Bunge kumuomba radhi EL - Mpango huu ukifanikiwa!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
Mmoja wa wabunge waliotajwa kwenye taarifa ya Kamati Teule ya Bunge anatarajiwa kujibu hoja zilizoelekezwa kwake na Kamati hiyo kwa kuleta taarifa "tofauti" ya Richmond ambayo anaamini ndiyo iliyokuwa sahihi. Mbunge huyo anadai kuwa "kama kuna ripoti mbili za Richmond mbona moja haitutaji mimi na EL lakini hii nyingine inatutaja".

Mbunge huyo anatarajiwa kuja na utetezi huo hasa baada ya kutakiwa na Bunge kuelezea madai yake kuwa ripoti iliyosomwa Bungeni na Mwakyembe "siyo yenyewe imebadilishwa" akiashiria kwamba yeye mwenyewe alikuwa ameipata ripoti hiyo kabla ya kuletwa Bungeni na alijua kilichomo.

Baada ya kampeni ya kusafishana magazetini kuingia kasoro baada ya siri ya kuundwa kwa "Agenda 21 kuwekwa hadharani na sasa inaonekana wameamua kwenda moja kwa moja Bungeni. Kwa vile mpango wao huo nao unafunuliwa siku chache kabla ya kikao cha Bunge kukutana kuna uwezekano mbunge huyo kuamua kuomba radhi kwa kauli yake ya Bungeni na kuamua "kufa kisabuni".

Hadi hivi sasa, inadaiwa bado kuna mgongano mkubwa kati ya viongozi wa CCM kiasi kwamba baadhi ya viongozi wa juu hawakuzungumza kwenye mkutano wao Richmond. Kama kampeni hiyo ya kumsafisha EL na Mbunge huyo itafanikiwa na kama itaonekana kuwa ripoti iliyosomwa Bungeni siyo "yenyewe" basi kuna wezekano wa Bunge kumuomba radhi Lowassa na Mbunge huyo.

Hata hivyo, kwa upande wao wajumbe wa kamati teule na wenyewe inasadikiwa kuwa wamejipanga vizuri kujibu mashambulizi yoyote dhidi yao na imesemwa kuwa Mbunge huyo anayetaka kuja na "ripoti nyingine" ya Richmond ajiandae kupata kibano cha kukumbukwa.

Wakati huo huo,
uongozi wa Chama cha CUF kinatarajiwa kukutana kesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kuelezea msimamo wao baada ya kusikia maelezo ya CCM kuhusu muafaka. Kuna dalili kuwa chama hicho kitatoa muda maalum kwa serikali ya Rais Kikwete na baada ya hapo kuanza kuingia "mitaani" kwa njia ya maandamano. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika saa nane mchana saa za Afrika ya Mashariki.
 
mkuu

sijafahamu bado hii khabari.

pia naona neno WAKATI HUO HUO umelirejea zaidi ya mara moja.

any way WEEKEND NJEMA.
 
Chama cha Wananchi (CUF) kinatarajiwa kutoa tamko lao kuhusu msimamo wa chama hicho kuhusu majadiliano ya muafaka kati yake na Chama cha Mapinduzi. CUF wanatarajiwa kutoa tamko na maelekezo kwa wanachama wake kuanzia saa 8 mchana kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar-es-Saalam.

Wakati huo huo, mmoja wa wabunge waliotajwa kwenye taarifa ya Kamati Teule ya Bunge anatarajiwa kujibu hoja zilizoelekezwa kwake na Kamati hiyo kwa kuleta taarifa "tofauti" ya Richmond ambayo anaamini ndiyo iliyokuwa sahihi. Mbunge huyo anadai kuwa "kama kuna ripoti mbili za Richmond mbona moja haitutaji mimi na EL lakini hii nyingine inatutaja".

Mbunge huyo anatarajiwa kuja na utetezi huo hasa baada ya kutakiwa na Bunge kuelezea madai yake kuwa ripoti iliyosomwa Bungeni na Mwakyembe "siyo yenyewe imebadilishwa" akiashiria kwamba yeye mwenyewe alikuwa ameipata ripoti hiyo kabla ya kuletwa Bungeni na alijua kilichomo.

Baada ya kampeni ya kusafishana magazetini kuingia kasoro baada ya siri ya kuundwa kwa "Agenda 21 kuwekwa hadharani na wenu mtiifu na sasa inaonekana wameamua kwenda moja kwa moja Bungeni. Kwa vile mpango wao huo nao unafunuliwa siku chache kabla ya kikao cha Bunge kukutana kuna uwezekano mbunge huyo kuamua kuomba radhi na kuamua "kufa kisabuni".

