Bunge kupitisha azimio la kumpongeza Spika Ndugai na Serikali kutobadili Makao Makuu ya shughuli zake

Hakuna azimio lolote lenye maana hapo

Nakumbuka Upinzani iliposema hakukuwa na sheria ya kuhamishia makao makuu Dodoma. Tena kwa kudai sheria itungwe na bujeti iwekwe - wakaambiwa wanapinga. Leo tunataka kufanya azimio la kutorejesha makao makuu ya serikali Dar!! Sijui tafsiri yake ni nini kama sio azimio hili ndio litachukuliwa sheria ya kuhamisha makao makuu!!

Mambo ya maana yanakosa hata kujadiliwa - tunakuja na azimio la kupongeza!!
 
Huyu Ndugai atakuwa ameforce kupongezwa. Huu ni Uzwazwa. Yaani Bunge zima linaburuzwa kuazimia kumpongeza mtu? Kwa mafanikio yapi haswa?
 
Bunge la Tanzania leo linaendelea na shughuli zake katika Mkutano wa 19, Kikao cha 40 ambapo baadhi ya shughuli ni kupitisha maazimio mawili

Azimio la kwanza ni Kuitaka Serikali kutobadili Uamuzi wa Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi na Shughuli za Serikali

Azimio la pili ni Kumpongeza Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kwa mafanikio ya Bunge la 11

Azimio la kwanza la kuitaka Serikali kutobadili uamuzi wa Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu linakuja wakati ambao tayari shughuli nyingi za Serikali zimehamia Dodoma. Rais na Wizara zote tayari zimehamia Jijini Dodoma
Mmmh...
Makubwa...
Hili bunge ni sarakasi tupu
 
Back
Top Bottom