Bunge kupitisha maamuzi yake kwa kupima sauti si sawa katika zama hizi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge kupitisha maamuzi yake kwa kupima sauti si sawa katika zama hizi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tetere Enjiwa, Aug 30, 2011.

 1. T

  Tetere Enjiwa JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 217
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wote tumeshuhudia maumuzi ya mambo muhimu ya husuyo nchi yetu yananavyo pitishwa bungeni, kwa waheshimia Wabunge wetu kuulizwa wanao kubali waseme ndio na wanao wakataa waseme hapana. Mwisho wa siku anaachiwa muulizwa swali kuamua walio shinda. Siamini kuwa hii inaonyesha umakini wowote katika kuendesha bunge na hasa kufanya maaumuzi.

  Katika mfumo tulionao sasa wa vyama vyingi na tukizingatia mabadiliko ya sayansi na teknologia tunatakiwa kubadilisha mfumo wa upigaji kura za maaumuzi ya bunge ili kuliongezea heshima bunge letu mbele ya jamii. Naomba kuwakilisha.
   
 2. W

  We can JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na wewe kabisa. Kuna watu hawana sauti, au kama wanazo hukutwa hawajawasha 'mike' zao. Hata bila ya kigezo cha besi au sauti nyembamba, sauti kali au au ya chini, ni ngumu kwa Spika kujua watu waliokubali au kutataa ni wangapi hasa pale ambapo, waliokubali na waliokataa wanakaribiana au wako sawa ki-idadi.
   
Loading...