Bunge kupitia upya vipengele vya pensheni vinavyolalamikiwa

Papaeliopaulos

Senior Member
Feb 19, 2011
149
48
Mwanasheria mkuu wa serikali ametoa ufafanuzi bungeni kuhusu vipengele vya marekebisho ya mifuko ya pensheni vinavyolalamikiwa, na kuahidi kuwa ataleta tena hiyo hoja bungeni ili wabunge wavipitie Upya.
Aidha amesema serikali haina hila yeyote katika hilo na kuwa uwezekano wa kuvirekebisha au kuvirejesha kama zamani upo.
Yeye mwenyewe angeweza kuvirekebisha kitaalamu lakini ameona sio vyema afanye mwenyewe

Source: TBC Bunge
 
Hiyo sheria hawakufiria hata kidogo.... Kwa wafanyakazi wa serikali hilo wanatambua cku zote na hawana ndoto ya withdrawal benefit ila kwa secta binafsi hapo walichemka kutaka kutoa hiyo kitu.
 
hapo alitumia nywele kufikiri sio kichwa
 
Hiyo sheria hawakufiria hata kidogo.... Kwa wafanyakazi wa serikali hilo wanatambua cku zote na hawana ndoto ya withdrawal benefit ila kwa secta binafsi hapo walichemka kutaka kutoa hiyo kitu.

Hawakuaangalia huku sector binafsi kabisa!! Ukiwa serikalini una uhakika wa ajira mpaka kustaafu lkn huku kwetu tuna mikataba ya kuanzia miezi sita hadi miezi 60,sasa nikimaliza mkataba wangu ndio nisubiri kwa miaka 28 mizima khaaa!! Bora warudishe hilo fao la kujitoa!
 
Mwanasheria mkuu wa serikali ametoa ufafanuzi bungeni kuhusu vipengele vya marekebisho ya mifuko ya pensheni vinavyolalamikiwa, na kuahidi kuwa ataleta tena hiyo hoja bungeni ili wabunge wavipitie Upya.
Aidha amesema serikali haina hila yeyote katika hilo na kuwa uwezekano wa kuvirekebisha au kuvirejesha kama zamani upo.
Yeye mwenyewe angeweza kuvirekebisha kitaalamu lakini ameona sio vyema afanye mwenyewe

Source: TBC Bunge

Hii nayo kali ya aina yake, inamaana sheria aliyosaini Rais inarudi tena bungeni kama mswada ujadiliwe and then asaini tena. Ni kama walikuwa wanatikisa kiberiti vile
 
wakati wanaandaa na kuvipitisha walikuwa wamekunywa viroba kama anavyosema mh Job Ndugai

Wadau tusiwalaumu sana wabunge maana serikali ilifanya ujanja ujanja kupitisha hicho kipengele!! Tangia mwanzo wa mchakato hakikuwepo hadi iliposomwa mara ya pili hakikuwepo so wabunge wakajua hule muswada una mambo yaleyale!
 
....Ni kweli kabisa viroba ndivyo vilisema ndiooooo bila hata kusomwa na kujadiliwa!!!kweli lile ni jumba la usingizi na makofi tafadhali...."Ndioooo"""
 
bora kukawa na wabunge viti maalum "migodini"kuliko kuwa na viti maalum "vijana au UWT".
wamekaa tu kalala bungeni mpaka wafanyakazi wa migodini ndio wanaona mapungufu ya sheria. Shame on you mjengoni!
 
za mwizi kweli na daima arobaini. ina maana hawakuelewa mwanzo mpaka watu wapige kelele ndio wakubali. ikio la kufa halisikii dawa, wakiileta tena haitakuwa straight patakuwepo pa kulalamikia tu.
 
Hawakuaangalia huku sector binafsi kabisa!! Ukiwa serikalini una uhakika wa ajira mpaka kustaafu lkn huku kwetu tuna mikataba ya kuanzia miezi sita hadi miezi 60,sasa nikimaliza mkataba wangu ndio nisubiri kwa miaka 28 mizima khaaa!! Bora warudishe hilo fao la kujitoa!

Mie mwenyewe staili yangu ya mkataba mpya umeanza June halafu hawajaandika unaisha lini sasa hapo ni kukaa mkao wa kula. Hawa jamaa huko serikalini wamevimbisha matumbo wakijua na sie ni kama wao wakati madirector wanakuna vichwa biashara yao hailipi na muda wowote wanapiga chini investment.
 
Kuna utamaduni uliojengeka kwa muda mrefu kwa watumishi wa serikali kutokuwa makini wanapofanya au kuamua mambo mengi, Ukifanya kazi serikalini unatumia sehemu ndogo sana ya akili yako kutokana na mfumo na urasimu wa kipuuzi uliojengeka kwa muda mrefu. Wakati mwingine watumishi wengine wanatumia nafasi zao kutoa maamuzi ya kuumiza uma kwa sababu tu ya elimu na vyeti vyao vya kukariri (ref.mikataba mibovu, sheria mbovu zinazotungwa sasa hivi n.k.).
Matokeo yake, watumishi wengi hawatafuti suluhu ya matatizo kwa nafasi zao bali wanabaki wakilalamika tu. Si ajabu kuwasikia mwaziri au hata waziri mkuu akilalamikia tatizo badala ya kulishughulikia mara moja.
Mafisadi na viongozi wengine wabinafsi, wasio na utu wanatumia mwanya huo kupitisha maamuzi na sheria mbovu zisizojali maslahi ya wengi, wanachoangalia ni kama tu zitawanufaisha wao wenyewe!
Hatuhitaji elimu kubwa sana ya darasani kutatua haya, tunachohitaji ni kuchagua au kuteua watu wenye uwezo wa kufikiria na kutoa maamuzi kwa faida ya wote!
 
Mwanasheria mkuu wa serikali ametoa ufafanuzi bungeni kuhusu vipengele vya marekebisho ya mifuko ya pensheni vinavyolalamikiwa, na kuahidi kuwa ataleta tena hiyo hoja bungeni ili wabunge wavipitie Upya.
Aidha amesema serikali haina hila yeyote katika hilo na kuwa uwezekano wa kuvirekebisha au kuvirejesha kama zamani upo.
Yeye mwenyewe angeweza kuvirekebisha kitaalamu lakini ameona sio vyema afanye mwenyewe

Source: TBC Bunge

Hivi ndivyo Mwanasheria wetu anayetumia nywele kufikiri anavyotenda kazi kwamba angeweza kutunga (kurekebisha) sheria yeye pekee yake (autocratically), hivi amelewa mvinyo gani huyu, mbona ana kauli za ajabuajabu? Au ndiyo mwanasheria kada?
 
capitalit hawapendi serikali,kwani kazi yao ni kutumia tuu na kuchukua kwa nguvu jasho za watu.Capitalist huwa wanaangalia mara nyingi wapi pa kuzichukua hela zao toka serikalini hata kuwapa rushwa.Kwani watendani wengi wa serikali hawana kipya cha kuingiza hela.ndio maana wanaiba wanenda ficha kusiko, wanainvest katik biashara isiyo na faida mabayo capitalist angeingiza.
 
Back
Top Bottom