Hadi hivi sasa, inadaiwa bado kuna mgongano mkubwa kati ya viongozi wa CCM kiasi kwamba baadhi ya viongozi wa juu hawakuzungumza kwenye mkutano wao Richmond. Mojawapo ya vitu ambavyo vinahofiwa kutokea huko mbeleni ni uwezekano wa Bunge kumuomba radhi Lowassa kama kampeni ya Mbunge huyo kijana itafanikiwa.

Wakati huo huo, uongozi wa Chama cha CUF kinatarajiwa kukutana kesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kuelezea msimamo wao baada ya kusikia maelezo ya CCM kuhusu muafaka. Kuna dalili kuwa chama hicho kitatoa muda maalum kwa serikali ya Rais Kikwete na baada ya hapo kuanza kuingia "mitaani" kwa njia ya maandamano. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika saa nane mchana saa za Afrika ya Mashariki.

Mkuu naona umeandika habari mbili zinazohitaji kujitegemea kwa zote zina uzito kivyake.Pili habari ya uwezekano wa EL kuombwa msamaha na bunge haiko plain kwangu sijui wenzangu may be I'm slow.Ila nachotaka ufafanuzi ni nini kiko kwenye hivyo ripoti nyingine ambayo haikuwakilishwa?,na je hii nyingine iliyosomwa si sahihi au?pili kunasehemu unasema MBUNGE huyu inawezekana kuomba msamaha na sehemu nyingine BUNGE kuomba msamaha.Tafadhali sherehesha habari hii iwe uchi maana kuwa kwangu slow naona labda ugeni wangu hapa kwa kuwa naona kama kuna sehemu unarejea bambiko lako la nyuma.
Natanguliza shukrani zangu.
 
Baada ya kampeni ya kusafishana magazetini kuingia kasoro baada ya siri ya kuundwa kwa "Agenda 21 kuwekwa hadharani na wenu mtiifu na sasa inaonekana wameamua kwenda moja kwa moja Bungeni. Kwa vile mpango wao huo nao unafunuliwa siku chache kabla ya kikao cha Bunge kukutana kuna uwezekano mbunge huyo kuamua kuomba radhi na kuamua "kufa kisabuni".
Sometime ni muhimu kujifagilia, na hasa pale unapoona watu wanachelewa kukufagilia..
 
haijakaa vizuri, hii iende kwenye nyepesi nyepesi, nothing supports it ! haina kichwa wala miguu ! nahisi, nahisi, nahisi kibaoooooooooo ! imetungwa hii bana !
 
Ilikuwa ni habari mbili tofauti... hiyo ya CUF iko tayari kwenye News.. hii ya ya mpango wa Mbunge we'll be seen in few days.. labda nimeiwahisha.... katika sehemu ya mapambano yale yale ya fikra. ...
 
Mutu,

Kwanza karibu sana JF

Nakubalina nawe kuwa hii habari haijakaa vizuri kueleweka
Mwankijiji....huko kuomba msamaha sijui mbunge/Bunge ndio kuko vipi vipi
 
Nafikiri itakuwa Vizuri kwa RA kuja na Ripoti nyingine maana tunaweza kutapa ka sherehe kengine kutokea bungeni.

Na pia watanzania tulio na hasira za kumlipa kila mwezi kutoka kwenye kamshahara ketu tunaweza kupata chanzo sasa cha kuomba kuturudishia pesa zetu zikiwa na riba.
 
Mutu,

Kwanza karibu sana JF

Nakubalina nawe kuwa hii habari haijakaa vizuri kueleweka
Mwankijiji....huko kuomba msamaha sijui mbunge/Bunge ndio kuko vipi vipi

Aksante! tupo pamoja ndugu
 
Mmoja wa wabunge waliotajwa kwenye taarifa ya Kamati Teule ya Bunge anatarajiwa kujibu hoja zilizoelekezwa kwake na Kamati hiyo kwa kuleta taarifa "tofauti" ya Richmond ambayo anaamini ndiyo iliyokuwa sahihi. Mbunge huyo anadai kuwa "kama kuna ripoti mbili za Richmond mbona moja haitutaji mimi na EL lakini hii nyingine inatutaja".

Mbunge huyo anatarajiwa kuja na utetezi huo hasa baada ya kutakiwa na Bunge kuelezea madai yake kuwa ripoti iliyosomwa Bungeni na Mwakyembe "siyo yenyewe imebadilishwa" akiashiria kwamba yeye mwenyewe alikuwa ameipata ripoti hiyo kabla ya kuletwa Bungeni na alijua kilichomo.

