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Fedha wa Mwaka 2022.

Mkutano wa kupokea na kusiikiliza maoni ya wadau utafanyika siku ya Jumanne tarehe 20 Septemba, 2022 saa 4:00 asubuhi katika ukumbi wa Pius Msekwa, Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma.

Kamati inawaalika watu wote wenye maoni kuhusu muswada huo kufika na kuwasilisha maoni yao kabla haujapelekwa hatua nyingine.

View attachment 2361604
Tozo kufutwa
 
Back
Top Bottom