Baada ya kampeni ya kusafishana magazetini kuingia kasoro baada ya siri ya kuundwa kwa "Agenda 21 kuwekwa hadharani na sasa inaonekana wameamua kwenda moja kwa moja Bungeni. Kwa vile mpango wao huo nao unafunuliwa siku chache kabla ya kikao cha Bunge kukutana kuna uwezekano mbunge huyo kuamua kuomba radhi kwa kauli yake ya Bungeni na kuamua "kufa kisabuni".

Hadi hivi sasa, inadaiwa bado kuna mgongano mkubwa kati ya viongozi wa CCM kiasi kwamba baadhi ya viongozi wa juu hawakuzungumza kwenye mkutano wao Richmond. Kama kampeni hiyo ya kumsafisha EL na Mbunge huyo itafanikiwa na kama itaonekana kuwa ripoti iliyosomwa Bungeni siyo "yenyewe" basi kuna wezekano wa Bunge kumuomba radhi Lowassa na Mbunge huyo.

Hata hivyo, kwa upande wao wajumbe wa kamati teule na wenyewe inasadikiwa kuwa wamejipanga vizuri kujibu mashambulizi yoyote dhidi yao na imesemwa kuwa Mbunge huyo anayetaka kuja na "ripoti nyingine" ya Richmond ajiandae kupata kibano cha kukumbukwa.

Wakati huo huo,
uongozi wa Chama cha CUF kinatarajiwa kukutana kesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kuelezea msimamo wao baada ya kusikia maelezo ya CCM kuhusu muafaka. Kuna dalili kuwa chama hicho kitatoa muda maalum kwa serikali ya Rais Kikwete na baada ya hapo kuanza kuingia "mitaani" kwa njia ya maandamano. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika saa nane mchana saa za Afrika ya Mashariki.

Mkuu sasa unasomeka five clear!

Ila kwani kamati si ndio ilikuwa inafanya uchunguzi na mwenyekiti wa kamati ndio aliyesoma ripoti na kudhibitisha kwamba ndio ripoti ya kamati yake Bungeni.

KAMA ripoti ni tofauti basi ilitakiwa watoke wachumbe wa kamati waseme mwenyekiti ame submit na kusoma ripoti toauti na tuliyoiandaa kutokana na uchunguzi kama kamati si mtu nje ya kamati anaweza claim ripoti sio.

Na huyu mbunge alionaje ripoti kabla ya bunge kukabidhiwa ?"nachelea ya kuwa hilo ni kosa" alikuwa anatafuta nini kama si kuharibu uchunguzi.Na hata kama hiyo ripoti nyingine ni kweli ilikuwepo na majina yao hayakuwepo kuna tatizo gani ?inawezekana kamati ilipata updates sasa isiongeze yao majina na mengineo MBONA reason is plain there is no need to complain.
Mbona hakuna tofauti na kugomea mtihani kusema mtihani sio wenyewe mtihani unaujua.Au ndio hawa wanafunzi wa pale Morogoro waliogombea mtihani sio wenyewe leo ndio viongozi wetu.

Inaonekana walihonga kamati i-submit ripoti walioandaa wao na kamati haikufanya hivyo.Big up kama ndio hivyo hata sisi wananchi ukipewa takrima unakula na kura humpi safikama ilikuwa hivyo somo zuri tehe tehe!
Hawo kama kujisafisha wana uhuru wa kisafisha tena kwa njia hii hasa EL kama hana maslahi na Richmond basi akubali amefanya uzembe mkubwa(negligence) na kusababishia Taifa hasara kubwa,

AMA sio mzembe basi ana maslahi na Richmond thats it!.Ila ngumu kusema uzembe ngoma straight forward maslahi Richmond ni yao.Maana vyombo vya usalama lazima zilitonya issue ila vikatulizwa maana Ripoti inasema Richmond si jina geni ilishafanya usanii katika wizara hiyo hio ya nishati.

Pia Tanesco walipojalibu pinga wakanyanganywa madaraka ikaundwa tender board tiifu kwa mkuu tu ambayo haifuati criteria za kiufanisi bali waliset yao ya kizushi ATI bei yake nafuu napo ilikuwa uwongo Duh !
 
Hapa mkuu Mwanakijiji wamekupachikia na wewe ukakubaliana na misemo yao - haukua na tofauti na Bi Zakia aliposema " Barua ameamdika Bilali yeye ametia sign tu".

Kulikua na kamati moja ambayo report yake imesha somwa na mapendekezo yamesha tolewa. La msingi pia, wahusika wote walipewa nafasi pamoja na wabunge kutoa hoja zao juu ya Richmond report!

Pole - wamekupata leo!
 
na kichwa cha thread NDIO MISLEADING KABISAAAAAAAAAAAAAAAAA, sijui ndio kupata audience kubwa hata sielewi !
 
RA asitake kujiingiza katika matatizo mengine. Hilo suala la kuwa na ripoti nyingine hatoweza kulitetea kwa sababu Bunge linaitambua ripoti ya Mwakyembe kuwa ndiyo ripoti halali. yeye kama anayo nyingine, kwanza itabidi aje na ushahidi usio na mashaka kuonyesha kuwa hiyo aliyo nayo yeye ndiyo halali. Pili, atatakiwa aeleze imekuwaje yeye awe na ripoti halili halafu kamati iwe na ripoti feki. Kuthibitisha hilo si jambo dogo.

Pia, akumbuke kuwa suala la kuwepo kwa ripoti nyingine,. lilidokezwa hata na EL alipotakiwa kujieleza lakini alipobanwa aliamua kufuta kauli yake. katika maelezo yake, EL alisema Bungeni kuwa 'ripoti ilikuwa imejaa magazeti ya udaku'. Lakini ripoti ya mwakyembe haikuwa na magazeti ya aina hiyo. Inaonekana EL alikuwa na hiyo ripoti nyingine ambayo RA naye anayo.

Lakini alipotakiwa na Selelii aeleze hayo magazeti ya udaku yapo wapi katika ripoti yao, EL alifuta kauli hiyo.
Mimi ningebmshauri RA kuwa mkondo anaouchukua utazidi kumharibia badala ya kumjenga.
Ni ushauri wa bure tu.... YAKISHAMWAGIKA...
 
KADA MPINZANI GROW UP!
Hivi mpaka hapo ulipofikia bado unashindwa kutofautisha BANA NA BWANA?
KIJANA HUELEWEKI ALAFU UNASEMA WENZAKO HAWAELEWEKI KHA!
 
leo vichwa vya habari "Rostam, Rostam" ana jambo... subirini tu... Kuna kiongozi toka Wizara ya Madini ambaye ameandaa dossier ya kumsafisha Lowassa...
 
Du hivi hawa mafisadi wana nguvu kubwa eeh!! Sasa naamini kwamba nchi imeshaibwa na kuirudisha kwa wenyewe ni mambo ya Kenya na Zimbabwe!!!!!!! Na watanzania tulivyo tutaiacha hiyo itapita tuuuuu.....Hivi huu utumbo mpaka lini??????
 
Mimi nadhani huyo Mbunge ana maelezo yake binafsi aliyoandaa kuipaka kamati teule matope.Anataka kutuaminisha kuwa kilichosomwa na kamati ya Mwakyembe ni ubatili mtupu??maweeeee,huyu anadhalilisha hata bunge letu na pia kukidhalilisha hata chama chake cha sisiem.

Ripoti ya pili hiyo alipewa na nani?na aliwaoji nani? na alitumwa na nani?.Ripoti na tafiti zina utaratibu wake.Huwezi kwenda taasisi yoyote kufanya uchunguzi bila kibali na ndo maana Bunge likaunda hii kamati teule kwa mujibu wa sheria.Huyu vipesa alivyotuibia vinampa kiburi sana.Kwanza hawajatutangazia kama pesa zetu za RICHMOND na EPA amesharudisha??

Naamini watafiti(researchers) wanajua maana ya ripoti kusomwa mbele ya wadau mbalimbali inahitaji ushahidi na usimamizi maalum wakati wa uchunguzi.Hii ya kwake imepikwa wapi?HOAX AND A NIGHTMARE

,Mkuu wa kaya na usalama wa Taifa kama mmeshindwa kumdhibiti huyu Fisadi,tuachieni WANANCHI ni kazi rahisi,Mleteni Jangwani au Diamond asome hiyo ripoti nadhani tutamsikia na kumwona vema kabisa kuliko huko mbugeni.Na matokeo yake atawaleteeni TIBAIGANA na Vyombo vingine vya usalama.
 
Du hivi hawa mafisadi wana nguvu kubwa eeh!! Sasa naamini kwamba nchi imeshaibwa na kuirudisha kwa wenyewe ni mambo ya Kenya na Zimbabwe!!!!!!! Na watanzania tulivyo tutaiacha hiyo itapita tuuuuu.....Hivi huu utumbo mpaka lini??????

Sasa wale waliokuwa wanambeza Mwanakijiji hapa inabidi waombe msamaha au waonekane jinsi walivyo low and down low kwenye issues kama hizi!
 
Back
Top Bottom